Mmoja wa wajasiriamali akionyesha
bidhaa zake katika moja ya maonyesho ya
biashara. PICHA|MTANDAO
ADVERTISEMENT
Moshi. Taasisi ya Vyuo Vikuu vya
Afrika Mashariki na Kusini imeanza
kutoa elimu ya uendeshaji biashara
kwa wajasiriamali wadogo mkoani
Kilimanjaro.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo,
Profesa Ted Maliyamkono aliyasema
hayo jana, wakati wa ufunguzi wa
mafunzo ya wajasiriamali wadogo 150
yaliyolenga kuwawezesha kurasimisha
biashara zao ili wapate mkopo na
kukuza biashara.
Alisema wafanyabiashara hao
hukumbana na changamoto nyingi
zikiwamo kukosa maeneo mwafaka ya
biashara, kupoteza mitaji pamoja na
rushwa.
Akizungumza katika mafunzo hayo,
mjumbe wa bodi kutoka Taasisi ya
Financial Sector Deepening Trust,
Erick Masinda alisema, utafiti
waliofanya umegundua kuwa, kuna
biashara ndogo na kati zinazofikia
milioni tatu, lakini ni asilimia 12 ya
wafanyabiashara wadogo na wakati
ambao wapo kwenye mfumo rasmi wa
kifedha.
Masinda alisema robo tatu ya biashara
hizo hazina usajili na kwamba
wafanyabiashara wengi hawatunzi
kumbukumbu zao na hawana elimu ya
uendeshaji pia.
Akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa
Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama
aliupongeza mkoa huo wa kuwa
miongoni mwa mikoa kumi
iliyoteuliwa na taasisi hiyo kupewa
elimu ya ujasiriamali na kusema hiyo
itawasaidia kuacha kuendesha
biashara zao kiholela.
Katika taarifa iliyosomwa kwa niaba
yake na Mkuu wa Wilaya ya Rombo,
Lembris Kipuyo alisema, ongezeko la
ukosefu wa ajira na uhaba wa huduma
za jamii ni kikwazo cha maendeleo
nchini.
Alisema kwa mji wa Moshi tatizo la
ajira limechangia vijana wengi
kujihusisha na uzururaji na uhalifu na
ili wajikwamue, Serikali itoe agizo kwa
halmashauri zote kutenga asilimia
tano ya mapato kwa ajili ya vijana
kupata mikopo na kujikwamua
kiuchumi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni