other blog

Jumamosi, 5 Novemba 2016

Joyce ndelchako afumuka makubwa kuhusu bodi ya mkopo na aamuru kuwa wote walioomba mkopo wapatiwe. shuka nayo hii..

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya
Juu (HELSB), imeagizwa
kuhakikisha kuwa fedha zote
zilizotengwa kwa ajili ya
mikopo ya wanafunzi
wanaoendelea na masomo
zinapelekwa vyuoni ifikapo
leo.
Agizo hilo lilitolewa bungeni
jana na Waziri wa Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Ufundi,
Profesa Joyce Ndalichako
baada ya wabunge mbalimbali
kuomba miongozo kwa Spika
kuhusu kuwapo kwa wanafunzi
wengi waliokosa mikopo kwa
mwaka wa fedha 2016/17.
Mwongozo kwa Spika ulitiliwa
mkazo na Mbunge wa Chalinze
(CCM), Ridhiwan Kikwete
aliyeeleza kuwapo taarifa
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM) kuwa
wanafunzi wanataka kugoma
kwa kukosa fedha za mikopo.
Kutokana na miongozo hiyo,
Mwenyekiti wa Bunge, Najma
Giga aliitaka Serikali kutoa
maelezo.
Akitoa kauli ya Serikali, Profesa
Ndalichako alisema fedha za
mikopo kwa ajili ya wanafunzi
zilikwenda vyuoni wiki moja
iliyopita.
“Tatizo lililotokea kwa UDSM
sijui kama walidanganyana au
la lakini hawakujaza fomu.
Serikali haitatoa mkopo kwa
mwanafunzi ambaye hajajaza
fomu. Na waliosaini leo
wataingiziwa fedha zao kwenye
akaunti na vyuo,” alisema.
Kuhusu wanaoendelea na
masomo, Profesa Ndalichako
alisema wanafunzi wote
wanufaika na wanaoendelea na
masomo wataendelea kupatiwa
mikopo kama ilivyokuwa
mwaka uliopita.
Alisema wanafunzi ambao
vyuo vyao vimewasilisha HELSB
taarifa za matokeo, Bodi
imekwishawatumia fedha
vyuoni kwa ajili ya kuwapa
mikopo wanafunzi hao.
Hata hivyo, alisema taratibu za
kuwabaini wanafunzi wenye
sifa zinaendelea na wasio na
sifa wataendelea kuondolewa
kupata mikopo.
Pia, alikiri kuwa ucheleweshaji
wa matokeo ya wanafunzi
wanaoendelea na masomo
umeathiri kasi ya kutuma fedha
vyuoni.
“Wizara yangu imekwishaagiza
vyuo vyote ambavyo
havijawasilisha matokeo ya
mitihani ya wanafunzi wao kwa
mwaka wa masomo uliopita,
kufanya hivyo mara
moja,” alisema.
Ndalichako alisema hadi
kufikia Novemba 3 mwaka huu,
Sh71.042 bilioni
zilikwishatumwa vyuoni kwa
ajili ya wanafunzi wa mwaka
wa kwanza na wanaoendelea
na masomo.
Akizungumzia utoaji wa
mikopo kwa mwaka wa fedha
2016/17, Ndalichako alisema
katika mwaka huo, Sh483
bilioni zimetengwa na
zimelenga kutoa mikopo kwa
wanafunzi 119,012, wanafunzi
93,295 wanaoendelea na
masomo na wa mwaka wa
kwanza 25,717.
Ndalichako alisema katika
mwaka wa fedha 2016/17
wanafunzi 58,010 walidahiliwa
na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU)
na orodha yao iliwasilishwa
HELSB na hadi Novemba 2,
mwaka huu, wanafunzi 21,190
wa mwaka wa kwanza
wamepewa fedha. Kati yao
4,321 ni yatima, 118 wenye
ulemavu na 87 ni waliosoma
sekondari kwa ufadhili wa
taasisi mbalimbali.

Jumapili, 4 Septemba 2016

mh.... hi ni hatari. CCM watashia kuanzisha ukuta .. Nimeamin kwamba wapinzani ndo mafisadi wakubwa... Hongera magufuli.

WABUNGE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameingia katika mzozo mkubwa na Rais John Magufuli, na sasa wameanza Job Ndugai, kumlazimisha Spika wa Bunge, awanusuru, MwanaHALISI linaweza kueleza.
Habari kutoka Ikulu, Ofisi ya Spika na Kamati ya Wabunge wa CCM, zinasema wabunge hao wamejiapiza kuwa Ndugai na Rais Magufuli wamekalia moto.
Sababu kuu inayotajwa ni hatua ya serikali, kwa amri ya Rais Magufuli, kuhoji na kufikisha mahakamani baadhi ya wabunge wa CCM wanaotuhumiwa kuomba rushwa kutoka kwa taasisi wanazosimamia.
Wabunge wa CCM waliofikishwa mahakamani ni Kangi Lugola (Mwibara), Victor Mwambalaswa (Lupa), na Suleiman Sadiq (Mvomero). Wanatuhumiwa kwa kwa kosa la kuomba rushwa ya milioni 30 kutoka kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Gairo ili wampendele katika kukagua hesabu za halmashauri yake mwaka 2015/16.
Mwingine ni Richard Ndassa (Sumve), ambaye anatuhumiwa kwa  kushawishi na kuomba rushwa ya Tsh 30 milioni kutoka kwa Felchesmi Mramba, Mtendaji Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)  ili amsaidie kuwashawishi wajumbe wengine wa Kamati ya Mtaji na Uwekezaji kupitisha bila kipingamizi taarifa ya TANESCO kwa mwaka 2015/2016.
Taarifa zinasema kuwa hadi Ijumaa iliyopita, Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) ilikuwa imehoji wabunge wengine 18 wa CCM, na ilikuwa imeshakamilisha taratibu zote za kuwafikisha mahakamani.
Miongoni mwa wabunge hao ni Martha Mlata (Viti Maalumu), Raphael Chegeni (Busega), Margareth Sitta (Urambo Mashariki), Mary Mwanjelwa (Viti Maalumu), Edwin Sanga (Kondoa Mjini). Majina mengine hayakupatikana hadi tunakwenda mitamboni.
Baada ya taarifa za kufikishwa mahakamani wabunge hao kuanza kuenea, kundi la wabunge wa CCM linadaiwa kumzonga Ndugai, wakimtaka awasimamie wabunge wa chama chake, asiruhusu wadhalilishwe.
Watoa habari wetu wanasema wabunge walimweleza Ndugai kuwa kitendo cha serikali kudhalilisha wabunge wa CCM kitaondoa umoja wao wa kutetea serikali, na kitaathiri msimamo wao katika umoja wa wabunge wa chama chao.
“Mweleze rais asitudhalilishe, sisi ni wabunge wa chama chake; asitafute sifa zake peke yake,” mbunge mmoja kijana alinukuliwa akimweleza Ndugai.
Kabla hata Ndugai hajawasiliana na rais kuhusu hoja za wabunge, taarifa zinasema rais mwenyewe alipata taarifa hizo kutoka kwa “vijana wake” ndani ya wabunge hao.
Mtoa habari kutoka Ikulu ameeleza gazeti hili kuwa Rais alipompigia simu Ndugai alizungumza kwa ukali, “hiyo ni mijizi, acha ifungwe tu.”
Gazeti hili lilipohitaji ufafanuzi wa Ndugai kuhusu masuala haya alithibitisha kuwa wabunge wake  wameshahojiwa na TAKUKURU, lakini akagoma kusema alichoambiwa na rais.
“Ni kweli kuna wabunge 18 wameshahojiwa na Takukuru. Hata hivyo, tumeshindwa kuwa na maelezo ya pamoja kwa kuwa kuna wengine wameitwa kama mashahidi, na wengine wamehojiwa kama watuhumiwa,” Alisema.
Alisema kilichotokea ni kwamba wabunge hao wamekuwa wanaitwa kwa nyakati tofauti, kwa sababu tofauti. “Mwingine anaitwa leo anahojiwa kwa tuhuma, mwingine anaitwa kesho kwa ushahidi pengine baada ya kutajwa na mwenzake,” alidokeza.
Baadhi ya wabunge wa CCM wameliambia gazeti hili kuwa kuna kesi zinatengenezwa kisiasa, hivyo wanajipa muda kuliweka sawa suala la tuhuma zinazowakabili.
Hata hivyo, taarifa zinasema wabunge wameikamia serikali, na wengi wao wanajiapiza kuunga mkono hoja za wapinzani kama namna ya kumkomoa Rais Magufuli.
Taarifa hizo hizo zinasema rais mwenyewe baada ya kusikia vitisho vya wabunge wa CCM, amemwambia Ndugai, “kama watatunisha misuli nitavunja bunge, turudi kwenye uchaguzi, tuone watarudi wangapi miongoni mwao.”
Taarifa hizi zinakuja ikiwa ni wiki moja tangu Spika kuahidi kuwa suala hilo litazungumzwa vizuri ndani ya Bunge kwa kuzingatia kanuni wala si mtaani. Source ni mwanahalisi..

Jumatano, 3 Agosti 2016

Mashirika ya kitawa kwa wote mnaotaka kuwa watawa

karibuni wote mjiunge na utawa maisha matakatifu ni maisha ya kazi na sala wanaotaka kuwa mabruda ... waandike barua kwa anuani ifuatayo mkurugenzi , scim brothers, s.l.p 29 Tosamaganga, Iringa. kumbuka kigezo uwe tu hujaoa na pia uwe umehitimu kidato cha nne. pia lipo shirika la mtakatifu carmel lilopo bunju kwa  malezi ya kipadre wote wenye nia mnaombwa kutuma maombi yenu kwa mkurugenzi tz kwa mawasiliano zaidi watumie email carmelitestz@gmail.com na Kwa upande wa masisita soma kibandiko cha mtakatifu consolata missionery kwa malezi ya kisista yaani utawa wa kwanza na pia shirika la mtakatifu charles borromeo

kumbuka mabruda na masista lazima uwe mhitimu wa kidato cha nne. pia uwe hujaoa wala hujazaaa  na kwa upande wa upadre lazima uwe mhitimu wa kidato cha sita na kufaulu uwezo wa kwenda chuo kikuuu ... karibuni utawani tujifunze maisha halisi ya bwana wetu yesu kristo.. Tumsifu yesu kristo .... kwa maelezo zaidi usisite kunipigia simu 0743719830

Alhamisi, 9 Juni 2016

UMMA KUHUSU KUFUNGWA KWA MUDA WA KUPOKEA MAOMBI YA UDAHILI WA KOZI ZA CHETI, DIPLOMA, DIPLOMA YA JUU NA SHAHADA YA KWANZA KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CAS) UNAORATIBIWA NA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

 
Tarehe 3 Juni 2016 ilikuwa siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya udahili wa kozi za Cheti, Diploma, Diploma ya Juu na Shahada ya Kwanza kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) unaoratibiwa na NACTE.
Baraza linapenda kuwaarifu waombaji udahili wa kozi tajwa hapo juu na umma kwa ujumla kuwa, kwa sasa maombi yote yaliyowasilishwa mpaka tarehe 3 Juni 2016 saa sita usiku yameanza kuchambuliwa kwa ajili ya kuchagua waombaji wenye sifa stahiki. Zoezi la kuchambua waombaji udahili na hatimaye kuchagua waombaji wenye sifa stahiki na waombaji hao kuidhinishwa na mamlaka husika na kutangazwa litachukua muda wa wiki nne (4) kuanzia tarehe 3 Juni, 2016.
Baraza linatambua uwepo wa waombaji wapya na baadhi ya waombaji walioshindwa kuwasilisha maombi yao kupitia mtandao ilipofika tarehe 3 Juni 2016. Waombaji wa namna hii na wengine wanaopanga kuwasilisha maombi yao kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) wanaombwa kuwa na subira mpaka hapo majina ya waombaji waliowasilisha maombi yao kabla ya kufungwa kwa mfumo watakapotangazwa.
Baada ya kutangazwa majina ya waombaji waliochaguliwa, Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) utafunguliwa tena kwa ajili ya kujaza nafasi za udahili ambazo zitakuwa hazijajazwa na waombaji waliowasilisha maombi yao kuanzia tarehe 4 Machi, 2016 hadi tarehe 3 Juni 2016.
Baraza linatarajia kufungua tena Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kwa ajili ya kozi za Cheti, Diploma, Diploma ya Juu na Shahada ya Kwanza wiki ya mwishoni mwa mwezi wa Sita, 2016.
Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
NACTE
Tarehe: 9 Juni, 2016

Jumapili, 29 Mei 2016

AJALI MBAYA YATOKEA MAKERERE BARABARA YA KUSHUKA MWIKA ILIYOHUSISHA NOA ITOKAYO TARAKEA KWENDA MOSHI





Mungu ibariki Tanzania mungu iokoe Tanzania .. yatupasa kutubu kila wasaa maana hatujui siku wala saa kitakapo tokea kiama.. AJALI HIYO HAIKUPONYESHA HATA MMOJA WOTE KUMI NA TANO WALIKUFA WENGI WAKIWA NI WA TARAKEA.. CHANZO CHA AJALI HIYO INASEMEKANA KUWA NI HITILAFU YA GARI ILIPOFELI BREAK NA KUSABABISHA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA MARA KADHAA .. WALIOSHUHUDIA AJALI HIYO WANASEMA KUWA ABIRIA KUMI NA MBILI WALIAGA DUNIA PAPO HAPO NA WENGINE WATATU WALIFIA KCMC ... YA MUNGU NI MENGI SIFA NA UTUKUFU ZIRUDI KWAKE .. YEYE NDIYE MUUMBA ..YEYE NDO ANACHUKUA APEWE SIFA MILELE...ROHO ZA MAREHEMU WOTE WAPATE REHEMA KWA MUNGU WAPUMZIKE KWA AMANI.

Jumatano, 18 Mei 2016

Marketers, Project Manager, Teachers

Nafasi za kazi ardhi chuo kikuu.. Omba sasa



VACANCY ANNOUNCEMENT
Ardhi University has vacant position in
the Administrative cadre.
The University subscribes to the policy
of an equal opportunity employer and
therefore invites applications from
candidates who are interested to work
in a thriving University environment
and have the requisite skills,
Qualifications and experience for
various positions as indicated below;
Job Title: Insurance Manager (1
Post) Re -advertised)
Required Qualifications:
• Holder of first Degree / Advanced
Diploma in Insurance or a
• Diploma in Business Field plus a
Certificate in Insurance or any other
recognized professional
Insurance qualifications. AND 3 years
post qualification experience in the
Insurance Industry at,
managerial or executive position.
Duties
i. To run a department for handling
Insurance business at Ardhi
University.
ii. To develop competitive quotes, to
prompt of documents promptly, and
proper advice at
the time of claims.
iii. To maintain follow-ups of claims of
their prompt settlement by Insurance.
iv. To develop and nurse relationship
with clients through, physical visits
and various
communication platform.
v. To enhance public awareness of the
Agency through various
communication strategies.
vi. To build support with Institutions in
Tanzania in order to have their
Insurance routed
through ARU’S Insurance Agency.
vii. To maintain an accurate and
complete customer database and
networking with
construction firms in order to solicit
business on engineering for ARU’S
Insurance
Agency.
Duty Station for the advertised post is
Dar es salaam.
GENERAL REQUIREMENTS FOR ALL
APPLICANTS
1. All academic awards should be
from recognized Universities and
Institutions.
2. All applicants with certificates from
foreign Universities should have the
certificates verified by the Tanzania
Commission for Universities (TCU)
3. All applicants must submit signed
application letters accompanied with
the following:
i) Copies of relevant academic and
professional certificates;
ii) Three names and complete
addresses of referees;
2iii) Current CV
4. Age limit: Not above 35 years
5. Applications should reach the
University by using the address below
not later than 5Th May, 2016.
6. Only short-listed applicants will be
contacted.
7. Those applied during the first
advertisement need not to apply
APPLICATION INSTRUCTIONS:
Interested applicants should submit
their applications to the undersigned:
The Deputy Vice Chancellor
(Planning, Finance and
Administration)
Ardhi University
P.O. Box 35176
DAR ES SALAAM