other blog

Jumapili, 30 Agosti 2015

Soma droo ya uefa hapa katika mechi za makundi Man Utd yapeta, Arsenal kwa Bayern Arsenal imetupwa kwa Bayern Munich wakati Manchester United ikipewa vibonde katika mashindano ya


Mshambuliaji wa FC Barcelona, Lionel
Messi akipokea tuzo ya mwanasoka bora
wa Ulaya kutoka kwa rais wa UEFA,
Michael Platini (kulia) baada ya kumshinda
mpinzani wake Cristiano Ronaldo wa Real
Madrid jana wakati kwa kupangwa kwa
ratiba ya Ligi ya Mabingwa UEFA jijinin
Monaco.
Monaco, Ufaransa. Arsenal imetupwa
kwa Bayern Munich wakati
Manchester United ikipewa vibonde
katika mashindano ya Ligi ya
Mabingwa, huku Lionel Messi akitwaa
tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka
wa Ulaya.
Katika ratiba hiyo iliyopangwa jana
jijini Monaco inaonyesha Arsenal
inakutana tena na Bayern kwa mara
ya tatu ndani ya misimu minne
mfululizo.
Gunners pia itacheza na Olympiakos
ya Ugiriki na Dinamo Zagreb ya
Croatia.
Manchester United imepangwa
kuchezwa na PSV Eindhoven mechi
itakuwa kimrudisha mshambuliaji
Memphis Depay kucheza na timu yake
ya zamani.
Chelsea imetupwa kwa Porto, klabu
ambayo Jose Mourinho alitwaa taji
lake la kwanza la mashindano hayo
2004.
Manchester City itawavaa mabingwa
wa Serie A, Juventus pamoja na
mabingwa wa Europa Ligi, Sevilla na
Borussia Monchengladbach.
Mabingwa watetezi Barcelona
wakipangwa katika Kundi E, pamoja
naza Bayer Leverkusen, Roma na
BATE.
Barca, ambao wametwaa taji hilo mara
tano katika hisoria ya timu hizo
wataanza utetezi wa nyumbani
wakisaka heshima mpya ya kuvunja
rekodi ya kulinyakua taji hilo mara
nyingi.
Juventus, ambao walicheza fainali ya
msimu uliopita dhidi ya Barca,
wamepangwa katika Kundi D,
sambamba na timu za Manchester
City, Sevilla na Borussia
Monchengladbach.
Katika Kundi A, mabingwa wa
Ufaransa, Paris Saint-Germain
wataumana na mabingwa wa
kihistoria barani Ulaya, Real Madrid
pamoja na timu za Shakhtar Donetsk
na Malmo.
Wakifuzu kwa kishindo katika hatua ya
makundi, Manchester United nao
wamerudi katika fainali hizo kwa kasi
baada ya kukosa mashindano hayo
kwa msimu mmoja.
Man United wametupwa katika Kundi
B wakiwa na timu za PSV, CSKA
Moscow na Wolfsburg ya Ujerumani.
Katika Kundi C, mabingwa wa Ureno,
Benfica watakuwa na mabingwa wa
zamani wa Hispania, Atletico Madrid,
Galatasaray na Astana.
Vinara wa Ligi Kuu England msimu
huu, Manchester City wamepangwa
kuanza mashindano hayo katika Kundi
D, ambalo pia lina timu za Juventus,
Sevilla na Borussia Monchengladbach.
Bayern Munich, ambao ni mabingwa
wa Ujerumani waliocheza fainali ya
Ligi ya Mabingwa 2012 dhidi ya
Chelsea, wamepangwa kuanza
kampeni za msimu huu katika Kundi F
pamoja na timu za Arsenal,
Olympiacos na Dinamo Zagreb.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu
England, wao wamepangwa katika
Kundi G, wakiwa na Porto, Dynamo
Kiev na Maccabi Tel-Aviv ya Israel.
Katika Kundi H, mabingwa wa Urusi,
Zenit, Valencia, Lyon na Gent. Ligi ya
Mabingwa Ulaya msimu huu
inatarajiwa kuanza mwezi ujao.
Katika hatua nyingine, mshambuliaji
wa kimataifa wa Argentina
anayeichezea Barcelona, Lionel Messi
amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa
Ulaya wa mwaka.
Messi ameibuka na ushindi katika tuzo
hiyo akiwabwaga wenzake wawili
Cristiano Ronaldo wa Real Madris na
mshambuliaji mwenzake wa Barca,
Luis Suarez.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni