other blog

Jumatano, 29 Julai 2015

Na katika teknologia.. Kampuni ya simu bandia za iphone yavamiwa


Kampuni iliyodaiwa kutengeneza simu bandia 41,000 aina ya Iphones kutoka kampuni ya Appleimevamiwa huko Uchina na watu 9 kukamatwa.Oparesheni hiyo ilishirikisha mamia ya wafanyikazi waliokuwa wakiandaa vipuri vya simu vilivyotumika kama simu mpya aina ya iphone tayari kuuzwa nje,huku simu hizo bandia zikizalisha kitita cha dola miloni 19.Kampuni hiyo iligunduliwa tarehe14 mwezi Mei lakini ikabainika katika mitandao ya kijamii na ofisiya usalama ya umma Beijing siku ya jummapili.Oparesheni hiyo ilianzishwa mwezi wa januari.Uchunguzi huo uliongozwa na kundi la mke na mumewe kaskazini mwa mji mkuu wa Uchina, kulingana na mamlaka yaBeijing.Walisema kuwa walidokezewa na mamlaka ya Marekani ambayo ilinasa simu hizo bandia .Ripoti hiyo inajiri wakati kuna msako wa bidhaa bandia unaotekelezwa na Uchina huku mamlaka hiyo ikiyashinikza makampuni kuweka nembo za ubora wa biadha.Uchina pia imekubali kufanya kazina mamlaka ya Marekani kupunguza kuwepo kwa bidhaa bandia zinazotoka nchi hizo mbili.Mshirikishe mwenzako

NA KTK MICHEZO CECAFA:Gor Mahia yafuzu nusu fainali


Mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini Kenya, Gor Mahia wameendeleza fomu yao bora katika kombe la CECAFA kwa kuilaza Malakia ya Sudan Kusini kwa magoli mawili kwa moja na kufuzu kwa nusu fainali.Beki wa Uganda, Godfrey Walusimbi ALIGEUKA KUWA MFUNGAJI NA KUTIA WAVUNI MAGOLI MAWILI.Mfungaji matata, Michael Olunga anayesakwa kutokana na ufungajiwake, alimuandalia pasi Walusimbi katika dakika ya 3 nayewalusimbi hakuchelea kuipa Gor uongozi.Gor ilizidisha uongozi wake kupitia Walusimbi KATIKA dakika ya 28 na kuwafanya mashabiki waGor waliokuwa katika uwanja wa kitaifa wa Dar Es Salaam.Kipa Boniface Oluoch ambaye amekuwa na fomu nzuri ya kutofungwa kwa zaidi ya mechi kumi kwenye ligi KUU NCHINI Kenya alifanya vyema langoni kwakuzaba shuti ya David Dada kunako dakika ya 13Kipindi cha kwanza kilikamilika Gor ikiongoza kwa magoli mawili kabla ya Thomas Jacob kuipa Malakia matumaini kwa kuelekezampira uliorushwa na Wisely Arasa's langoni katika dakika 66.Mkufunzi wa Al Malakia, Ramzi Sebit amelaumu usimamizi wa mechi kwa kupoteza.''Mwamuzi hakufaya usimamizi bora wa mechi'' alidai.Mpinzani wake, Frank Nuttal, anayeifunza Gor Mahia, amefurahia ushindi huo huku akiongeza kuwa wanalenga kufanya vyema katika nusu fainali.Gor, iliyoaga Makala ya kombe hilo mwaka uliopita sasa itamenyana na Al Khartoum ya Sudan.Al Khartoum, iliyochukua nafasi ya El Merreikh kuwakilisha Sudan kwenye kombe hilo, iliicharaza APR ya Rwanda kwa magoli manne bila jibu.

Miguel Herrera afutwa kazi


Kocha kutoka Mexico, Miguel Herrera amefukuzwa kazi baada ya kumshambulia mwandishi wa habari wa kituo kimoja cha luninga.Hatua hii ya kufukuzwa kazi kwa kocha huyo kunakuja ikiwa ni mbili tu baada ya kuongoza kikosihicho kwenye kombe la saba la medali ya dhahabu nchini Marekani.Miguel Herrera mwenye umri wa miaka 47 amekuwa akiiongoza timu hiyo ya Mexico kwa miaka16hadi sasa. katika utetezi wake Herrera amesema kuwa alifanyiwa fujo ndo maana akafikia hatua hiyo.

Boko harram wataisha asema buhari raisi wa nigeria...wasonga mrombo.


Msemaji wa rais wa Nigeria,Muhammadu Buhari,amesema amejipanga kupambana na kundi la kigaidi la Boko Haram kama litaendesha mashambulizi yake katika mipaka ya kimataifa.Msemaji huyo , Garba Shehu , aliiambia BBC kuwa tangu rais Buharia achaguliwe mwezi Mei amejipanga kutatua migogoro inayoikabili nchi hiyo tangu wananchi wa Nigeria wampe dhamana ya kuwaongoza. Cameroon, Chad na Niger wote wanashiriki katika kikosi kazi cha askari karibu elfu tisa , ambao wanatarajiwa kuwa tayari kwa mapambano mwezi ujao.Hata hivyo hapo jana kundi la wapiganaji wa Boko Haram walituma ujumbe kwa rais Buhariwakielezea kuwa wapo tayari kwa mazungumzo.

Jumanne, 28 Julai 2015

Wahamiaji ufaranza wakabiliwa vikali...


Kampuni wa usafiri inayofanya safari
zake kati ya Ufaransa na Uingereza ya
Eurotunnel imesema maelfu ya
wahamiaji wamekuwa wakijaribu
kuingia nchini Uingereza kupitia
usafiri huo.
Ripoti ya kampuni hiyo imebainisha kuwa
idadi ya majaribio ya wahamiaji kutaka
kuvuka mpaka kupitia usafiri aina hiyo ya
usafiri imeongezeka mno,kwani
wahamiaji hao watu hao wanajificha
kwenye magari ya mizigo,kupanda vizuizi
ilimradi tu waingine katika vyombo hivyo
vya usafiri na kuvuka.
Katika mkutano wa Mawaziri wa mambo
ya ndani wa Ufaransa na Uingereza
uliofanyika mjini London,mbinu za
pamoja kuweza kudhibiti wahamiaji hao
kuvuka zimejadiliwa na kuelezea hali
kuwa ni tatizo kubwa kwa sasa.
Wahamiaji hao kutoka nchi za Sudani na
Afghanstan waliopo bandari ya Calais
nchini ufaransa ya Calais ndiyo
waliobainika kutaka kuvuka kwenda
nchini Uingereza kwa mfumo huo, wengi
wa wahamiaji hao wanatoka nchini Sudan
na Afghanstan.
Mwaziri hao wa mambo ya ndani wa
Ufaransa na Uingereza wanasema
wamebaliana tutafanya kazi pamoja
kuwarejesha wahamiaji hawa ambao
wengi wao wanatoka Afrika Magharibi,na
kuwahakikishia watu kwamba safari za
aina hii haziwi lango kuu la wahamiaji
kuingia Uingereza.
Na tayari serikali ya Ufaransa imekwisha
anza kuweza jitihada za ziada kama idadi
zaidi ya askari,na uingereza itatoa kiasi
cha paundi million saba kuimarisha
ulinzi,japo kuwa Mbunge wa Bunge la
Ulaya Claude Moraes anasema haamini
kama hatua ya kuwarejesha wahamiaji
hao makwao kutasaidia kutatua tatizo
hilo

Obama sasa rasmi aonyesha kero kwa viongozi wa afrika watukutu wa madaraka... na benson mwAnga.


Rais wa Marekani Barrack
Obama,amewasuta viongozi wa Afrika
ambao wanaendelea kusalia
madarakani hata baada ya katiba
kutowaruhusu kuendelea kuwania
tena wadhfa wa urais.
Katika hotuba ya kwanza ya rais wa
Marekani kwa muungano wa Afrika katika
makao makuu ya umoja huo mjini Addis
Ababa,amesema kuwa Afrika haitapiga
hatua iwapo viongozi wake watakataa
kuondoka madarakani baada ya muda
wao kuisha.
Amemtaja hayati Nelson Mandela wa
Afrika Kusini, ambaye alikaa madarakani
kwa muhula mmoja tu wa miaka mitano
na anafahamika pakubwa kote duniani
huku akiheshimiwa kama kigogo wa bara
Afrika, tofauti na marais wengi
wanaoendelea kukwamia madaraka.
Ameongezea kuwa wakati waandishi
wanapofungwa huku wanaharakati
wakitishwa,demokrasia huwepo tu kwa
jina.
Akimnukuu shujaa Nelson Mandela
akisema kuwa unapoheshimu uhuru wa
wengine watu wote huwa huru.
Amesema kuwa ishara kuu ya maendeleo
katika taifa ni vile linavyowachukulia
wanawake wake.
Amewaambia viongozi wa Afrika kwamba
maendeleo ya bara hili yanategemea
demokrasia,uhuru na haki za
kibinaadamu.
Anasema kuwa muda umewadia wa
kubadilisha mtizamo wa Afrika kama bara
duni lenye kulemewa na umaskini na
mizozo.
Aidha amepongeza umoja wa Afrika AU
na shirika la Umoja wa mataifa katika
mapambano dhidi ya makundi ya
wapiganaji wa kiislamu kama vile, Boko
Haram kaskazini mwa Nigeria na Al -
Shaabab Afrika mashariki.
Amemtaja hayati Nelson Mandela wa
Afrika Kusini, ambaye alikaa madarakani
kwa muhula mmoja tu wa miaka mitano
na nafahamika pakubwa kote duniani
huku akiheshimiwa kama kigogo wa bara
Afrika, tofauti na marais wengi
wanaoendelea kukwamia madaraka.

Soma magazeti ya leo kwa headlines kalikali... kipitia hapa