Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya,
Ahmed Msangi.
Mbeya. Watu 41 wakiwamo wanawake
tisa wamekamatwa mkoani hapa kwa
tuhuma za kufanya vurugu katika
maeneo mbalimbali wakati wa
kampeni zinazoendelea kuwanadi
madiwani na wabunge.
Kamanda wa polisi mkoani hapa,
Ahmed Msangi amesema hayo leo
alipozungumza na waandishi wa
habari kuhusu tathimini ya matukio ya
uchaguzi.
Amesema tangu kampeni zilipoanza
matukio 30 ya uhalifu yalifanyika
yakiwahusisha wanaume 32 na
wanawake tisa.
Amesema tukio moja kati ya hayo
lilimhusisha Aman John ambaye
amefikishwa kortini na kupatikana na
hatia iliyosababisha alipe faini ya
Sh30,000.
“Kesi nane kati ya matukio hayo zipo
mahakamani zikiwa katika hatua
mbalimbali lakini kesi tatu majalada
yapo ofisi ya wanasheria wa Serikali
wakati kesi zingine 19 zinapelelezwa,’’
amesema.
Amesema waliokamatwa
wametuhumiwa makosa mbalimbali
yakiwamo ya kuchana mabango ya
wagombea wa Urais, Ubunge na
Udiwani.
‘’Wengine wamekamatwa kwa makosa
ya kung’oa bendera, kuharibu mali,
kufanya fujo, kujeruhi, kuingilia
mkutano, kutishia kuua kupigana
hadharani na wizi’’ amesema kamanda
huyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni