Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA,
Dr. Slaa akiwa kwenye mkutano na
waandishi wa Habari katika ukumbi wa
Hoteli ya Serena.
Slaa: Watanzania wana kiu ya
kujua kwanini amekuwa kimya
kwa muda mrefu sasa licha ya
harakati za kisiasa kuendelea.
Muda utakaotumika ni saa moja,
hakuna muda mrefu sana.
Ameamua kufanya hayo kwa kuwa
imefika mahali ukweli lazima
usemwe na upotoshwaji
ukomeshwa. Namna pekee ya
kufanya hivyo ni kutoka
hadharani na kuusema ukweli.
Sote tunafahamu kuwa hana tabia
ya kuchenga mambo, mengi
yamesemwa na watu tofauti,
kwenye mitandao, magazeti na
viongozi wake!
Hana ugomvi na kiongozi yoyote,
kwa kuwa siasa sio ugomvi. Kama
binadamu wa kawaida hana chuki
wala hasira na binadamu
mwingine yoyote!
Iwe wazi kuwa katika Taifa kuna
misingi ambayo inaongoza taifa.
Inapofika mahali taifa
linaongozwa kwa msingi ya
propaganda na upotoshwaji
matokeo yake ni vurugu kubwa
katika taifa. Yeye amekataa hayo
yote!
Anasema kuwa YEYE hakuwa
likizo kama inavyosemwa na
viongozi wake! Atafafanua kwa
kifupi!
Kilichotokea ni kuwa aliamua
kuachana na siasa, tarehe 28 Julai
2015, majira ya saa tatu usiku,
baada ya kuona yanayofanyika
ndani ya chama chake
hayamridhishi.
Mtangulizi wa shuguli ambaye
anatoka kwenye kampuni ya
mahusiano ya umma
anamtambulisha Dr. Willibrod
Slaa.
Anasema kuwa kwa muda mrefu
Slaa amekuwa alama ya harakati
za ukombozi dhidi ya makucha ya
mkoloni mweusi.
anaongeza kuwa Dr. ataongea kwa
muda kisha kuruhusu maswali
kutoka kwa waandishi,
anamkaribisha!
Kinachosemwa ni kuwa Dr. Slaa
alishiriki tangu mwanzo kwenye
mchakato. Anasema ni kweli
alishirii kwenye majadiliano,
akaweka msingi na msimamo
wako. Kuna wakati wengi
wanashinda kutokana na wingi
wao, wewe unayeamini katika
misingi inabidi uachie ngazi.
Azam TV wameanza matangazo
kupitia kipindi chao cha KITUO
CHAKO CHA UCHAGUZI, wako LIVE
sasa... Bado uchambuzi wa safari
ya Kisiasa ya Dr. Willibrod Slaa
unaendelea.
Tumepelekwa moja kwa moja
kutoka Hoteli ya Serena
Mtangulizi wa shuguli ambaye
anatoka kwenye kampuni ya
mahusiano ya umma
anamtambulisha Dr. Willibrod
Slaa.
Anasema kuwa kwa muda mrefu
Slaa amekuwa alama ya harakati
za ukombozi dhidi ya makucha ya
mkoloni mweusi.
anaongeza kuwa Dr. ataongea kwa
muda kisha kuruhusu maswali
kutoka kwa waandishi,
anamkaribisha!
==========================
Slaa: Watanzania wana kiu ya
kujua kwanini amekuwa kimya
kwa muda mrefu sasa licha ya
harakati za kisiasa kuendelea.
Muda utakaotumika ni saa moja,
hakuna muda mrefu sana.
Ameamua kufanya hayo kwa kuwa
imefika mahali ukweli lazima
usemwe na upotoshwaji
ukomeshwa. Namna pekee ya
kufanya hivyo ni kutoka
hadharani na kuusema ukweli.
Sote tunafahamu kuwa hana tabia
ya kuchenga mambo, mengi
yamesemwa na watu tofauti,
kwenye mitandao, magazeti na
viongozi wake!
Hana ugomvi na kiongozi yoyote,
kwa kuwa siasa sio ugomvi. Kama
binadamu wa kawaida hana chuki
wala hasira na binadamu
mwingine yoyote!
Iwe wazi kuwa katika Taifa kuna
misingi ambayo inaongoza taifa.
Inapofika mahali taifa
linaongozwa kwa msingi ya
propaganda na upotoshwaji
matokeo yake ni vurugu kubwa
katika taifa. Yeye amekataa hayo
yote!
Anasema kuwa YEYE hakuwa
likizo kama inavyosemwa na
viongozi wake! Atafafanua kwa
kifupi!
Kilichotokea ni kuwa aliamua
kuachana na siasa, tarehe 28 Julai
2015, majira ya saa tatu usiku,
baada ya kuona yanayofanyika
ndani ya chama chake
hayamridhishi.
Kinachosemwa ni kuwa Dr. Slaa
alishiriki tangu mwanzo kwenye
mchakato. Anasema ni kweli
alishirii kwenye majadiliano,
akaweka msingi na msimamo
wako. Kuna wakati wengi
wanashinda kutokana na wingi
wao, wewe unayeamini katika
misingi inabidi uachie ngazi.
Baada ya Edward Lowassa
kukatwa na CCM Dodoma,
Mshenga wake alimpigia simu na
kuuliza nini kifuate baada ya
tukio la dodoma. Akamuambia
wawasiliane na mwenyekiti
Freeman Mbowe, Gwajima nae
akafika kwenye kikao hicho.
Msimamo wa Slaa ni kuwa ni
lazima kumsikiliza mtu kabla ya
kuamua nini cha kufanya.
chadema ni cham cha siasa na
hakiwezi kumkataa mtu yeyote
kujiunga na chama.
Wakaweka vijana kuchunguza nini
wanataka hao wanaotaka
kujiunga na chama!
Slaa akataka kwanza Lowassa
atangaze kutoka kwenye chama
chake alichopo, kisha atangaze
anakwenda kwenye chama gani.
Atumie nafasi hiyo ya mkutano
huo ajisafishe na tuhuma zote
ambazo amekuwa akituhumiwa
na watu.
Chadema ni cham ambacho kwa
muda mrefu kimejijenga kwa
msingi, na ni lazima wapokee mtu
ambaye hawezi kukichafua chama
chao.
Lowassa hakutangaza kujitoa,
wala kujisafisha hadi kwenye
mkutano ambao uliandaliwa na
chadema. Slaa hakuhudhuria ule
mkutano.
Kwenye kila jambo kuna jambo la
kuzingatia. Mtu anayejiunga
popote anakuja kama mtaji au
kama mzigo? Lowassa anakuja
chadema kama asset au liability?
Ijulikane, suala sio urais! Mpaka
siku hiyo Slaa hakuwa amechukua
fomu ya Urais kwenye chama
chake. Slaa hakuwa anamzuia
Lowassa kugombea urais
chadema. Alitaka mgombea
mwenye sifa na uwezo wa kukitoa
Chama cha Mapinduzi.
Hakutamka popote kuwa anataka
kugombea, hata 2010
hakugombea, aliombwa
kugombea! Urais wake binafsi
hauwezi kuikomboa nchi bila
mchango wa jamii nzima.
Mwafrika, [01.09.15 15:45]
Suala la adha Lowaasa ni msizo au
mtaji halikujibiwa hadi siku ya
mkutano tajwa. Wakataka kujua
anapokuja anakuja na akina nani,
ni wafuasi wa aina gani; vijana wa
bodaboda, vijana wasio na ajira
au watu waliosombwa tu, au
wanakuja kwenye mapambano?
Jibu lilikuwa ni kuwa tungepata
wabunge 50 na wenyeviti wa CCM
mkoa wasiopungua 22, wenyeviti
wa CCM wilaya 88. Slaa akakiri
kuwa kama ni hivyo kutakuwa na
tetemeko (la kisiasa).
Wakahitaji majina ya hao
waliotajwa kwa kuwa walikuwa
kwenye mchakato wa kupitisha
majina kwenye chama. KAtibu
mkuu makini huwezi kuchukuwa
watu usiowajua. Hakuna jina
nililopewa mpaka tarehe 25.
Tarehe 25 wakamfata na
kumuambia aitishe Kamati Kuu
ya chama. Akakubali lakini
akatahadjharisha kuwa hajapata
majina na hajapata jibu kuwa
Lowassa ni asset au liability.
Lakini akaitisha kikao kwa kuwa
ni jukumu la kikatiba la katiba.
Mwenyekiti akapiga simu,
anasikia kuwa hajaridhika. Tangu
2004 Slaa hajawahi kugombana na
mwenyekiti wake, isingekuwa
sawa kama wangetofautiana
kwenye kikao rasmi.
Wakakutana na Mwenyekiti,
Gwajima, Lissu na wakajadiliana
mpaka saa 9 mchana. Maneno
kuwa alikuwa anakubaliana na
mpango huo tangu mwanzo SI
KWELI!
Mkutano ukashindikana. Wdau
wakasema waende nyumbani kwa
Lowassa, Slaa akakataa wakaenda
Kamati kuu.
Kikao kikafanyika hadi saa 12
jioni. Ikaundwa kamati ndogo ya
kumshawishi Slaa. Akakataa!
Akaandika barua ya kujiuzulu kwa
kamati, Prof. Safari akaichana
barua yake. Akaandika barua
nyingine kwa Makamu-Zanzibar,
makamu akamuambia kuwa haya
mambo yamepangwa,
asijisumbue!
Wanasema siasa ni mchezo
mchafu, yeye anaaamini kuwa
siasa ni sayansi! Asubuhi ya
kesho akaandika barua,
wasichojua ni kuwa kujiuzulu
hakuhitaji barua. Maneno
yakazuka kuwa Slaa hajaandika
barua!
Upotoshwaji ukaendelea kuwa
Slaa atazungumza na waandishi
wa habari, wengine wakasema
amefungiwa, amefungiwa na
mkewe na kadhalika! Ukweli ni
kuwa alikuwa na Lissu, Gwajima
na Mbowe tangu asubuhi.
Maamuzi aliyoyafanya yanatokana
nadhamiri yake!
Josephine nae ni mwanaharakati,
ana sababu ya kuwa na uchungu.
Alipigwa mwaka 2011 wakati
wengine walijificha! Propaganda
hizo tumeshazisoea!
Kama kuna mwenye ushahidi wa
propaganda hizi aje, audited
report zipo! Josephine halipwi na
chama! Watu wanasema kuwa Slaa
analipwa mil. 7, yeye ameendelea
kula mihogo na maharage kama
walivyoahidi mwaka 2010.
Wana uchungu na harakati!
Kikubwa katika harakati ni
credibilty, jina la chama
kilichojengwa kwa muda mrefu
kisichafuliwe kwa namna yoyote!
Mwanasiasa yoyote hataki
kuchaguliwa, na Slaa nae hataki
kuchaguliwa!
Wanasema kuna maslahi mapana
ya taifa, ni nani anayapima?
Lazima kuwe na kipimo cha
kuapima hayo maslahi badala ya
kutegemea mtazamo wa mtu!
Anafafanua suala la liability sasa!
Wamekuwa waongo kwa kuwa
hakuna kipengele hata kimoja cha
madai ya Slaa kimetekelezwa.
Alisema wabunge waje kabla ya
kura ya maoni ya CCM, kuja
baada ya hapo ni kutafuta
kichaka cha kujificha!
Watanzania wameijenga Chadema
kwa damu yao, rasilimali zao!
Watu hawawezi kukimbilia
kirahisi wakati sio wasafi,
akiwemo Sumaye na wengine.
Nani hajua kama Sumaye ni
fisadi? Kwa muda mrefu Slaa
haongei na Sumaye kwa kuwa
alimtuhumu kwa ufisaidi.
Sumaye ni mtu ambaye
wanahabari walidai kuwa Sumaye
alisema kuwa atahama chama
endapo Lowassa atateuliwa, leo
akageuka!
Leo anamsafisha Lowaasa,
dhambi haisafishwa kwa dhambi.
Anakumbusha jina la Mr. Zero
(jina la utani la Sumaye).
Chama kimepokea makapi, na
katibu alitahadharisha kuwa
chama hakipokei makapi! Hakuna
ambaye alijitoa kwa hiari, wengi
walikuja baada ya kukatwa.
Wenyeviti wengi ni mzigo,
akiwemo Msindai.
Anangoja ajibu amlipue hadharani
kwa kuwa alikuwa mwenyekiti wa
kamati ya bunge hesabu za
serikali z mitaa.
Siku aliyoambiwa aitishe kamati
kuu aliuliza majina, akaambiwa
anakuja chizi! Chizi ni nani, hata
nyie hamumjui! Anaitwa chizi kwa
kuwa ni mwizi wa kura ndani ya
CCM.
Kuna haja gani ya kushindana
kama tunampango wa kuiba kura
pia. Wakamtaja Guninita, nani
asiyemjua udhaifu wake? Hawezi
kuandika hata ukurasa mmoja wa
ripoti, amehama vyama mara
kadhaa!
Mwafrika, [01.09.15 15:45]
Viongozi wa Chadema wamepata
kigugumizi, waseme nani
ameongeza thamani kwenye
chama?
Najua maneno ya kuwa ni lazima
kuiondoa CCM kwanza hata
ikibidi tuweke mkataba na
shetani, mimi ni padre wa Kanisa
Katoliki! Kuwaondoa CCM kwa
namna yoyote hakuleti
maendeleo. CCM itaondolewa kwa
program siriaz, sio kutumia watu
wale wale!
Lazima tujue nini kilifanya
Watanzania waamini chadema,
kwa kuwa waliamini wana misingi
isiyoyumba na uadilifu. Leo
tunasimamia uadilifu?
Wanasema mwenye ushahidi
aende mahakamani. Kama
tusingewatuhumu Mramba na
Yona wasingefikishwa kizimbani.
Chadema imefungwa mdomo kwa
kisingizio cha ushahidi!
Ni bora kukaa kimya kuliko
kupotosha. Anasema nukuu ya
biblia kuhusu wapotoshaji!
Inapofika mahali unapoambiwa
hakuna mwenye dhambi ni
makosa, dhambi haisahihishwi
kwa dhambi nyingine! CCM
wamekuwa waoga, wamewalea
watu hawa kwa muda mrefu!
Kwa Wafrika choo ni neno baya,
kwa wazungu choo ni rest room!
Choo cha Kitanzania huwezi
kukihamisha ndani ya chumba
cha kulala na ukakiita choo,
huwezi kulala kwa kuwa kitanuka,
tena zaidi!
Ufisadi ilikuwa ajenda iliyowapa
umaarufu CHADEMA, leo
wamewachukua. Waanweza kuwa
na ujasiri wa kukemea ufisadi?
Mwaka 2008 Slaa alikuwa bungeni
wakati wa sakata la Richmond,
anafahamu kwa uzuri
anachokimaanisha. Bahati mbaya
waandishi hawasomi makaratasi,
na wabunge wa CCM pia.
Lowassa hatuhumiwi kwa habari
ya Richmond pekee!
Lowassa aliambiwa na Slaa aache
kulalamika, atangaze uhalali au
uharamu wa Richmond, anamtaka
aseme hao 'wakubwa' ni akina
nani? Ni afadhali sifa yake
iharibike kuliko kusema uongo.
Ni aheri kupotea kwenye siasa za
dunia kuliko kusimamia uongo!
Msingi wa kwanza wa Richmond:
Ili uelewe ni lazima urudi kwenye
taarifa ya Kamati ya Mwakyembe,
Slaa alifuatwa asubuhi ya siku ile
kupewa rushwa, anashuru Sitta na
Mwakyembe wajitokeze!
Akamuuliza mtoa rushwa kama
anatoa m.500 kwa mbunge,
atakuwa nazo ngapi? Aliwaambia
Sumaye na Lowassa kuwa rushwa
ni jambo linaloanzia kifuani
kwanza. Mwanzo wa jambo hili ni
taarifa ya Baraza la Mawaziri la
10.2.2006. Kamati ya mwakyembe
iliangalia faili la kikao kile kisha
kuandika ripoti!
Suala hili lilianzia wakati wa
utawala wa mkapa kutokana na
dharura ya umeme nchini,
wakawasiliana na kampuni moja
ya Amerika Kaskazini kwa suluhu
ya muda mfupi ya umeme.
Serikali ya Kikwete ikapokea lile
suala. Wakaruhusu mpango
uendelee, ila kwa kufuata sheria.
Hiyo ilikuwa kauli ya Baraza la
Mawaziri!
Wakati auala lile linaamuliwa,
Lowassa alikuwa Waziri Mkuu! Na
ndie mwenye mandate ya
maamuzi ya Serikali, iweje leo
akane kuhusika?
Taarifa ya Mwakyembe
inapotoshwa! Taarifa ilitaka
Waziri Mkuu ajipime, au bunge
limjadili na kumchukulia hatua.
Lowassa akakimbia kwa kuwa
alijua Bunge lingemfukuza kazi!
Waliioomba tenda walikuwa 26,
waliorudisha walikuwa 8. Kamati
ya Tathmini ikaona hakuna
anayefaa hata mmoja! Waziri
Msabaha akaagiza taarifa ile
ifutwe na tathmini ifanyike upya,
mara ya kwanza, ya pili, ya tatu
na ya nne. Jeuri wa Msabaha
ilitoka wapi?
Baraza likaamua baadaye tenda
iliyopewa kwa kampuni ya kwanza
ifutwe! Lowassa alishiriki!
TANESCO wakatoa ushauriwa wao,
Mamlaka husika ikatafute
internatonal tender ya kununua
turbine!
Lowassa akaingilia mchakato
dakika za mwisho, akamuagiza
katibu muhtasi wake!
Kwanini Lowassa, kwa kuwa
anagombea urais, rais
asiyeaminika hawezi kuchaguliwa!
Lowassa alishawahi kumuita Slaa
kuhusu habari ya Meremeta, na
kumuambia kuwa taarifa yake
inaiaibisha Serikali! Kampuni ya
jeshi imewahi kutengeneza gari,
imehujumiwa na wahuni.
Akamtaka Lowassa amuambie ni
nani aliyehusika?
Akamuita mwingine kwnye
Speaker lounge. Slaa akamuambia
kuwa yeye ni fisadi kichwani,
rohoni mpaka...!
Tunamsifia Lowassa kuwa
an=taleta maji wakti jimbo la
Lowassa halina maji na ufisadi
mkubwa umefanyika kwneye
jimbo hilo. Mnazungumzia shule
za kata wakati wakati hamjua
zimeanza wapi?
Slaa anataja nafasi alizowahi
kushika Afrika. Uamuzi wa
kujenga shule za kata ulifikiwa
mwaka 90 huko Thailand, mpango
huo ukaitwa Education for All, sio
MMES kama unavyoitwa leo!
Mwafrika, [01.09.15 15:45]
Anasoma barua ya Ibrahim
Msabaha kwa Flugence Kazaura,
mkurugenzi wa bodi wa TANESCO!
Mpango ulikuwa kuondoa suala la
umeme mikononi mwa tanesko
kwa kuwa imeshindwa kutekeleza.
Ugomvi wake na Masha ni kwa
kuwa Lowassa alimlaumu Masha
kuingilia mchakato wa serikali,
akawekewa kinasa sauti
chumbani.
Waziri Mkuu haruhusiwi na sheria
kuingilia mchakato wowote wa
tenda.
Kwenye kampuni nane
zilizowasilisha maombi ya zabuni,
Richmond ni kampuni iliyokuwa
mbovu. Ilikuwa ni kampuni ya
steshenari, sio umeme!Wakadai
wana ushirikiano na kampuni
nyingine ya umeme, kampuni
hiyo ikakataa kujihusisha na
Richmond, wala kuzalisha na
majenereta!
Bill Clinton aliwai kukutwa na
kashfa, walitaka kumchukulia
hatua si kwa sababu ya zinaa, bali
kwa kuwa alifanya uongo! Kwa
kuwa alidanganya umma! Hata
sheria za Tanzania zinakataza
kuongopa, hata kesi za uchaguzi
za Slaa zimethibitisha hilo.
Lowassa anadai yeye
alisimamisha tenda, Slaa
anaonesha uthibitisho wa hilo
kwa barua za Lowassa kwenda
kwa Msabaha zinazokanusha hilo,
'Anaisoma'! Waziri Mkuu
aliharakisha mchakato wa tenda,
tofauti na sheria ya PPRA. Barua
imeandikwa miezi mitatu baada
ya mkataba kusainiwa, kwa
maagizo ya Waziri Mkuu.
Tanesko ikaagizwa kusaini
mkataba ambao haikuhusika
kwenye kuujadili! Anaona aishie
hapo... Anaupigia chapuo
mdahalo wa Sitta na Mwakyembe,
anasema Lowaasa nae afike
kuondoa utata na kusema ukweli!
Chadema ni chama kilichotoa
matumaini kwa vijana wengi!
Isifike mahali tukawa washabiki
kama 2005 ambapo watu
waliahidiwa maisha bora,
wakajikaanga kutokana na
ushabiki! Anatoa ushahidi wa
kitakwimu wa mfumuko wa bei...
Slaa ana uchungu kuona chama
alichokijenga, kikifikia hatua ya
kusomba watu kwa mabasi na
malori kisha mkasema mafuriko
hayazuiliki! Hayuko tayari,...
Anakataa kuwa ZEZETA!
Ajenda ya Chadema ni nini,
ilikuwa ni rushwa! Wananchi
waliamini kwa kuwa msingi huo
ndio unakijenga chama!
Sehemu kubwa ya kilichosemwa
Jangwani ni ilani ambayo
ilishaandaliwa tayri, hakuna kipya
kilichosemwa. Kinachomuuma ni
chama makini kuwa kibovu zaidi
ya Chama cha Mapinduzi!
Hatuwezi kujenga maadili tukiwa
na watu wachafu, anaishi na
mwanamke bila kufunga ndoa
kwa kuwa Serikali ya CCM haitaki
afunge ndoa. Kesi yake ililetwa na
mawaziri, waandishi wa habari na
mtu kutoka IKULU. Ndoa
inafungwa na Mungu!
Scotland Yard iliamrisha Lowassa
achunguzwe, inakuwaje leo
tunamtetea? Huu ni ushabiki usio
na vielelezo, Slaa ana ushahidi!
Hakuna ulazima wa kwenda
mahakamani kwa kuwa kesi ya
rushwa ni jinai, ni kesi ya
serikali! Slaa au mwingine hana
locus ya kwenda mahakamani
kwa kesi ya jinai!
Mwakyembe alisema kesi ya jinai
haina mwisho (kama zilizyo za
madai).
chadema iliahidi kusafisha nchi
kwanza endapo itashika dola,
huku maendeleo yakiendelea!
