other blog

Jumamosi, 22 Agosti 2015

‘Utatu’ huu kumaliza mechi Azam, Yanga Baada ya tambo za muda mrefu kuhusu ubora wa vikosi vyao, Azam na Yanga zina silaha hatari tatu

Dar es Salaam. Baada ya tambo za
muda mrefu kuhusu ubora wa vikosi
vyao, Azam na Yanga zina silaha hatari
tatu kila moja zinazoweza kumaliza
mechi mapema.
Mbinu za makocha Hans Pluijm na
Stewart Hall kwa dakika 90 zinaweza
kutuliza mizuka ya mashabiki wao
wakati timu zao zinapofungua msimu
wa Ligi Kuu.
Katika mchezo huo, Yanga italazimika
kuwa makini na washambuliaji watatu
wa Azam, John Bocco, Kipre Tchetche
na chipukizi Farid Mussa wanaoweza
kubadili matokeo wakati wowote.
Ukuta imara wa Azam ambao
haujaruhusu bao kwenye mechi zaidi
ya kumi ukiwa chini ya Serge Pascal
Wawa, Aggrey Morris, Said Morad
unatakiwa kuwa makini, kuwachunga
Donald Ngoma, Simon Msuva na Amissi
Tambwe, ambao wamekuwa chaguo la
kwanza Yanga, ingawa pia anaweza
kutumika Malimi Busungu.
Yanga na Azam zimekuwa na upinzani
zinapokutana kwenye mchezo wa Ngao
ya Jamii, Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam, zina na kumbukumbu ya
matokeo ya sare ya 0-0 kwenye
mchezo wao wa mwisho, robo fainali
ya Kombe la Kagame, ambao
uliamuliwa kwa penalti 5-3 zilizoipa
ushindi Azam.
Timu hizo zinakutana mara ya tatu
mwaka huu, baada ya awali kwenye
mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Azam
iliishinda Yanga 2-1, kisha zikakutana
kwenye mashindano ya Kagame na
Azam kushinda kwa penalti 5-3.
Hata hivyo, Azam haina rekodi nzuri
dhidi ya Yanga kwenye mechi za Ngao
ya Jamii, mara mbili timu hiyo
imepoteza kwa kufungwa bao 1-0,
mwaka juzi na pia 3-0 mwaka jana.
Kurejea uwanjani kwa nahodha Nadir
Haroub ‘Cannavaro’, Tambwe na
Ngoma waliokuwa majeruhi tangu
timu yao (Yanga) ilipokuwa kambini
Mbeya kumempa ahueni kocha Pluijm
anayeona kikosi chake kuwa
kiimekamilika.
Pluijm ambaye hupenda kutumia
mifumo ya 4-3-3 au 4-4-2, alisema
wako kamili na hawana hofu leo,
watalipa kisasi cha penalti 5-3 za
Kombe la Kagame. Kocha wa Azam,
Stewart Hall, hupenda kutumia
mfumo wa 3-5-2, amekiri kuwa mechi
itakuwa ngumu.
-

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni