other blog

Jumamosi, 22 Agosti 2015

Saa 48 hatari za Msenegali wa Simba Mshambuliaji mpya wa klabu ya Simba, Papa Niang kutoka Senegal ana saa 48 za kuthibitisha ubora


Mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal,
Papa Niang akiwasili Uwanja wa Ndege wa
Julius Nyerere, Dar es Salaam jana tayari
kwa majaribio kwenye klabu ya Simba.
Picha na Said Khamis
Dar es Salaam. Mshambuliaji mpya
wa klabu ya Simba, Papa Niang
kutoka Senegal ana saa 48 za
kuthibitisha ubora wake, vinginevyo
ataondoka kama wengine
waliomtangulia.
Simba imepanga kumpa mkataba wa
miaka miwili kwa sharti la kuonyesha
kiwango cha kuridhisha kwenye
mchezo wa Jumatatu dhidi ya Mwadui
ya Shinyanga.
Kwa upande wake, Niang alisema jana
baada ya kuwasili nchini,” Nimekuja
kufanya kazi na kama ni majaribio
wasipoteze muda, najiona tayari
nimefuzu.
“Nimecheza soka Ulaya kwa miaka
minane na kwenye mashindano
makubwa kwanini nishindwe kucheza
hapa ?
Alijigamba kuwa yeye ni
mshambuliaji mwenye uwezo wa
kufunga mabao na pia anaweza
kutengeneza nafasi za mabao kwa
wenzake.
“ Mpaka sasa nina rekodi nzuri ya
ufungaji wa mabao nikiwa na klabu ya
Al Shabab ya Kuwait, nimefunga
mabao manane msimu huu.
Nimetengeneza mabao mengine 11 na
hii ni kutokana na nafasi niliyokuwa
nikipangwa ya nyuma ya
mshambuliaji wa kati.
“Sioni kama majaribio ni saizi yangu
kwa sababu ninajielewa na ninajua
uwezo wangu. Sijui kwanini Simba
wanapoteza muda,” alijinasibu.
Aliongeza, “ Ninacheza nafasi zote za
ushambuliaji. Kazi itakuwa kwa kocha
kuamua nicheze wapi, kimsingi,
nitafunga mabao nikiwa kokote.
Anipange kama mshambuliaji wa
pembeni, iwe kulia au kushoto
atafurahi, lakini akiniweka katikati
atanipenda zaidi.”
Wakala wa mchezaji huyo, Massouka
Ekoko , raia wa Cameroon alisema, “
Niliambiwa Simba inahitaji mfungaji,
lakini pia mchezaji anayeweza
kumudu kufunga akitokea kushoto au
kulia mwa kiwanja na Niang
nimemleta kwa kuwa najua
atawasaidia. “
Tayari, uongozi wa klabu hiyo
umemwachia jukumu kocha Dylan
Kerr kuamua mchezaji mmoja wa
kigeni atakayetemwa kwenye kikosi
hicho endapo Niang atafuzu na kusaini
mkataba.
Msenegali huyo aliwasili Dar es Salaam
jana tayari kufanya mazungumzo ya
awali na uongozi wa klabu hiyo kabla
benchi la ufundi la timu hiyo kuamua
kumpima uwezo kwenye mchezo wa
kirafiki dhidi ya Mwadui ili
kujiridhisha kabla ya kumpa mkataba.
Rais wa Simba, Evance Aveva
aliliambia gazeti hili jana kuwa
mchezo wa Jumatatu dhidi ya Mwadui
inayonolewa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’
ndiyo utaamua kama Niang atabaki
Simba msimu huu, ama la.
Aveva alisema kocha Kerr ndiye atatoa
uamuzi wa mwisho baada ya mchezo
huo na endapo ataridhika na kiwango
chake atapewa mkataba wa miaka
miwili.
Endapo Niang atafuzu, Simba
italazimika kupunguza mchezaji
mmoja wa kigeni ili kubaki nao saba
kama kanuni za TFF zinavyoelekeza.
Hata hivyo, Aveva alisema jukumu hilo
wamelikabidhi kwa kocha wao na
baada ya mchezo wa Jumatatu atatoa
msimamo wake.
Wachezaji wa kigeni waliopo Simba ni
Emery Nibomana na Kelvin
Ndayisengaa ( Burundi), Justice
Majabvi (Zimbabwe) , Hamis Kiiza,
Simon Sserunkuma na Juuko Murshid
(Uganda) na kipa Vincent Angban,
raia wa Ivory Coast.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni