Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Zuberi
Mwombeji
Lushoto.Watu wawili wamefariki
dunia na wengine 15 kujeruhiwa
baada ya basi walilokuwa wakisafiria
kuacha njia na kupinduka katika Kijiji
cha Longoi Kata ya Mtae wilayani
Lushoto jana majira ya saa 11.00 jioni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,
Zuberi Mwombeji alisema leo kuwa
ajali hiyo imelihusisha gari la Kampuni
ya Shambalai ambalo lilikuwa likifanya
safari zake kutoka Dar es salaam
kuelekea Mtae ambapo lilipinduka na
kuingia kwenye korongo.
Kamanda Mwombeji amesema abiria
waliofariki katika ajali hiyo miili yao
imeshatambulliwa ambapo mmoja ni
mkazi wa Mtae na mwingine ni mkazi
wa Vuli.
Aidha Kamanda Mwombeji alieleza
kuwa chanzo cha ajali hiyo bado
hakijafahamika ila ubovu wa barabara
pia unaweza kuwa umechangia kwa
ajali hiyo.
Majeruhi wa ajali hiyo akiwemo
dereva wa basi hilo, Sadiki Ayoub
mkazi wa Mlalo wamelazwa katika
Hospitali ya Wilaya ya Lushoto kwa
matibabu zaidi na hadi leo hali zao
zinaendelea vizuri huku wengine
wakipewa ruhusa.
Ingawa dereva wa basi hilo
amejeruhiwa katika ajali hiyo lakini
yupo chini ya uangalizi wa jeshi la
polisi kwa ajili ya kuho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni