Mwanasheria Mkuu wa Chadema,
Tundu Lissu, akizungumza na
waandishi wa habari, Dar es Salaam
jana kuhusu kupotea kwa msaidizi
wa mwenyekiti wa chama hicho, Ben
Saanane. Kulia ni Ofi sa Habari,
Tumaini Makene na Katibu Mkuu
wa Baraza la Vijana (Bavicha), Julius
Mwita.
CHAMA cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), kimeitaka
Serikali kutumia vyombo vyake vya
ulinzi na usalama kumtafuta
msaidizi wa mwenyekiti wa chama
hicho, Bernard Saanane , ambaye
ametoweka katika mazingira ya
kutatanisha zaidi ya mwezi mmoja
sasa.
Chadema imesema Serikali ndiyo
yenye uwezo pekee wa kiufundi
kujua na kuamuru mashirika ya
simu kueleza mawasiliano yake ya
mwisho yalivyokuwa.
Akizungumza na waandishi wa
habari jana, Mwanasheria Mkuu wa
Chadema, Tundu Lissu alisema
katika siku za karibuni, Saanane
amekuwa akiongoza kampeni
kwenye mitandao ya kijamii, kuhusu
kuhakikiwa kwa shahada za
uzamivu (PhD) kwa baadhi ya
viongozi.
Mwanasheria huyo wa Chadema,
alisema wakati fulani Saanane
alitumiwa ujumbe wa maneno
kupitia simu yake ya kiganjani
akitishiwa kuacha kuikosoa Serikali.
“Nanukuu maneno aliyotumiwa:
“Ben Saanane unachokitafuta ndani
ya Serikali hii utakipata, kwa elimu
na uwezo wako hatukutarajia
ungefikia hatua ya ajabu kwa namna
ulivyofikia, hujiulizi kwanini upo
huru hadi muda huu.
“You are too young to die. Tunajua
utaandika na hili, andika lakini the
next post hutaandika ukiwa na
uhuru wa kutosha, andika but your
days are numbered.
“Unajua kuna rafiki yako alipuuza
na hutaki kuandika kuhusu yeye,
labda kwa kuwa alitangulia, andika
Ben, andika sana, ongea, sema
lakini utajikuta mwenyewe na
chatu,” alinukuu Lissu.
Alisema: “Katika miezi ya hivi
karibuni watu ambao wamekuwa
wakiikosoa Serikali kupitia mitandao
ya kijamii wamekuwa wakikamatwa
na watwambie kama wanamshikilia
Ben Saanane ili tujue.
“Serikali ndiyo yenye udhibiti wa
mipaka yetu kuanzia baharini, nchi
kavu, mipaka yetu ya anga na hata
katika bandari, hivyo ituambie,”
alisema Lissu.
Aidha mbunge huyo wa Singida
Mashariki alisema yeyote
anayefahamu taarifa za Saanane
azitoe hadharani katika vyombo vya
habari, polisi na hata katika vyombo
vingine vya Serikali.
Aidha Lissu alisema taarifa za
kupotea kwa Saanane wamezifikisha
ngazi za kimataifa na wataendelea
kuzisambaza ili dunia nzima ijue.
Akizungumzia kuhusu taarifa
ambayo imesambaa katika mitandao
ya kijamii kuwa Mwenyekiti wa
chama hicho, Freeman Mbowe
anajua aliko Saanane, alisema:
“Mara ya mwisho Ben amewasiliana
na mwenyekiti Novemba 14 mwaka
huu akiwa Dodoma na huwa
hawaongozani, bali Ben anafanyia
kazi zake makao makuu ya chama.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni