other blog
Jumatatu, 19 Desemba 2016
Chuo cha serikali za mitaa kimetoa harufu ya ufisadi wa ngono....Waziri ataka Bodi Chuo cha Serikali za Mitaa kushughulikia malalamiko
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
(Tamisemi), Mhe.George
Simbachawene, ameiagiza bodi ya
chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo
mkoani Dodoma (LGTI), kuyafanyia
kazi malalamiko ya vitendo vya rushwa
ya ngono katika idara ya taaluma na
mitihani.
Mhe.Simbachawene ametoa agizo hilo
tarehe 25 Novemba, 2016, wakati
alipokuwa akizungumza na wanafunzi
pamoja na uongozi wa chuo hicho
wakati wa mahafali ya nane ya chuo
hicho.
Amesema katika moja ya maeneo
ambayo hajaridhishwa nayo, idara ya
mitihani ambayo imekuwa
ikilalamikiwa na wanafunzi juu ya
urasimu uliopo hasa wakati wa
wanafunzi wanapo hitaji matokeo
yao.
Aidha, Waziri Simbachawene
amesema malalamiko mengi
yamekuwa katika idara hiyo kwa
kipindi kirefu lakini uongozo wa chuo
hicho umeendelea kulikalia kimya bila
kuchukua hatua.
"Naiagiza bodi ya chuo kuhakikisha
kuwa idara hii inachukuliwa hatua
ikiwa ni pamoja na kuifumua na
kuiunda upya kwani malalamiko haya
yamekuwa ya muda mrefu watu
wanaohusika na idara hii wamekuwa
na ukilitimba wa hali ya juu
mwanafunzi anapotaka kupata
matokeo ya mitihani yake ni
atazungushwa kama nini," amesema
Mhe.Simbachawene.
Amesema hali hiyo imekuwa ikiashiria
uwepo wa vitendo vya rushwa mbaya
ya ngono kati ya wahusika wa idara ya
mitihani na wanafunzi wa kike lakini
pia wanafunzi wa kiume kudaiwa
fedha.
"Naomba mlifanyie kazi suala hili
haraka sana kwani haya malalamiko
mimi ninayo kwa mda mrefu lakini na
shangaa uongozi mmekaa kimya hali
ambayo imefikia hatua hata kama
mwanafunzi kalipia ada ya hosteli
lakini bado atazungushwa hadi
muhusika mwentee apende utazani
anaomba bure,"amesema.
Aidha aliongeza kuwa kitu kingine
ambacho anautaka uongozi wa chuo
hicho kukifanyia kazi ni namna ya
matumizi ya fedha za chuo kwani
kumekuwepo na upotevu wa fedha
lakini hakuna hatua zilizochukuliwa
kwa waliohusika.
"Fedha za chuo zimeibiwa na
wahusika wapo hadi hii leo lakini
hakuna kilichuuliwa naomba wahusika
wasimamishwe haraka ili uchuguzi
ufanyike na hatua zingine kuchukuliwa
kwa wahusika," alisema.
Hata hivyo amesema kuwa kuna kila
sababu ya serikali kutengeneza
utaratibu ambao utakuwa unatumika
katika kuwaajili wanafunzi
wanaomaliza katika chuo hicho
ambao wanataaluma ya utumishi
katika mamlaka za serikali a mitaa.
"Serikali inatumia takribani bilioni 8.3
kwajili ya kuendesa chuo hichi
kilamwaka lakini wanafunzi
wanapotoka hapa wanakosa kazi hali
ambayo si sahihi kutokana na
uwezkezaji huo unaofanywa na
serikali kwa mwaka kwani hata ujenzi
wa chuo hiki umeghalimu sh. bilioni
36.5 hivyo ni lazimu wahitimu hawa
tuwatumie ipasavyo,"alisema
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya
Wadhamini ya chuo hicho Prof.
Suleiman Ngware alisema kuwa
maagizo yote yaliyotolewa na Waziri
atayafanyika kazi haraka iwezekanvyo
na wahusika wote watachukuliwa
hatua.
"Mheshimiwa Waziri yote uliyoagiza
tutayafanyia kazi na hatua kali
zitachuliwa kwa wahusika wote bila ya
kumuonea mtu," amesema Prof.
Ngware.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni