Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James
Mbatia
Dar es Salaam. Siku moja baada ya Dk
Willibrod Slaa kuibuka na kuelezea
kilichotokea wakati wa kumkaribisha
Edward Lwoassa Ukawa na hatimaye
kutangaza kuachana na siasa,
Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James
Mbatia amejibu tuhuma zilizotolewa
na Dk Slaa huku akitahadharisha kuwa
zinalenga kulipasua taifa.
Mbatia ambaye ni Mwenyekiti Taifa
wa NCCR Mageuzi amesema leo jijini
Dar es Salaam alipokuwa akizungumza
an waandishi wa habari kuwa mambo
yaliyozungumzwa Dk Slaa ikiwa ni
pamoja na kashfa zakuwatuhumu
viongozi wa dini kuhongwa na Lowassa
si yakweli na yanaweza kuligawanya
taifa.
Mbatia amesema kuwa Dk Slaa
angepaswa kutoa hoja zake na sio
kuwashambulia watu binafsi
wakiwemo viongozi wa dini.
‘’Mimi nilitegemea Dk. Slaa ataeleza
hoja zake, lakini hoja za kashfa za
kuwahusisha viongozi wa dini hasa
maaskofu ni hoja ambazo ni wazi
zimelenga kulipasua taifa’’ alisema
Mbatia.
Pia Mbatia amekiri kuwa Dk. Slaa
alishiriki katika mchakato wa
kumkaribisha Lowassa lakini katika
vikao vyote Lowassa hakuwahi kusema
atakuja na wabunge toka Chama Cha
Mapinduzi.
‘’ Katika kikao cha kujadili juu ya
kumpokea Lowassa tukiwa na viongozi
waandamizi wa Ukawa pamoja na
Lowasaa kilichofanyika tarehe 20
mwezi wa saba , Lowassa hajawahi
kutamka kuwa atakuja na wabunge 50
toka Chama cha Mapinduzi, wala
hakusema atakuja na wenyeviti wa
mikoa na wilaya’’
Akizungumzia suala la Dk. Slaa kudai
alipewa rushwa ya Sh500m ili kuzuia
ripoti ya Richmond isiingie bungeni,
Mbatia ameuliza kwanini Dk.Slaa
hakuripoti kipindi hicho na anakuja
kuongelea sasa.
“Nashangaa tangu sakata la Richmondi
litokee ni miaka saba hadi sasa, lakini
Dk. Slaa hakuwahi kusikika
akilizungumzia, na kwanini hakuripoti
kwenye vyombo vinavyohusika’’ alihoji
Mbatia.
Aidha Mbatia amevitaka vyombo vya
habari kuandaa midahalo maalum
ambayo itawahusisha viongozi wa
kisiasi ili kujibu mambo
wanayotuhumiwa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni