other blog

Jumapili, 2 Agosti 2015

Yajue madhara ya kufanya kazi usiku....haya hapa naye riziki malya


Kumekuwa na utafiti ambao umekuwa ukiendelea kwa miaka kadhaa miongoni mwa watu wanaofanya kazi usiku na jinsi inavyoathiri afya yao vibaya.Ni swala la kuchemsha bongo kulingana na mwandishi Sarah Montague.Kwa miaka kadhaa sasa nimekuwa nikiamka usiku ili kwenda kazini, hio ndio gharama ya kufanya kipindi hiki na ni kipindi nafurahia kufanya.Nimekuwa nikijiuliza kama ntaathirika pakubwa kwa siku za baadae.Je, huenda kuamka kwangu usiku nikiwa sijatosheka usingizi ukawa unaathiri mwili wangu, shida inayoweza kutibiwa na kulala vyema?Mimi ni mmoja tu wa watu 3.5 milioni nchini Uingereza ambao hufanya kazi kwa zamu wengine wakifanya kazi kwa masaa mengi zaidi na kufanya kazi usiku woteNa si kwa wale wanaofanya kazi usiku pekee kwani watu zamani walikuwa wanalala kwa saa 8 lakini sasa wengi hulala saa 6 na nusuWatu wengi hudhania kulala ni starehe.Kengele yangu ikilia 3.25 asubuhi,mimi hujiambia nitalala zaidi baadae.Lakini kulala ni swala la umuhimukama tu kula na kupumua.Huo ni wakati wa akili zetu kufanya kazi kwa yale tumeyafanya katika nyakati za siku nzima na kutengeneza mawazo ya kumbukumbu, huku mwili ukidumishwa.Tumekuja kugundua kwamba hata iwapo wanaofanya kazi usikuhulala mchana, wao hulala masaayasiyofaa.Ili kujua mengiSarah Montague anafanya kazi usiku katika BBC redio 4.Imekuwa ikiaminika kuwa mili yetu huenda ikazoeshwa kufanya kazi usiku lakini kutokana na mtaalamu Proff Russel Foster kutoka chuo kikuu cha Oxford, utafiti unaonyesha kuwa mwili huwa hauzoei mabadiliko hayo.Wanaofanya kazi usiku huenda wakapata magonjwa kama vile ugonjwa wa kisukari aina ya 2, ugonjwa wa moyo na hata saratani.Wanasayansi wanasema mtu yeyote anayefika kazini mwendo wa saa kumi asubuhi, kama mimi,wana uwezo mdogo wa kutatua maswala sawa tu na mtu aliyekunywa pombe.

Arsenal kupambana na Chels


Ligi kuu ya Uingereza inaanza tena siku ya jumapili wakati ambapo mabingwa wa ligi hiyo Chelsea wanakutana na washindi wa kombe la FA Arsenal katika kombe la Charity Shield itakayogaragazwa katika uwanja wa Wembley.Mechi hiyo inajiri siku 64 baada ya kumaliza ligi hiyo na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Aston Villakatika fainali ya FA.Pende zote mbili hazijafanya usajili mkubwa katika msimu huu ijapokuwa kipa Petr Cech ataanzishwa dhidi ya timu yake yazamani Chelsea.Chelsea vilevile inaweza kumuanzisha mchezaji wao mpyaRadamel Falcao.Falcao mwenye umri wa miaka 29alihudumu katika kilabu ya Manchester United msimu uliopita lakini hakuweza kutamba kwani aliweza kufunga mabao 4 katika mechi 29 alizocheza pekee.Siku ya jumapili itazikutanisha timu hizo mbili huku mkufunzi waArsenal akitarajia kuishinda timu inayofunzwa na Mourinho kwa mara ya kwanza kati ya mechi 13 walizocheza huku wakufunzi hao wawili tayari wakitofautiana.Mourinho alisema kwamba Arsenal imetumia fedha nyingi msimu huu ikilinganishwa na Chelsea katika kipindi cha miaka kadhaa iliopita ,huku Wenger akijibu kwamba hasikizi kile watu wanachosema ama kufikiri.

ichaCECAFA:Gor Mahia kuchuana na Azam


Kilabu ya Azam kutoka Tanzania imefuzu katika fainali ya ombe la Kagame CeCAFA baada ya kuindoa KCCA ya Uganda kwa baomoja kwa bila katika mechi ya nusu fainali ya pili iliochezwa katika uwanja wa kitaifa wa Dar-es-Salaam nchini Tanzania.Hatua hiyo inaaminisha kwamba Kilabu ya Gor Mahia ya Kenya itakabiliana na Azam katika fainaliya Kombe la CECAFA.Azam ilihitaji bao la dakika za mwisho lililofungwa na Farid Musa kuilaza KCCA kutoka Uganda na kufuzu katika awamu ya kilele cha kombe hilo.Fainali hiyo itachezwwa siku ya jumapili katika uwanja huohuo.Gor Mahia ilifuzu katika fainali baada ya kuicharaza kilabu ya Al Khartoum kutoka Sudan 3-1 kupitia mabao yaliofungwa na Michael Olunga,Innocent Wafula na Meddie Kagere.K'Ogalo sasa itashiriki katika fainali ya kwanza tangu mwaka 1985.

Mwanariadha hatari sana David Rudisha ashindwa nyumba


Bingwa wa mbio za Olimpiki anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 800 David Rudisha alishindwa kwa mara ya kwanza nyumbani Kenya.Rudisha mwenye umri wa miaka 26,alichukua nafasi ya pili nyuma ya mwanariadha Ferguson Rotich mwenye umri wa miaka 25 jijini Nairobi.Hatahivyo Rudisha atashiriki katika mashindano hayo yatakayofanyika Beijing baadaye mwezi huu.''Nimeshtushwa na kushindwa kwangu lakini ninafurahi niko katika timu ya taifa'', alisema Rudisha ambaye alidai kwamba bado haijamarika vilivyo.Rudisha alishinda ubingwa wa mita 800 mjini Daegu mwaka 2011 lakini akakosa riadha za ubingwa mjini Moscow kupitia jeraha alilopata.''Bado sijafanya zoezi lakuimarisha kasi yangu,ijapokuwa niko aslimia 90 tayari.Kwa sasa nimesalia na wiki tatu kuimarisha kasi aliongezea.

Umesikia hii mwanzilishi wa fb kuwa baba...


Mwanzilishi wa mtandao wa facebook Mark Zickerberg na mkewe Priscilla Chan wanatarajiamtoto wa kike.Wawili hao walitangaza katika ujumbe wao katika ukurasa wa facebook wa bwana Zuckerberg, ''Priscilla na mimi tuna habari njema:''Tunatarajiwa mtoto wa kike'', aliwaandikia takriban watu milioni 33 wanaomfuata katika mtandao huo.Katika ujumbe wake Zuckerberg mwenye umri wa miaka 31 alifichua kwamba mkewe aliharibikiwa na mimba mara tatuhapo awali,lakini akongezea kwamba hatari ya kuharibikiwa na mimba nyengine kwa sasa iko chini sana.Amesema kwamba wameamua kutoa tangazo hilo ili kuwapa watu wanaokabiliwa na tatizo kama hilo motisha wa kuendelea kuwa na subra.

Eti generali wa raisi wa burundi auwawa kisa shuka nayo...


Mamlaka nchini Burundi inasemakuwa jenerali Adolphe Nshimirimana ameuawa.Imeripotiwa kuwa alifariki katika shambulizi la roketi katika gari lake kaskazini mwa mji mkuu wa Bujumbura.Jenerali Adolphe Nshimirimana alikuwa rafiki wa karibu wa rais Pierre Nkurunziza.Hata baada ya kuondolewa kama afisa wa idara ya ujasusi mwezi Novemba mwaka jana alikuwa akionekana na wengi kama mwenye ushawishi mkubwa nchini humo.Alishtumiwa kwa kusimamia oparesheni za kukabiliana na waandamanaji baada ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza kwamba atawania muhula wa tatu mbali na kuhusika pakubwa katika kuzima jaribio la mapinduzidhidi ya rais huyo.Kwa sasa wengi wana hofu ya hatua itakayochukuliwa na wafuasi wa Nshimiriman

Vijana rombo hawasikii lolote kuhusu pombe za kienyeji ... swali ni je wamefunga ndoa na hizo pombe...?




Ni masikitiko na wala sio raha,, vijana wakionekana kuathiriwa na hizo pombe za kienyeji. Kwa nini nasema wameathirika? Inasikitisha kila muda vijana wamekaa vijiweni tena vya mbege na kimoraly .. cha kustaabisha serikali imeuchunA juu ya suala hilo huku vijana wakiendelea kuchoka kuliwa na mafunza na kuchafuka kupita maelezo... kwa kweli kwa mwenendo huu tutapoteza sana nguvu kazi kwa taifa...