Mgombea urais wa CCM, Dk John
Magufuli akihutubia wafuasi wa chama
hicho waliofurika katika Viwanja vya
Jangwani, Dar es Salaam wakati wa
uzinduzi wa kampeni za chama hicho jana.
Picha na Edwin Mjwahuzi
Dar es Salaam. Mgombea urais wa
CCM, Dk John Magufuli amefungua
pazia la kampeni za chama hicho
kwenye Viwanja vya Jangwani katika
tukio lililohudhuriwa na maelfu ya
wananchi, huku akieleza mambo 25
atakayoyafanya iwapo Watanzania
watamchagua kuwa Rais wa Awamu ya
Tano.
Huku akitumia maneno: “Mimi kazi
tu”, “Tanzania ya Magufuli ni ya
viwanda”, Dk Magufuli aliyetumia
dakika 53 kueleza sera zake, kuanzia
saa 11.40 hadi 12.33 jioni alisema
Watanzania wanataka kitabu kipya cha
mabadiliko na yeye na mgombea
mwenza, Samia Suluhu ndiyo
wanaoweza kuyaletea.
Mgombea huyo wa urais wa CCM
aliahidi kuanzisha mahakama
maalumu ya kusikiliza kesi za rushwa
na ufisadi, kumaliza tatizo la
wanafunzi wa elimu ya juu kukosa
mikopo, kuhakikisha mama lishe
hawabughudhiwi, kusimamia haki za
wasanii, kulinda Muungano na
usalama wa nchi.
Aliahidi kutoingilia utendaji kazi wa
Bunge na Mahakama, kuheshimu
mawazo ya vyama vingine vya siasa,
kuimarisha vyombo vya ulinzi na
usalama, wafanyabiashara wadogo na
wakubwa wote kulipa kodi, kuendeleza
kilimo, mifugo, uchimbaji wa madini,
majisafi na elimu bora.
Nyingine ni kusimamia nishati ya gesi,
ujenzi wa barabara, reli, kuboresha
sekta ya utalii, kuimarisha uwekezaji,
kuwasaidia walemavu na kusimamia
uhuru wa habari.
Mkutano huo ulioanza rasmi saa 9.30
alasiri ulihudhuriwa na viongozi
mbalimbali wa Serikali na CCM,
wakiongozwa na Mwenyekiti wake,
Rais Jakaya Kikwete na marais
wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na
Benjamin Mkapa. Wengine ni Waziri
Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba na
Salim Ahmed Salim.
Ahadi alizotoa
Mgombea huyo alitoa ahadi
mbalimbali ikiwamo ajira akisema:
“Ninataka Watanzania wapate ajira,
kazi ya Serikali itakuwa kukusanya
kodi tu. Viwanda vinaweza
kutengeneza ajira kwa asilimia 40 hasa
kwa vijana wanaohitimu vyuo
mbalimbali nchini.”
Kuhusu ubinafsishaji, alisisitiza: “Kuna
viwanda vilibinafsishwa sasa wahusika
wasipoviendeleza wajiandae
kuvirudisha haraka.”
Mbali na kurejesha viwanda
vilivyobinafsishwa, alisema akipewa
ridhaa hiyo atahakikisha chini ya
uongozi wake, anajenga viwanda vingi
vipya, akiainisha vile mahsusi kwa
shughuli za kilimo, mifugo, kusindika
nyama na madini.
Alitaja kipaumbele kingine kuwa ni
kilimo na kwamba atahakikisha sekta
hiyo ambayo ndiyo mhimili wa uchumi
inaendelezwa.
“Tutaleta vitendea kazi, pembejeo na
vifaa vingi vya kisasa na vya kutosha
kwa wakulima… kama nilivyosema
hapo awali, tutajenga viwanda kwa
ajili ya wakulima pia.
Mbunge huyo wa zamani wa Chato
alisema pia kipaumbele kingine katika
Serikali yake ni kuhakikisha kuwa
wananchi wa mjini wanapata majisafi
na salama kwa asilimia 95 na wananchi
wa vijijini wanapata maji kwa asilimia
85.
Kuhusu afya alisema: “Tutahakikisha
tunakuwa na vituo vya afya, zahanati
na hospitali katika maeneo mbalimbali
kwa sababu tunaamini maendeleo ya
kweli hayawezi kupatikana kama
wananchi hawana afya bora.”
Kipaumbele kingine ni mikopo kwa
wanafunzi wa elimu ya juu akisema
watakuwa wanapata mikopo kwa
wakati bila kuchelewa na kwamba
watajikita pia katika kujenga hosteli
kwa wanafunzi wa vyuo.
“Mishahara ya walimu na wafanyakazi
wote tutaishughulikia. Hata madereva
haki zao za msingi lazima ziangaliwe,”
alisema huku akishangiliwa na wafuasi
wa chama hicho.
Mgombea huyo alisema anafahamu
kero ya msongamano wa magari katika
Jiji la Dar es Salaam na kwamba
maendeleo ya kweli yatapatikana
kama changamoto hiyo itafanyiwa
kazi.
“Tutaunganisha mikoa yote kwa
barabara zenye viwango vya lami na
pia tutajenga barabara za juu saba
jijini hapa,” alisema Magufuli.
Alisema akipewa ridhaa hiyo
itashughulikia suala la reli kwa
kujenga reli ya kisasa kwa viwango vya
Standard Gauge” na kuboresha
bandari na usafiri wa anga.
Kuhusu maliasili, alisema ni
kipaumbele katika Serikali yake
endapo akipewa ridhaa ya kuongoza
nchi huku akieleza kukerwa na
ujangili... “Ninapata shida sana
ninapoona meno ya tembo yanauzwa
Ulaya halafu unaambiwa yanatoka
Tanzania… sasa unajiuliza yanapitaje?”
Alisema ili kushughulikia suala hilo
atahakikisha watendaji wa sekta hiyo
wanaboreshewa masilahi yao ili
wachangie mapato ya nchi.
Aliahidi Serikali yake kuwa rafiki wa
wawekezaji na kwamba italinda
masilahi ya wafanyabiashara.
Mgombea urais huyo aliahidi kuwa
atalinda uhuru wa habari na atafanya
kazi na waandishi wa habari siyo tu
wakati wa kipindi cha kampeni, bali
hata baada.
Katika ahadi zake, Dk Magufuli
hakuwaacha wasanii, alisema
atahakikisha wanapata hakimiliki na
kuhakikisha wao pamoja na
wanamichezo wanaanzishiwa mfuko
kwa ajili ya kuwasaidia k
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni