other blog

Jumanne, 28 Julai 2015

Sentensi tisa za Boss wa Clouds FM, Joseph Kusaga kuhusu Tuzo ya Diamond Platnumz MTV MAMA 2015…

Jibu la Linah baada ya shabiki kuuliza uhusiano wake na kaka yake Zari (Bosi Mutoto).


Lina akiwa na kaka yake zari wakionekana kutomazana kwenye love swali ni je amemuacha amini,? Na je walisema ni tasa atazaa au?

kakaribishwa UKAWA, amejiunga nao? Majibu ni haya kwa Mbatia…

“ Watanzania wanataka mabadiliko,
wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta
nje ” >> Hii ni moja ya sentensi ambazo
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Monduli, Edward Ngoyai Lowassa
aliziongea Arusha May 30 2015
alipotangaza nia ya Kugombea Urais
kupitia CCM.

CCM ilikuwa na Wagombea zaidi ya 40
ambao walitangaza nia na kuchukua fomu
za Kugombea Urais 2015 lakini baadae
Chama hicho kikampitisha Dk. John
Pombe Magufuli kugombea nafasi hiyo,
baada ya hapo kukawa na headlines
nyingi sana kuhusu ishu ya Edward
Lowassa na UKAWA.
Viongozi wa Umoja wa UKAWA
wamekutana Dar na mmoja wa Viongozi
hao, James Mbatia amesema
wamekubaliana kumkaribisha Mbunge
Edward Lowassa ndani ya UKAWA na
wako tayari kumpa nafasi na kushirikiana
nae.
‘ UKAWA tunahitaji viongozi wenye sifa,
uwezo na weledi katika kulinda
kuheshimu na kusimamia rasilimali za
Taifa… Tunamwalika Edward Lowassa
ajiunge na UKAWA na tuko tayari
kushirikiana nae kuhakikisha tunaing’oa
CCM madarakani kwenye Uchaguzi Mkuu
ujao.. Tunaamini ana uwezo wa
kuhamasisha umma kuikataa CCM na
udhalimu wake ‘ >> James Mbatia .
Zimeandikwa stori nyingi kuhusu Mbunge
huyo kujiunga CHADEMA, kingine
kilichoibua maswali mengi ni ishu ya
UKAWA kuchelewesha kumtaja Mgombea
wao wa Urais… hapa ziko picha mbili
zilizoenea Mitandaoni zikimwonesha
Mbunge Edward Lowassa pamoja na
Viongozi wa UKAWA, kuna chochote
kinafuatia?



Jumatatu, 27 Julai 2015

Hatimaye dar foleni ipo palepale pamoja na kuongezwa kwa vbr ....


Dar es Salaam. Wakati mashine za
Biometric Voters Registration (BVR)
zikiongezwa kulingana na mahitaji,
zogo limezuka kwenye Kituo cha Mtaa
wa Saranga, Kimara baada ya
wananchi waliojiorodhesha kufikia
10,000 huku kukiwa na mashine tatu.
Zogo hilo lilitokana na baadhi ya
wananchi kufika kwenye kituo hicho
alfajiri jana, wakiamini wamewahi,
lakini walishangaa waandikishaji
kuanza kuwaita waliowawekwa viporo
tangu juzi. Baadhi ya wananchi
walisikika wakitishia kumpiga mmoja
wa wasimamizi wa kazi hiyo Sada
Mbonde, aliyepewa jukumu la
kuwapanga watu foleni.
Mbonde alisema wananchi hao
wanamuweka katika wakati mgumu
kwa kuwa waliosalia juzi
waliorodheshwa kwenye karatasi na
kuahidiwa kukamilishiwa taratibu za
kupata vitambulisho vyao jana.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Saranga,
Godwin Muro aliiomba Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC), kuongeza mashine
ili wananchi wengi waandikishwe kwa
kuwa wako zaidi ya 10,000.
Wakati huohuo; kutokana kugoma
kufanya kazi mashine za BVR,
wananchi wa Kata ya Kimara, Kituo
cha Shule ya Chekecheke ya Mtakatifu
Thomas walitaka kuwafukuza
waandikishaji baada ya kugundua
kuwa changamoto hiyo taarifa
zilikuwa hazifiki kwa uongozi husika ili
kutatua.
Wananchi hao ambao walifika kituoni
hapo alfajiri, walisubiri kwa muda bila
mafanikio na ilipotimu saa 8:00
mchana walimtaarifu mwenyekiti wao,
Rafael Mlay suala hilo.
“Nimezungumza na mkurugenzi na
ameniambia kuwa hana taarifa kama
kituo hiki kina mashine moja, anajua
kuwa zipo tatu, hivyo ameagiza
nyingine mbili zije mara moja. Zipo
njiani zinakuja, nawashauri
muendelee kusubiri ili mambo yaende
sawa,” alisema Mlay.
Baada ya kauli hiyo ya mwenyekiti,
wananchi hao waliwataka maofisa
waliotumwa na NEC waondoke kwa
madai kuwa wanawafanyia hujuma
kwa kuwa wengi wao ni wafuasi wa
chama pinzani.
Ilipotimu saa 10:30 jioni, Mlay
alilijulisha gazeti hili kwa simu kuwa
mashine moja imeongezwa na ile ya
mwanzo imetengenezwa hivyo
uandikishaji unaendelea kama
kawaida.
Hata hivyo, katika maeneo mengine
uandikishaji umeonyesha mafanikio
baada ya kuongezwa kwa mashine za
uandikishaji na kupunguza
msongamano wa watu.
Katika Kituo cha Shule ya Msingi
Segerea, mashine moja iliongezwa na
kufanya kituo hicho kuwa na mashine
mbili.
ADVERTISEMENT
Hali ilikuwa tofauti katika Kituo cha
Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa wa
Migombani kwa kuwa hakukuwa na
foleni.
Mkazi wa Mtaa wa Migombani, Kata ya
Segerea, Amina Ramadhan alisema
alifika kituoni saa mbili asubuhi, lakini
hadi saa nne asubuhi alipata
kitambulisho chake.
Katika vituo vya Shule ya Msingi
Jangwani na Kunduchi mashine
ziliongezwa kutokana na mwitikio wa
wananchi.
Ofisa Mtendaji wa mtaa wa huo, Said
Kikuwi alisema mwanzoni walikuwa na
mashine moja kwa kila kituo, lakini
waliongezewa nyingine mbili kutokana
na wingi wa watu.
Katika Kituo cha Salasala, Mbezi Beach
pia uandikishaji ulifanyika vyema
kutokana na kuongezwa mashine.
Foleni haikuwa kubwa kutokana na
utaratibu wa kuitwa majina kwa
namba.
Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Salasala,
Abdallah Mbupi alisema wakati
uandikishaji unaanza walikuwa na
mashine saba, lakini hadi jana
walikuwa na mashine tisa.
Mwandishi msaidizi katika Kituo cha
Zahanati ya Kawe, Jaston William
alisema wananchi pia wamekuwa
sehemu ya changamoto kubwa katika
utendaji wa kazi hiyo.
“Watu wanapeana namba mtaani
halafu wakija hapa asubuhi tukianza
kuwaandikisha wale tuliowakuta ni
ugomvi. Sasa tumeweka utaratibu wa
kutoa namba kwa watu 100 ambao
tunawaandikisha kwa siku moja
wanaobaki tunawaandika majina
wanaendelea na shughuli zao kwa
sababu tuna mashine moja,” alisema.
Mwandikishaji msaidizi katika Mtaa wa
Changanyikeni, Kituo cha Chuo cha
Takwimu, Vincent Emmanuel alisema
kazi inaendelea vizuri, lakini
changamoto kubwa ni nguvukazi.
“Kama kila kituo kingekuwa na fundi
wa hizi mashine ingekuwa vizuri. Kwa
sasa kila kata ina fundi mmoja, hivyo
ni rahisi kukuta muda mfupi baada ya
kuondoka katika kituo husika tatizo
jingine likajitokeza hivyo kuchukua
muda mrefu kurekebishwa au
kumsubiri fundi,” alisema.

Watangaza nia wilaya ya rombo katika nafasi ya ubunge hatimaye wamwaga sera zao katika ofisi ya kijiji cha marangu,, kitowo..imeandaliwa na,wasonga mrombo..

Ni mkutano mkubwa kabsa uliowakutanisha wanaolele na watangaza nia ktka viti vya ubunge pamoja na udiwani wa kwanza alikuwa ni Emanueli tumaini kavishe kutoka kata ya makiidi.. mgombea huyu ndiye mgombea pekee ambaye ni kijana, ana umri wa miaka 38 ana degree ya sheria na uhasibu kutoka sua.. ameeleza mikakati mbalimbali kama vile kupanua elimu kwa kutumia mifuko ya bunge... kutoa hati miliki na waatalamu wa ardhi,...kusaidia makundi ya vijana kupata mikopo kwa ajili ya mtaji...na mwisho ni kutumia taaluma yake kuwasaidia hasa vijana.




Mwingine aliyeomba ridhaa ya chama kumsimamisha kama mgombea ni engeneer bernard boniface kavishe.


Mwingine ni mwanamke anayejiita Nortburga alphonce maskini mwenye digrii ya uzamili ktk sheria na pia alishawahi kuwa mkurugenzi wa halmashauri mbalimbali na pia ndiye aliyechuana na mramba mwaka 2010..


Mwingine ni kalisti silayo tootoz yeye ni mfanyabiashara tarakea na moshi.. anajihusisha na biashara ya kuuza vitabu vya vyuo na vifaa vya maabara pia ni mwanakamati ktk chuo cha ukunga huruma..

Mwingine ni meja generali msitaafu meja gabrieli pius meela huyu ni mwanajeshi msitaafu, ni mzee machachari sana akiongea kwa mbwembwe zote kwamba ameeanda smg ya kuimaliza chadema cha msingi tumpe ridhaa hiyo ya kututetea



Mwingine ni mr colman samora kange huyu ni msomi ana degree tatu moja ya sheria nyingine ya utawala bora na katiba na nyingine ni ya...





Wote wanaomba saport yako ili wapewe ridhaa ya kuongoza kimbo la rombo kupitia chama cha mapinduzi ccm.. ahsante.

Jumapili, 26 Julai 2015

CHAMA CHA UKOMBOZI WA UMMA (CHAUMMA) CHAMTANGAZA MGOMBEA KITI CHA URAIS WA ZANZIBAR KUPITIA CHAMA HICHO.reAport by denic lyamuya..




Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma Zanzibar (CHAUMMA) Faki Salum Abdalla akitoa salamu za Chama hicho wakati wa Mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) wa kumtambulisha Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia chama hicho katikaUkumbi wa Umoja wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Mjini Zabnzibar.Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza mgombea nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia CHAUMMAkatika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar.Katibu Mkuu wa CHAUMMA Ali Omar Juma akitowa wasfu wa mgombea nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama hicho katikamkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar.Mgombea Kiti cha Rais wa Zanzibar kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Mohd MasoudRashid akijitambulisha na kueleza sera zake mbele ya waandishi wa habari katika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye Ulemavu Kikwajuni, Mjini Zanzibar. (kulia) mgombea mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho Issa Abass na (kushoto) Katibu Mkuu Ali Omar Juma.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar




Steps Entertainment kusaidiana na serikali kupambana na wahalifu wa filamu postead by mr kimario

Meneja Mkuu wa kampuni ya usambazaji filamu Steps Entertainment Bw.Jairaj Almoradan akifafanua jambo wakatiwa mkutano na Sekretarieti ya Bodi ya Filamu Tanzania,wakati wa makubalianoya Utekelezaji wa sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza ya mwaka 1976 kati ya wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo na Makampuni mbalimbali ya Filamu nchini.wa pili kulia ni Afisa uhusiano wa Steps Entertainment Bw. Cloude Ngalaba,wa tatu kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi.Joyce Fissoo ,wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Sekretarieti ya bodi ya Filamu Tanzania.Bi. Angela Ngowi. Mazungumzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Bodi ya Filamu jana jijini Dar es salaam.PICHA NA ANNA ITENDA MAELEZOMwenyekiti wa Pili Pili Entertainment Bw.Nilesh Bhatt akieleza jambo wakati wa mahojiano na sekretarieti ya Bodi ya Filamu Tanzania. wa pili kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi.Joyce Fissoo ,wa kwanzakulia ni Mwenyekiti wa Sekretarieti ya bodi ya Filamu Tanzania.Bi. Angela Ngowi. Mahojiano yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Bodi ya Filamu jana jijini Dar es salaam…………………………………..KAMPUNI ya usambazaji na utengenezaji filamu nchini Steps Entertainment imeahidi kushirikiana na serikali kupambana na wanaokiuka sheria ya filamu na michezo ya kuigiza ya mwaka 1976.Hayo yamesemwa jana na meneja Mkuu wa Steps Entertainment Bw. Jairaj Almoradan jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na Sekretatieti ya Bodi ya filamu Tanzania.Bw.Almoradan amesema kampuni yake haitapokea kazi za wasanii wasiofuata sheria kwa kutengeneza filamu zilizo kinyume na maadili na zilizo kinyume na sheria.Amesema kuwa sheria inawataka kutengeneza filamu zinazofuata maadili na kuwasilisha master kopi kwa ajili ya kuidhinishwa kuingia sokoni.“tutajitahidi kuwaeleza wasanii na tutakuwa wakali kutopokea filamu ambazo tunaona zipo kinyume na maadili na utamaduni wetu.”Amesema Bw. Almoradan.Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Bi. Joyce Fissoo amesema bodi imekuwa ikipata malalamiko kuhusiana na baadhi ya filamu kuwa kinyume na maadili ya Mtanzania.“Sisi kama bodi kazi yetu ni kukaguafilamu na matangazo yake kama yapo kimaadili na yamefata sheria ikiwa ni pamoja na kuzipa madarajafilamu hizo kabla hazijaenda sokoni.”amesema Bi.Fisso