Anasoma barua ya mchakato wa
Richmond kuwa DOWANS.
Kampuni imesajiliwa Costa Rica,
na mwenyekiti asiye na anuani,
simu wala jengo! Siku
iliyosajiliwa, mmiliki alisajili
makampuni mengine 99! Zaidi ya
hayo ana makampuni mengine
zaidi ya 50, DOWANS ni jina tu.
Kampuni haipo!
Dowans sio kampuni halisi huko
Kosta Rika, nchi nzima hakuna
kampuni yenye uwezo wa
kuzalisha umeme kwa kiwango
hicho!
Leo Lowaassa anatuambia
tufunge mdomo, huu ni udikteta!
Anakumbusha sakata lake na
Waziri Marmo...
Mabilioni ya fedha yanalipwa kwa
kampuni ambayo haipo!
Tunapenda ushabiki... Acha sifa
iharibike!
Anasema hataki kuingia kwenye
mambo ya Babu Seya! Vyuo vikuu
vinatumia kesi ya Babu Seya
kama case study. Mtoto mdogo
hawezi kutoa ushahidi
mahakamani, haki inapuuzwa kwa
kuwa mtoto hawezi kutoa
ushahidi!
Kesi ya Ulawiti rais hana
mamlaka nayo, anatoa wapi
kiburi cha kusema kuwa atamtoa?
Aliyeagiza polisi kuingia na polisi
kuingia na mbwa msikiti wa
mwembechai ni Sumaye, akiwa
waziri mkubwa. Leo hii ni mpiga
kampeni wa Lowassa! Leo
tunataka kura kwa namna yoyote!
Ni afadhali kutokuwa na rais wa
aina ya mtu huyu! anayesaka kura
kwa kusaka huruma za watu. Slaa
hayuko tayari kuona hilo
linatokea...
Anahitimisha kwa kusema
hajagusa chochote kuhusu ilani
wala mkakati!
Mwafrika, [01.09.15 15:45]
Kama taifa tuna kazi kubwa ya
kuchambua vitu nje ya
shamrashamra, maneno matamu!
Tumeshaumwa na nyoka,
tusilaghaiwe na maneno ya watu
hawa tena!
Utendaji uliotukuka unapimwa
kwa utafiti, sio kwa ukasuku na
kunukuu maneno ya wanasiasa!
Lowassa alipokuwa Waziri Mkuu,
matatizo ya wakulima na wafugaji
yalikuwepo, alifanya nini?
Lowassa aliwahi kubadili mpaka
wa Monduli na Karatu na
kusababisha mgogoro!
Mkampenia wake, Sumaye
alisababisha matatizo ya ardhi
Mvomero, akipora ardhi ambayo
ilitakiwa yajengwe makao makuu
ya Mvomero! Mengine ya Sumaye
ameyaweka kiporo, hisa zake za
kampuni aziweke wazi kama
Sekretarieti ya Maadili
inavyotaka!
Kutotangaza mali kunatosha
kumtoa mtu ubunge! Sembuse
Urais?
==============================
=========================
Ukweli huwa una tabia ya
kuegemea upande, anasemea
speculation kuwa ameisema
chadema peke yake.
Anasema amestaafu siasa, hana
chama lakini bado anabaki kuwa
mtanzania, mtetezi wa wanyonge
na atabaki hivyo! Ataendelea
kuwatumikia watanzania kadiri
ya Mungu alivyomjalia vipawa!
Kama alivyoombwa kugombea
urais 2010!
Anaweza kuwatumikia Watanzania
bila kuwa na chama!
Anasema kuwa hajapata vitisho
kama alivyopata kipindi hiki,
inazidi hata wakati alipotangaza
List of Shame. Rostam ndiye
anafadhili kampeni za urais wa
Lowassa! Anamnukuu vitisho
vyake! anakiri kuwa maaskofu
wamehongwa, Rostam akiwa
anaona, m60-m300!
Anasema hatenda chama
chochote, anasisitiza! Amejitoa
rasmi siasa za vyama vya siasa...
Ataendelea kuwa msimamiaji wa
anachokiamini!
Anawataka watu aliowataja
watoke hadharani, anatoa baraka
za KIMUNGU kwa nchi na watu
wake!
MASWALI!
Swali: Unawammbia nini
Watanzania kuelekea uchaguzi, ni
rais yupi anafaa?
Amesema hana chama, hampigii
kampeni mtu yoyote! Amesema
anafanya uchambuzi wa madhara
ambayo taifa litapata endapo
watamchagua Lowassa, na kwa
kuwa na uzoefu nao kwa muda
mrefu!
Hataki kufanya kampeni yoyote.
Anawaelimisha Watanzania
kuacha ushabiki
utakaowagharimu! Ni watu
wachache wanoweza kumtaja mtu
kwa majina, kuna tofauti ya
wanaotaja ajenda tu na wanaotaja
majina.
Rostam alimuambia kuwa ana
dakika 5 za kuishi, apige magoti
na kusali! Aliweka roho yake
rehani kwa ustawi wa taifa
hili...Anakumbusha ya
Mwembeyanga na namna Usalama
wa Taifa walivyokuwa na tension.
Magazeti mengi yaliogopa hata
kuandika habari, isipokuwa
MWanaHalisi!
Swali: Siasa ingekuwa asset kama
angekuja na wabunge kadhaa.
Angekuja kama asset, mengine
yangesafishika?
Kulikuwa na vigezo viwili, ama
asset na liability, yaani hayo
madhambi yote aliyoyasema.
Baada ya hayo wangefanya
tathmini kama anapokelewa au
hapokelewi. Anatoa mfano wa
Shirikisho la Afrika Mashariki na
nchi zinazotaka kujiunga!
Swali: Waliopokelewa ni makapi.
Je wewe ulikuwa kapi 95?
Anauliza kama watu wanaamini
yeye alikuwa kapi? Tupime
vigezo... Makapi ni watu
waliokataliwa na watu wao baada
ya kuwa wabunge kwa muda
mrefu. CCM wakasema kuwa
hakuwa mwenzao: hakuwa
anahonga, hakuwa anapokea
rushwa na kadhalika!
Kuingia kwa tiketi ya Chadema
ulikuwa ukombozi kwake!
Swali: Umetangaza kustaafu siasa,
una kadi za vyama viwili.
Unazirudisha au unakaa nazo?
Watanzania tuelimika, kadi sio
uanachama. Kadi ni mali ya
mwanachama, unaweza kuichoma,
kuweka kumbukumbu au
vyovyote, sawa na kadi ya ndoa
ambayo hairudishwi hata kama
ndoa itavunjika. Tuulize maswali
ya kujenga.
Swali: Anaoneka baada ya kukosa
urais anamshambulia Lowassa!
Wapi Slaa alichukua fomu ya
Urais, hakuwa na nia na urais
wala hawezi kukasirika. Tuache
ushabiki, tuwe na mtiririko na
kuzingatia hoja! Mwandishi awe
msikivu sana... Ameeleza tangu
mwanzo, hana chuki wala ugomvi
na mtu yoyote!
Chama cha Mapinduzi kilishakuja
kumpa ofa kadhaa kuachia jimbo
la Karatu, akaweka sharti la
mkataba wenye sahihi za watu
watatu; Rais, Slaa na Yesu Kristo.
Swali: Kama wewe uliweza
kuhama, wengine nao hawawezi?
Dr. Slaa hakuwa na uchafu
wowote, tatizo halikuwa kuhama
chama, tatizo ni watu wa aina
gani wanahama chama?
Swali: Unahamasisha uwazi,
mbona wewe umemficha muovu
mmoja?
Silaha haziwekwi zote mezani,
amewaomba anaowatuhumu
wajitokeze!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni