other blog

Alhamisi, 24 Septemba 2015

Njia bora na sahihi kwa vijana kujiwekea akiba kwa sababu ya maisha ya kesho..hii hapa..imeandaliwa na mwandishi wa rombo wasonga mrombo


Taifa lenye akiba ya kutosha na
uchumi imara linakuwa na uwezo
katika kujiletea maendeleo na hata
kustahimili majanga yoyote
yanapotokea. Nguvu hiyo inatokana na
uwezo mkubwa wa akiba na mtaji
iliyowekezwa kwenye miradi
mikubwa.
Mtu kuweka akiba, ni muhimu sana
kama vile ilivyo kwa taifa. Saikolojia ya
matumizi ya fedha inaonyesha kuwa
mtu hupenda kutumia sasa kuliko
kusubiri baadaye ambapo ingeongeza
faida na thamani zaidi.
Fedha ni kitu ambacho kipo tu kwa
muda kama mtu aliyekuwa nayo sasa
akishindwa kuidhibiti leo, kesho
hatakuwa nayo. Suala mtambuka hapa
ni je, kwa nini niweke akiba au
niwekeze kwa jambo lingine?
Ningependa nizungumzie juu ya njia
mbalimbali za kuweka akiba ambapo
zikitumika zinaweza kukuletea faida
kwa karne hii, japo kiuhalisia kwa
Waafrika kuweka fedha ni tatizo sugu
kwa walio wengi. Hali kama hii
inatokana na uwezo mdogo wa
kudhibiti fedha kwa mitindo ya kisasa
na kibiashara pia. Elimu juu ya jambo
hili haijafika au haijakaa vizuri katika
upande wa ubongo iliyo wazi kwa
mazingira ya hapa nchini.
Zipo njia ambazo ni nzuri zikitumika
kwa kuweka akiba kwa faida
zitaongeza maendeleo ya wengi. Njia
hizo ni:
Moja, ni kununua fedha za kigeni.
Mara nyingi fedha za kigeni mfano
Dola za Marekani, Euro, Pound ya
Uingereza na fedha kutoka Bara la Asia
kama vile za Saudi Arabia, huwa
zinapanda thamani ukilinganisha na za
Tanzania.
Mfano, ulinunua Dola moja ya
Marekani Novemba, mwaka jana kwa
Sh1,300. Mwaka huu unaiuza kwa
Sh2,100. Ukipiga hesabu umepata
faida ya Sh800. Kama ulinunua Dola
10,000, leo hii ikiziuza una faida ya
Sh1 milioni, na kadhalika.
Mtindo wa kununua dola kwanza
unapunguza kubeba lundo la fedha
nyingi, inakuzuia kuitumia bila
sababu, hivyo kuendelea kuwa akiba,
kukulinda na kukuwezesha uwe na
faida pale mfumuko wa bei
unapoongezeka na inaweza kukusaidia
iwapo itakulazimu usafiri nje ya nchi.
Ukisafiri nje ya nchi itakufanya
usitumie fedha nyingi za kununua za
kigeni kwa gharama kubwa.
Pili, ni simu benki. Huu ni mfumo
ambao upo sana siku hizi eneo la
Afrika Mashariki. Siku hizi kampuni za
simu zimewezesha mtu kuweka akiba.
Huduma imeboreshwa zaidi kwa
kuweza kuzihamishia kwenye akaunti
za benki, kulipia huduma na bidhaa au
kuzitoa katika nchi nyingine kulingana
na aina ya fedha za eneo husika.
Hii inamuwezesha hata kama mtu
akiwa mbali na benki na kuwa na
uwezo wa kuokoa muda kwa kutumia
pesa alizoweka kwenye simu yake kwa
kuzitoa kwa wakala aliye karibu naye.
Vilevile, kwa kutumia simu waweza
kuvuta fedha kutoka kwenye akaunti
yako ya benki na kuziingiza kwenye
simu yako na kuwa huru kuzitoa ili
kuzitumia eneo lolote kwa kutumia
mawakala.
Siku hizi pia kwa kutumia akiba
kwenye simu unaweza kupata huduma
nyingine kupitia simu hiyo kama vile
kununua umeme, kulipia bili ya maji,
matibabu, king’amuzi na hata tiketi za
kuingia kwenye michezo ya soka au
tamasha. Mtu aweza kudunduliza
fedha kidogokidogo kwenye simu yake.
Tatu, kuweka akiba kwa kutumia benki
na taasisi nyingine za kifedha. Hii
husaidia sana kuhamasisha huduma za
kuweka akiba kwa malengo kama vile
kumsomesha mtoto au amana.
Uwekaji wa fedha za namna hiyo pia
huweza kusaidia kuwa na fedha za
kukabili dharura na kuwa na mitaji
mikubwa ya kibiashara na hatimaye
kuleta maendeleo makubwa
yaliyokusudiwa.
Nne, ni kumkopesha mtu na kurudisha
kwa riba. Siku hizi aina hii ya
ukopeshaji imeenea sana, hasa mijini
na vyuoni. Hii imetokana na watu
kuzidi kukua sana kiuelewa,
wamebadili mwelekeo kutoka
kumkopesha mtu pasipo riba hadi
kuwa na faida.
Watu wameerevuka na kufahamu
kuwa fedha ya mwezi au wiki hii ni
tofauti na ya mwezi au wiki lijalo.
Tatizo lililopo ni kwamba hakuna
maandishi ya kukopeshana kwa walio
wengi kwa sababu za kujali utu. Lakini
ukweli ni kwamba wanadamu wengi
wana tabia ya kubadilika. Kama huna
maandishi ya kukopeshana itakuwa
vigumu kupata fedha zako pale
anapokuwa si mwaminifu.
Tano, ni kuwekea bima mali zako na
biashara yako. Hii ni njia ambayo ni
muhimu sana maana hakuna mtu
anayeweza kuzuia majanga ambayo ni
ya asili au ya kawaida, hivyo bima
hasaidia sana siku ukipata ajali ya
biashara kwa kuibiwa au kuungua.
Sita, ni kununua vitu kama nyumba,
ardhi na vifaa vya gharama vyenye
kudumu muda mrefu. Hivi waweza
kuviuza baadaye kwa bei ya juu.
Maendeleo ya mtu mmojammoja ni
mafanikio ya taifa. Taifa lenye akiba ya
kutosha kwa kawaida linakuwa imara
na wananchi wenye akiba kwa njia
mbalimbali kama nilivyoorodhesha, ni
watu wenye maisha ya uhakika.
Dharura zote wanaweza kuzikabili na
hapa ndipo pia mitaji mikubwa ya
biashara inatokea. Kuweka akiba ni
jambo la msingi, tuanze leo kuweka
akiba. MPENZI MSOMAJI KAMA UMEGUZWA NA MAKALA HAYA TUANDIKIE KWENDA EMAIL HII kimarioerasmi@gmail.com

Haya libabu la arsenal hii Ndoa ya Arsene Wenger yavunjika Ndoa ya kocha wa Arsenal, Arsene Wenger na mke wake, Annie iliyodumu kwa miaka mitano imevunjika


Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger na
mkewe Annie
Strasbourg, Ufaransa. Ndoa ya kocha
wa Arsenal, Arsene Wenger na mke
wake, Annie iliyodumu kwa miaka
mitano imevunjika baada ya miezi
kadhaa ya uvumi.
Habari za kimahakama mjini
Strasbourg zilieleza jana kuwa wawili
hao wenye binti wa miaka 18,
wamekuwa hawaonekani pamoja
tangu mwaka 2013.
Wenger, mwenye umri wa miaka 65 na
mkewe, Annie 59 wamefikia mwafaka
wa kugawana mali.
Mara kadhaa, kocha huyo alikiri kuwa
shinikizo kubwa la kazi kwenye klabu
hiyo ya London Kaskazini
limesababisha matatizo kwenye ndoa
yake.
Nyaraka za kimahakama zilionyesha
kuwa wawili hao walitengana Juni
mwaka huu.
Hata hivyo, nyaraka hizo zimeeleza
kuwa si talaka kamili, bali
wametengana kisheria, jambo
linalomaanisha kuwa wana jukumu la
kuendelea kuwa pamoja.
Wawili hao walifunga ndoa Desemba
2010 baada ya uhusiano wa muda
mrefu, lakini wamekuwa si wenye
furaha kwa muda sasa.
“Wamegawana mali na rasilimali,
wamefikia mwafaka wa kutengana.
Mwaka 2008, kocha huyo alieleza
dhamira ya kuacha soka ili kuwekeza
nguvu kwenye ndoa.
Alisema: “ Miaka kumi iliyopita,
nilimweleza mke wangu (Annie),
‘Anipe miaka mitano zaidi katika soka
inatosha’, lakini hadi leo ninaendelea
na kazi.
“Ni vigumu kuwa na muda wa kutosha
kukaa pamoja kwa sababu ya ratiba
ngumu ya masuala ya soka. Kuna
wenzetu wanaondoka Jumatatu na
kurudi Ijumaa
“Ninasafiri kikazi, lakini tatizo si kiasi
gani cha muda ninaotumia mbali ya
familia yangu, bali ubora wa muda
ninaotumia na familia yangu.
“Nikizingatia hilo, kuna madhara.
Familia inakosa ubora wa huduma
wanazostahili nikiwa nyumbani, kwani
ninafikiria mchezo unaofuata.”
Aliongeza: “Mke wangu anapenda
kuangalia soka, anaona mechi za
Arsenal akiwa nyumbani . Siyo shabiki,
lakini anapenda michezo. Ni kwa kuwa
hakuwa na chaguo.”
-

Watu 41 wakamatwa kwa kutishia amani kwenye kampeni Watu 41 wakiwamo wanawake tisa wamekamatwa mkoani hapa kwa tuhuma za kufanya vurugu katika


Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya,
Ahmed Msangi.
Mbeya. Watu 41 wakiwamo wanawake
tisa wamekamatwa mkoani hapa kwa
tuhuma za kufanya vurugu katika
maeneo mbalimbali wakati wa
kampeni zinazoendelea kuwanadi
madiwani na wabunge.
Kamanda wa polisi mkoani hapa,
Ahmed Msangi amesema hayo leo
alipozungumza na waandishi wa
habari kuhusu tathimini ya matukio ya
uchaguzi.
Amesema tangu kampeni zilipoanza
matukio 30 ya uhalifu yalifanyika
yakiwahusisha wanaume 32 na
wanawake tisa.
Amesema tukio moja kati ya hayo
lilimhusisha Aman John ambaye
amefikishwa kortini na kupatikana na
hatia iliyosababisha alipe faini ya
Sh30,000.
“Kesi nane kati ya matukio hayo zipo
mahakamani zikiwa katika hatua
mbalimbali lakini kesi tatu majalada
yapo ofisi ya wanasheria wa Serikali
wakati kesi zingine 19 zinapelelezwa,’’
amesema.
Amesema waliokamatwa
wametuhumiwa makosa mbalimbali
yakiwamo ya kuchana mabango ya
wagombea wa Urais, Ubunge na
Udiwani.
‘’Wengine wamekamatwa kwa makosa
ya kung’oa bendera, kuharibu mali,
kufanya fujo, kujeruhi, kuingilia
mkutano, kutishia kuua kupigana
hadharani na wizi’’ amesema kamanda
huyo

Kipindupindu chaendelea kunyonga watu dar.. Kipindupindu chaendelea kuua D’Salaam Idadi ya watu waliopoteza maisha kwa ugonjwa wa kipindupindu imeongezeka na kufikia 17 baada ya


Watoto wakicheza katika jalala eneo la
Bugando Mwanza, mazingira ya namna hii
ni hatari kwa afya zao.
Dar es Salaam. Idadi ya watu
waliopoteza maisha kwa ugonjwa wa
kipindupindu imeongezeka na kufikia
17 baada ya watu wengine wawili
kupoteza maisha jana.
Hata hivyo, idadi ya watu
walioripotiwa kuugua ugonjwa huo
tangu ulipuke katika Jiji la Dar es
Salaam Agosti 17, imefikia 2,000.
Ofisa Habari wa Manispaa ya Temeke,
Joyce Msumba alisema kuwa jana
walipokea wagonjwa wapya saba na
kati yao, mmoja ameshafariki dunia.
Msumba alisema wagonjwa wengi
hawatoki katika Manispaa hiyo bali
wapo wanaotoka eneo la Buguruni
katika Manispaa ya Ilala na
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
mkoani Pwani.
Alisema tayari wameshatoa taarifa
kwa maofisa wa afya wa wilaya zao ili
wafuatilie hali katika familia zao.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya
Kinondoni, Victorina Ludovick alisema
wamepokea wagonjwa wapya 31 idadi
inayofanya watu waliolazwa katika
kambi ya ugonjwa huo kufikia 38.
Dk Ludovick alisema wagonjwa wengi
wanatoka maeneo ya Buguruni,
Vingunguti, Jangwani, Ilala,
Mchikichini, Tabata na Kigogo.
Alisema kuendelea kusambaa kwa
ugonjwa huo kunatokana na wakazi
wengi wa maeneo hayo kutozingatia
kanuni za afya wanazofundishwa na
wataalamu.
“Magari ya matangazo yanapita katika
mitaa yao kila siku kutoa elimu na
kuwahamasisha kunawa mikono kwa
sabuni baada ya kutoka chooni,
kuchemsha maji ya kunywa na
kuzingatia usafi wanapoandaa
vyakula,” alisema Ludovick
Alisema maofisa afya wanaendelea na
kazi ya kukagua mazingira
wanayofanyia kazi wafanyabiashara
wa vyakula na matunda ili kuwabaini
wanaokiuka agizo la kuacha kufanya
biashara hiyo hadi ugonjwa huo
utakapokwisha.

Idd kwa waislamu wengine imewasababishia kifo Mamia ya mahujaji wafariki katika mkanyagano Makka Watu wasiopungua 717 wamekufa, huku wengine 816 wamejeruhiwa leo jirani na mji mtakatifu wa Makka


Watu wasiopungua 717 wamekufa,
huku wengine 816 wamejeruhiwa leo
jirani na mji mtakatifu wa Makka
walikokwenda kuhiji ikiwa ni sehemu
ya utekelezaji wa moja ya nguzo
muhimu katika Imani ya dini ya
Kiislamu, maofisa Saudi Arabia
wathibitisha.
Kwa mujibu wa Baraza la Taasisi na
Jumuiya za Kiiislam nchini, kati ya
mahujaji 2,000,000 waliokwenda Saudi
Arabia mwaka huu, 1,500 wanatoka
Tanzania.
Japokuwa Msemaji wa Baraza hilo,
Shekhe Rajabu Katimba amesema
hakuna vifo vilivyokwisharipotiwa hadi
sasa toka Makka, taarifa zisizo rasmi
kutoka huko zinasema Mtanzania
mmoja amekufa na mwingine
amejeruhiwa baada ya kutokea
mkanyagano.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji
la BBC, katika maafa hayo, mahujaji
wengine wasiopungua 816
wamejeruhiwa katika eneo la Mina.
Vifo hivyo vimetokea ikiwa ni siku
chache kupita baada ya kutokea jail
nyingine ambapo winchi lilianguka na
kuua watu 109 katika msikiti ambapo
kulikuwa kukifanyika ibada ikiwa ni
maandalizi ya kuelekea sikukuu ya leo.
Haya ni maafa makubwa zaidi kutokea
katika sikukuu ya Eid Al Hajj baada ya
kupita takribani miaka 25. Kwa mujibu
wa Kurugenzi ya Wizara ya Usalama
wa Raia nchini Saudi Arabia, maafa
hayo yametokea kati ya saa sita
(majira ya Afrika Mashariki) katika
makutano ya mitaa namba 204 na 223
wakati mahujaji hao wakipanda ngazi
kuelekea jengo la ghorofa tano ambalo
limeuzunguka mnara, maarufu kwa
jina la Jamarat Bridge. “Tukio hilo
limetokea baada ya mahujaji
kuongezeka ghafla wakielekea kwenye
mnara,” taarifa ya wizara iliongeza.

Jumatano, 23 Septemba 2015

Maaaajabu haya .. mtoto mwenye miguu minnee azaliwa rombo ..kijiji cha kitowo


Mpenzi msomaji haya ni maajabu ambayo huwa hutokea kwa nchi za wenzetu lakini leo nishtuka sana na habari hizi ambazo hazijathibitishwa.. ila chanzo kmoja kinasema kwamba mtoto huyo alizaliwa katika zahanati ya kasuruwa.. tarehe 21/03/2014 na hadi sasa mtoto huyo amehamishiwa daresalamu ambako wanaishi wazazi wake ila nyumbani kwao ni kitowo ... habari hizi hazijathibitishwa pindi zitakapo kuwa sawa mtapata hapahapa eaglefm endelea kutufuatilia ili upate ukweli.

Jumanne, 22 Septemba 2015

Kwa vume kunani.. Liewig ajitetea Stand United kuchemsha Wakati uongozi wa Stand United ukiwakingia kifua mashabiki wa timu hiyo kwa kumfanyia vurugu


Kocha wa Stand United, Patrick Liewig
Dar es Salaam. Wakati uongozi wa
Stand United ukiwakingia kifua
mashabiki wa timu hiyo kwa
kumfanyia vurugu kocha, Patrick
Liewig mwenyewe amesema uwezo
wake hauwezi kupimwa kwa mechi
mbili.
Liewig ameiongoza Stand kushinda
mechi moja na kutoka sare mbili tangu
alipojiunga na timu hiyo alijikuta
kwenye wakati mgumu wa kutaka
kupigwa na mashabiki baada ya timu
yake kuruhusu kipigo cha mabao 2-0
dhidi ya Azam wiki iliyopita mjini
Shinyanga.
Akizungumza na gazeti hili jana,
Mfaransa huyo alisema anajiamini na
anaamini yeye ni kocha mwenye
uwezo huku akisisitiza asipimwe kwa
matokeo ya mechi mbili ambazo timu
yake imekwishapoteza tangu kuanza
kwa ligi.
“Nahitaji kupewa muda, timu ya Stand
inajengwa taratibu, mashabiki wawe
na subira endapo wanahitaji mafanikio
kwani naamini ushindi hupo,” alisema
kocha huyo kwa kifupi.
Mwenyekiti wa Stand United, Aman
Vicent alisema kitendo kilichofanywa
na mashabiki wao kinaweza kutokea
katika timu nyingine yoyote ni cha
kawaida katika soka.
“Unajua tulitarajia makubwa
ukizingatia kocha analipwa fedha
nyingi sasa kitendo cha kufungwa
mechi mbili mfululizo kiliwakasirisha
mashabiki na kulazimika kufanya kile
kilichotokea, lakini tumeyamaliza na
tunajipanga kwa mechi zijazo,”
alisema Vicent.
Liewig aliajiliwa kuinoa Stand kama
kocha mkuu miezi michache kabla ya
ligi kuanza, kocha huyo pia aliwahi
kuifundisha Simba huku akiacha
rekodi ya kuwaibua vijana kwenye
timu hiyo.
Naye Mchambuzi wa soka na kocha wa
zamani wa Taifa Stars, Mshindo Msolla
amemtetea kocha huyo raia wa
Ufaransa na kueleza kuwa hastahili
kulaumiwa hivi sasa kutokana na
matokeo ya timu hiyo imepata na
kusisitiza kuwa wachezaji wa timu hiyo
hakuwasajili yeye.
“Liewig hastahili lawama, timu
ameikuta tayari imesajiliwa hivyo
matokeo ya sasa yanawahusu uongozi,
wanachotakiwa kufanya kwa sasa ni
kumpa muda wa kuijenga timu hiyo na
itakapofika kipindi cha dirisha dogo
aachiwe afanye usajili wa wachezaji
anaowahitaji,” alisema Msolla.