Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)
limemfungia mwanamuziki wa Bongo
Fleva, Zuwena Mohamed maarufu
kama Shilole kujihusisha na shughuli
za sanaa kwa muda wa mwaka mmoja.
Mwanamuziki huyo anayejulikana pia
kama Shishi Baby amekumbwa na
dhahama hiyo baada ya kusambaa kwa
picha zinazomuonesha akicheza
jukwaani akiwa katika mavazi
yanayokinzana na maadili ya
Kitanzania akiwa nchini Ubelgiji.
Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey
Mngereza amezungumza na
Mwananchi Digital kwa njia ya simu
leo na kusema hatua hiyo
imechukuliwa baada ya awali kumpa
onyo kwa matukio ya kupanda
jukwaani kufanya sanaa akiwa katika
mavazi yasiyozingatia maadili ya
Kitanzania.
“Awali tulimuonya kwa vitendo hivi,
akakiri kosa na kuahidi kwa maandishi
kuwa hatarudia kufanya hivyo”
alisema na kuongeza: “Hata hivyo,
wadau wa muziki watakumbuka
alichokifanya nchini Ubelgiji. Lilikuwa
tukio la aibu kwake kama msanii, aibu
kama mwanamke na aibu kama
Mtanzania” alisema.
Amewataka wasanii kujitathimini
kabla ya kupanda jukwaani na kuonya
kuwa Basata itaendelea kuchukua
hatua kama hizo dhidi ya msanii
yeyote atakayebainika kuvunja/
kukiuka maadili ya nchi. Shilole
amekiri kupokea barua kutoka Basata
akisema, hivi sasa yuko kwenye
majadiliano na mwanasheria wake na
kusema anakusudia kukata rufaa
kupinga kufungiwa huko. “Mashabiki
wangu watulie kwani hii ni
changamoto, tunaifanyia kazi kila kitu
kitakuwa sawa hivi karibuni” alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni