other blog

Jumapili, 30 Agosti 2015

By rizik malya ... Logarusic amrejesha Kenya Ivo Mapunda Kocha wa zamani wa Simba, Zdravko Logarusic amempa kibarua kipa wa zamani wa klabu hiyo, Ivo


Ivo Mapunda
Dar es Salaam. Kocha wa zamani wa
Simba, Zdravko Logarusic amempa
kibarua kipa wa zamani wa klabu hiyo,
Ivo Mapunda (pichani) kwa kukubali
kumsajili katika klabu yake, AFC ya
Leopards ya Kenya.
Mapunda aliliambia gazeti hili jana
kuwa muda wowote atasaini kuichezea
klabu hiyo ya Ligi Kuu Kenya baada ya
kutoswa na Wekundu wa Msimbazi.
Ivo, ambaye alidaiwa kuchukua Sh10
milioni za awali kwa ajili ya kusaini
mkataba mwingine na klabu hiyo
aliachana na klabu hiyo kwa madai ya
viongozi wa klabu hiyo kuwa aligoma
kusaini fomu za usajili.
Kipa huyo mahiri na mzoefu aliliambia
gazeti hili kuwa ameitwa na Logarusic
kwa ajili ya kufanya mazungumzo na
kisha kusaini mkataba.
“Logarusic alinifundisha wakati ule
nikiwa Gor Mahia na alivyokuja Simba
nami nikamfuata, kisha akaondoka na
kujiunga na AFC Leopards na ameniita
ili niende huko,” alisema.
Pia, Ivo aliwataka wachezaji nchini
kuwa makini na mikataba yao na kama
wanashindwa kujisimamia wenyewe
inafaa watafute watu wa karibu wa
kuwasimamia kwani viongozi wengi wa
klabu kubwa ni wajanja wajanja.
“Nawashauri wachezaji wawe makini
kwenye suala la mikataba, wawe
makini kuisoma vizuri mikataba yao
na kama wakishindwa watafute
wasimamizi wa karibu.
“Wachezaji wengi wamekumbana na
matatizo ya mikataba yao na hiyo
inatokana na kutoisoma vizuri
mikataba hiyo na kuielewa ndipo
usaini,” alisema.
Aliongeza: “Viongozi wengi ni wajanja
katika masuala ya mikataba, baadhi
yao siyo wa kweli na kuna masuala ya
bima na mengine muhimu kwenye
mikataba hawayafuti, wanachoangalia
ni kukutumia wakishakuchoka
wanakuacha na mchezaji ukiwa
mkweli kwao wanakuweka pembeni.”
“Mchezaji ukipata timu inakupa
maslahi mazuri iwe nje ya nchi au
hapa nyumbani wewe nenda tu
hakuna haja ya kujishauri kwani mpira
ni biashara.
“Using’ang’anie sehemu moja hata
kama haina masilahi kwako hata kama
unacheza nje na hakuna masilahi na
nyumbani kuna timu imekuita
inalikupa vizuri rudi,” alieleza.
Kuhusu kuachwa na Simba, alisema ni
mizengwe, lakini binafsi hajali kwani
hawezi kukosa timu ya kucheza.
“Kuna maneno mengi yametokea,
naamini ni mizengwe imesababisha
yote haya kwani iliamriwa tukae kikao
cha pamoja mwisho wa siku
nikaambiwa sina ushirikiano.
“Wakati naendelea kuuguza majeraha
kuna kiongozi wa Simba alitumwa
kuniletea fomu za usajili, lakini
hakunitafuta na baadaye nikasikia
amerudisha majibu kwa viongozi kuwa
sionekani na kamati ya usajili ikaamini
bila kuniita ili nijitetee.
Aliongeza: “Nilishangaa sionekani vipi
wakati mimi nipo kila siku na wengi
walifahamu kuwa ninaumwa, lakini
isitoshe hata huyo kiongozi
aliyetumwa kwangu sina mazoea naye
na hata kuhusu masuala ya mimi kuwa
majeruhi hakuwa anafuatilia sasa sijui
alikuwa na lengo gani la kurudisha
majibu kama hayo.”
Alisema hakuwa na haraka ya kusaini
mkata mpya wakati mkataba wake
umebaki miezi michache kwa sababu
alihakikishiwa kuwa ataendelea
kuitumikia timu hiyo msimu ujao.
“Sikuwa na haraka ya kusaini mkataba
mpya baada ya mkataba wangu kubaki
miezi michache kwa sababu sikuwa na
wasiwasi, waliniambia kuwa
wataendelea na mimi, hivyo sikuona
haja ya kusaini mapema kabla ya
mkataba wangu haujaisha na isitoshe
tayari walishanipa kiasi cha fedha,”
alisema kipa huyo aliyewahi kuichezea
pia Yanga miaka michache iliyopita na
baadae kwenda nje ya nchi.
-

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni