other blog

Jumapili, 26 Julai 2015

TCRA: TV ZENYE MIGONGO NA MATUMBO MAKUBWA PIA ZITAPOKEA MATANGAZO YA DIGITALI reaported by mr kimario..

Na Mohammed Mhina, ZanzibarImeelezwa kuwa TV zote zikiwemo zile zenye migongo, matumbo na viuno virefu zote zina uwezo sawa wa kupokea matangazo ya digitali na Watanzania waepuke uvumi wa watu wachache wanaodai kuwa TV za zamani hazitapokea zitafutwa mara Tanzania itakapoingia kwenye mfumo wa Digitali.Wito huo umetolewa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano hapa nchini TCRA ambaye pia na Mratibu wa Ofisi za Kanda Bw. Victor Nkya, wakati wa mkutano wa Wataalamu wa Mawasiliano ya Habadi kwa njia ya digitali kutoka nchi za SADC unaojadili umuhimu wa mfumo wa Digitali.Bw. Nkya amesema kuwa wananchihawana haja ya kuwa na hofu juu yaTV walizonazo zikiwemo zenye matumdo na migongo mikubwa kuwa hazitaweza kupokea matangazo ya televishen katika mfumo mpya wa digitali.Amesema kutokana na watu wengi kutumia televishen za Analojia, ni lazima kila mmoja wetu awe na kingamuzi na kazi ya Mamlaka ya mawasiliano ni kuwajengea wananchi matumaini na kuepuka kudanganywa.Kwa siku za hivi karibuni baada ya Tanzania kuridhia mabadiliko ya mfumo wa Digitali, wananchi wamekubwa na wasiwasi wakidhanikuwa huo ndio mwisho wa tv za zamani.Awali akifungua Mkutano huo wa siku tatu hapa mjini Zanzibar, Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Mh. Rashid Suleiman, amewataka wananchi kukabiliana na changamoto mbalimbali zitakazojitokeza wakati wa mabadiliko ya kutoka katika mfumo wa analojia na kuingia katika digitali.Amesema ni vema wananchi wakahama mapema kutoka katika mfumo huo wa zamani ili kuepuka usumbufu wakati yatakapotokea mabadiliko hayo kwani hakutakuwa na muda wa nyongeza kama Watanzania walivyozoea.Na kuna umuhimu wa wananchi pia kusikiliza maelekezo ya wataalamu badala ya kusikiliza propaganda za watu wasio na ujuzi juu ya teknolojia hiyo.“Watanzania hawana haja ya kuogopa na badala yake wajiandae kujipatia vingamuzi na kinyume cha hivyo watashindwa kupata matangazo ya televishen kama wanavyotarajia.” Alisema Waziri.Amesema kila mabadiliko yana hasara na faida zake, lakini kwa mabadiliko ya kutoka katika mfumo wa analojia kwenda digitali, kuna faida kubwa na moja ya faida hizo ni kuwawezesha watu wote kupokeamatangaza sawa na yenye ubora unaofanana na kwa wakati muafaka.Mkutano huo wa siku tatu unazishirikisha nchi zote za Jumuiyaya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC ikiwemo Angola, Afrika ya Kusini, Malawi, Namibia, Botswana,Swazlland, Lesotho, Msumbiji na wenyeji Tasnzania.

WASANII WAFUATE TARATIBU WANAPOENDA NJE YA NCHI- BASATA reaport by mr kimario


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa nchini linawakumbusha wasanii wote nchini kuhakikisha wanafuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo wanapokwenda njeya nchi kufanya maonesho au kushiriki shughuli yoyote ya Sanaa ili kuepuka matatizo na mikanganyiko mbalimbali inayoweza kujitokeza.Kwa mujibu wa taratibu zilizopo, msanii yeyote anapokwenda nje ya nchi anapaswa kujaza fomu maalumu inayotolewa na BASATA na baadaye kupewa kibali bure (bilagharama yoyote) ambacho mbali nakueleza wapi msanii anaelekea kinaeleza kwa kina tarehe ya kuondoka kwa msanii na ile ya kurudi nchini.Kutokana na kukua kwa sekta ya Sanaa nchini hususan muziki na filamu wasanii wengi wamekuwa wakipata fursa ya kwenda nje ya nchi kufanya maonesho na shughulizingine za Sanaa hivyo suala la kufuata sheria, kanuni na taratizu zakupata vibali vya kwenda nje ya nchini muhimu sana ili kuhakikisha kwanza; safari zao zinakuwa na baraka ya moja kwa moja kutoka Serikalini, pili kusaidia upatikanaji wa takwimu sahihi za wasaniii wanaokwenda nje ya nchi, tatu usalama wa wasanii wetu na mwisho, kuwakabidhi bendera ya taifa kama ishara ya uwakilishi na ubalozi wa nchi yetu katika mataifa wanayoyatembelea.BASATA limekuwa likiwaelekeza wasanii wote kuomba vibali vya kwenda nje ya nchi na kuripoti katika balozi zetu zilizoko kwenye mataifa mbalimbali ili kuhakikisha wanakuwa na wenyeji katika nchi husika kwa lengo la kujitambulisha pia kupata msaada pale kunapotokea tatizo lolote linalohitajiutatuzi wa Serikali.Dunia imekuwa na matukio mengi ya kiusalama ni vema kuchukua tahadhari hasa ikizingatiwa kazi za Sanaa huambatana na mikusanyiko mikubwa ya watu hali ambayo inaweza kuzaa matatizo kwa wasaniiwetu wakiwa nje ya nchi bila kuwa na nyaraka stahiki.Baraza la Sanaa la Taifa linatambua kwamba wasanii wanapokwenda nje ya Tanzania kwa lengo la kufanya kazi ya Sanaa wanakwenda kuipeperusha bendera ya Taifa letu,kwa mantiki hii ni mabalozi wa nchi.Hivyo basi, lazima wawe wazalendo,wajivunie utanzania na kuiwakilisha vyema nchi yetu.Ieleweke kwamba Serikali inafarijikana kupata heshima kubwa inapoonawasanii wetu wakivuka nje ya mipaka na kwenda kupata mafanikio kwenye majukwaa ya kimataifa suala ambalo ni kuitangaza Tanzania kupitia Sanaa na Utamaduni baada ya kuzingatia taratibu zote. Ndiyo maana kupitia mitandao yake ya kijamii na hata katika programu ya Jukwaa la SanaaBASATA limekuwa likihamasisha wadau wa Sanaa kuwaunga mkono wasanii na kuwapigia kura kunapokuwa na shindano lolote linalohitaji ushindi wa kura (popularvote). Aidha, BASATA limekuwa likiandika taarifa kwenye vyombo vya habari kumpongeza msanii yeyote anapofanya vizuri nje ya mipaka ya nchi yetu.Ni sababu hii ndiyo imelifanya BASATA muda wote kuwasisitiza wasanii na menejimenti zao kutambua wajibu wao kwa serikali hasa katika kuhakikisha wanafuata taratibu zote zilizopo na kutoa taarifa hitajika serikalini ili kuepuka mikanganyiko na sintofahamu inayoweza kujitokeza.Lengo ni kuhakikisha kupitia taarifa sahihi zinazokuwa zimetolewa na menejimenti za wasanii au wasanii wenyewe pia kupitia taarifa zilizopo kwenye vibali vya kwenda nje kwa wasanii husika, Serikali nayo inajipanga ipasavyo katika kuhakikisha wasanii wetu wanaagwa na baadaye kupokelewa kwa heshima wanaporejea nchini.BASATA linaamini kwamba haileti picha nzuri na kwa kweli inashusha morali wasanii wetu wanaporudi nyumbani na mafanikio makubwa pasi na mapokezi ya Kiserikali kwa sababu tu menejimenti za wasanii zinashindwa kujipanga kwa maana ya kuzingatia taratibu zilizopo na kutoa taarifa stahiki za lini msanii atarejea na wakati gani ili mamlaka husika ifanye utaratibu wa mapokezi.Serikali kupitia BASATA imefanya mapokezi stahiki kwa wasanii Peter Msechu aliposhinda shindano la Tusker Project Fame, Mtunzi wa filamu Timoth Konrad wakati filamuyake ya ‘Dogo Maasai’ iliposhinda tuzo nchini Marekani na hivi karibuni imefanyika kwa Msanii Mayunga aliyeshinda shindano la Airtel Tracing Star. Aidha, washiriki wote wa mashindano ya urembo wamekuwa wakifanyiwa hivyo kamailivyo kwenye sekta ya michezo.BASATA linatoa wito kwa wasanii kudumisha upendo baina yao na kuhakikisha wanakuwa na ushirikiano pia mawasiliano ya karibu na Serikali muda wote kwani zipo mamlaka ambazo zipo kwa ajiliya kusimamia sheria, kanuni na taratibu katika tasnia ya Sanaa.Ni wazi kwamba kama wadau wote wa sanaa wakielewa utaratibu huu basi sekta ya Sanaa ambayo kiasili ni ya upendo, mshikamano na amani itaendelea kukua katika mwenendo mwema na kuwa yenye tija zaidi kwa wasanii wenyewe pamoja na jamii kwa ujumla. Wasanii tudumishe upendo, amani na mshikamano.Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini.Godfrey MngerezaKATIBU MTENDAJI

Ndoa Uhispania sasa mpakamiaka 16 reaported by mabere gudlack


Umri wa kuoana nchini Uhispania sasa ni miaka 16 kulingana na sheria ya nchiUhispania imeongeza umri wa ndoa kutoka miaka 14 hadi 16 , ikiwa ni nchi iliyoidhinisha umri wa chini zaidi wa kuolewa barani Ulaya.Kabla ya kupandishwa kwa miaka,wavulana na wasichana wangeweza kuolewa wakiwa na miaka 14kwa ruhusa ya hakimu.Mabadiliko hayo yamekuja miezi kadhaa baada ya serikali kuongeza miaka ya idhini ya kuolewa kutoka miaka 13 hadi 16.Serikali ilitangaza azma yake ya kufanya marekebisho ya sheria mwezi Aprili 2013, lakini mabadiliko hayo yameanza kutekelezwa leo Alhamisi.Hatua hiyo imeafikiwa na maafisakutoka shirika la watoto duniani Unicef na makundi ya haki za watoto nchini Uhispania.Kwa mujibu wa gazeti la El Pais (nchini Uhispania), ni ndoa 365 zilizowahusisha wavulana na wasichana wa chini ya miaka 16 zilizofungwa kati ya mwaka 2000 na 2014 - huku tano tu zikifungwa mwaka 2014.

Chupi zazua kizaazaa Bungeni imeeandaliwa na raymond kaaya aka chuga...

Mbunge mmoja nchini Zimbabwealizua kizaazaa bungeni pale alitumia chupi za kina mama kusisitiza hatma ya raia masikini wa nchini hiyo ambao hawana uwezo wa kununua chupi mpya.Katika kikao kilichokua kikipeperusha moja kwa moja kwenye runinga ya taifa, Priscilla Misihairabwi-Mushonga, wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change (MDC), alitoa karatasi ya plastiki iliyokuwa na chupi hiyo. Kisha akamuuliza waziri wa fedhana sera za serikali kuhusiana na uagizwaji wa chupi kukuu ambayoanasema ni ya bei nafuu na zinasababisha madhara makubwa kwa afya ya kina mama.''Bwana spika hebu tazama hizi chupi ninazo hapa, hizi ni mpya na hugharimu dola mbili kila moja.''''Hizi zilizoko mkono wangu wa kushoto ni mitumba na hugharimu dola moja kwa chupi mbili. alisema mbunge huyoAkijibu swali hilo waziri wa fedha Patrick Chinamasa alimtania mbunge huyo Misihairabwi-Mushonga kutokana na uamuzi wake wa kubeba chupi hizo bungeni lakini amesema wizara yake inachunguza suala hilo. ''Bwana Spika, kabla sijajibu swahili hilo, naamini mheshimiwa mbunge hangelifanya kitendo kama hicho kusisitiza hoja yake'' alisema waziri huyo wa fedha.Chinamasa amesema atalishughulikia suala hilo wiki ijayo wakati atakapotoa taarifa rasmi ya serikali kuhusuiana na sera zake za kiuchumi.Mbunge huyo Misihairabwi-Mushonga baadaye alitimuliwa bungeni baada ya kumkabili vikalimbunge wa chama tawala cha ZANU-PF ambaye alimshutumu kwa kutumia matamshi ya kibaguzi.Uchumi wa Zimbabwe umedorora kwa muda wa miaka kadhaa iliyopita hali iliyosababisha viwango vya umasikini kupanda kutokana na idadi kubwa ya watu wasio na ajira.Nguo kuukuu au mitumba zimefurika masoko ya nchi hiyo na mara nyingi huagizwa kutoka Mozambique na Zambia.Nguo zingine hutengenezwa uchina huku zingine zikitoka Ulaya kama misaada.Mwaka wa 2012 waziri wa fedha Tendai Biti alitaka serikali ya nchi hiyo kupiga marufuku uuagizaji wa chupi za mitumba akisema ni tishio kubwa kwa afya ya raia wa nchi hiyo.

Elimu ya msingi kutolewa bure Tanzania je inawezekana???


Je unaona wewe kama inawezekana??? Kama jibu lako ni ndio tuma ndoi kwenda number 0768527419 na kama ni hapana tuma kwenda namba hiyohiyo... imeandaliwa na dennice lyamuya..

West Ham yasonga mbele Europa league reapoted by riziki malya....


Mashabiki wa West HamLigi ya Europa iliendelea hapo jana ambapo West Ham ya England imesonga mbele katika hatua ya mzunguko wa tatu baada ya kuiondoa Birkirkara ya Malta kwa penalt 5-3.Matokeo mengine haya hapa chiniNewtown AFC 1 - 3 FC CopenhgnAstra Giurgiu 0 - 0 Inverness CTAberdeen 2 - 2 HNK RijekaBirkirkara FC 1 - 0 West HamWest Ham United imeshinda5-3 kwa penaltiLinfield 1 - 3Spartak TrnavaShirak FC 0 - 2 AIKAlashkert FC 2 - 1 Kairat AlmatyDebrecen 9 - 2 Skonto RigaDinamo Minsk 4 - 0 Cherno More VarnaFK Qabala 2 - 0 FK CukarickiFK Spartaks Jurmala 1 - 1 FK VojvodinaInter Baku 2 - 2 FH Hafnarfjördur

Dzeko kuondoka Man City reaport by baraka kutoka majuu...


Kocha Mkuu wa Manchester City Manuel Pellegrini amekubali kuwa mshambuliaji wake Edin Dzeko anaweza kuondoka kwenyeklabu hiyo.Dzeko mwenye miaka 19 yupo pamoja na kikosi cha Man City katika safari ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi huko Australia na hakucheza wakati timu hiyo ilipocheza na AC Roma ya Italia siku ya jumanne.Kuna taarifa Dzeko huenda anaweza kuhamia kuchezea moja ya vilabu huko nchini Italia.