[image_2
Zinazoonekana hapo juu ni nyama za mbuzi ambazo tiyari zimeshaandaliwa kuuzwa kwa wakazi wa eneo la useri..
Leo ni siku ya tisa ambapo ugonjwa hatari wa wanyama ujulikanao kama kimeta kulaza watu wapatao 16.. nikifanya mahojiano ya moja kwa moja na wamama pamoja na wakazi waliothiriwa na ugonjwa huo wa tarakea na useri nawanukuu" tulinunua nyama ya ng'ombe ambayo tiyari ilishapimwa na madaktari na kusema aendelee kuuza lakini cha kushangaza tukasikia wengi waliotumia ile nyama wamekimbizwa hospitalini ilitubidi sis wenyewe tujihami kwa kukimbilia hospitalini na kupewa matibabu haraka na kupata nafuu ..huku tukiambiwa kuwa wenzetu wamekwisha fariki.. nililia sana na kuilaumu serikali kwa,nini watuletee madaktari feki wa mifugo.. bac tunaomba,serikali itangaze hali ya tahadhari ya kula, nyama kwani mpaka sasa sio serikali ya kijiji mpaka wilaya zote zimenyamaza tu. Serikali ituonee huruma.." walimalizia wakazi hao
Mpaka sasa inasemekana watu 16 wameaga dunia kwa kula nyama hiyo ya kimeta Rombo huku serikali ikijitahidi kupita kutangaza ukusanyaji na ulipaji wa kodi kila siku huku suala la kimeta likitupwa nje .. watalipa je kodi kama watakufa kimeta? Serikali piteni na mtangaze tahadhari ya kutokula nyama.. suala la madaktari kuna,wengine hatujui kama walilazimishwa kufanya kazi hiyo inakuwaje huyu anasema uza na mwingine anakuja anasema acha. Mimi nafungasha mikoba yangu na kuondoka kwani sina cha kuwasaidia labda tu taarifa zifike mahali husika maana hii nchi ina wenyewe .. imeandaliwa na wasonga mrombo kutoka wilayani rombo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni