other blog

Ijumaa, 14 Agosti 2015

Jifunze kuweka kumbukumbu vizuriWiki mbili zilizopita, tulijifunza kupitia safu hii ya mbinu za mafanikio, tulijifunza kuh imeandaliwa na dennic lyamuya


Wiki mbili zilizopita, tulijifunza kupitia safu hii ya mbinu za mafanikio, tulijifunza kuhusu umuhimu wa kutumia muda kwa manufaa.Tulijifunza mbinu mbalimbali za kukabiliana na uzembe katika kutumia muda pamoja na mbinu za namna ya kuutumia kikamilifu.Lengo ni kufanya muda ukutumikie ili upate tija kimaisha na si wewe ukimbizanena muda, kiasi kwamba unaanzakulalamika kuwa “muda si rafiki.”Kumbukumbu ni muhimu katika kurahisisha mambo yako ili yaende haraka kuliko muda unavyokwenda. Leo nitazungumzia juu ya namna ya kuimarisha kumbukumbu.Mwaka 2009 nilipokuwa Chuo Kikuu cha Mzumbe, wakati somo la IT (Information Technology), nilipata wazo kamakweli vichwa vyetu vingekuwa ni kompyuta, ningewashauri watu waongeze chip (hard disk au kihifadhi kumbukumbu), ili kuongeza kiwango cha kutunza kumbukumbu vichwani lakini ubongo wa mwanadamu ni mashine kubwa ambayo ipo na mambo chungu nzima kuliko kifaa hiki cha kompyuta ama mashine yeyote ile ya kisasa.Hivyo basi kama mtu anataka kuboresha kumbukumbu kichwani anahitaji maarifa au juhudi fulani ili aweze kuwa na namna nzuri ya kutunza kumbukumbu.Mathalan ni kama mtu anayekwenda kufanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito, kadiri anavyozidisha na kuweka juhudi,ndiyo mishipa na misuli yake inavyozidi kutanuka hivyo hata katika kuboresha utunzaji wa kumbukumbu kwenye ubongo, inafanya kazi sawa.Nina maana kwamba ukiweka maarifa na juhudi fulani ndiyo uwezo wako unaongezeka. Kuna aina kadhaa ya vitu vya kutunzia kumbukumbu, mfano taswira yapicha, sentensi na mizaha.Zipo namna mbalimbali za kuboresha utunzaji wa kumbukumbu vizuri. Hizi ni kama vile mazoezi ya mara kwa mara, kudhibiti msongo wa mawazo, kulala vyema, kutovutasigara, kulala kwa ukamilifu, kula vizuri na kwa usahihi, pangilia taarifa zako, penda kuelewa na weka uhusiano kati ya mambo mapya na ya zamani.Mazoezi ya mara kwa mara husaidia kuongeza oksijeni kwenye ubongo, hivyo kupunguza majanga ambayo husababisha kupoteza kumbukumbu, mfano wa magonjwa kama kisukari na matatizo ya moyo (cardiovascular).Jaribu kudhibiti msongo wa mawazo. Hali hiyo husababisha kuharibu sehemu ya ubongo ijulikanayo kama hippocampus. Vilevile msongo wa mawazo husababisha kuwa ni vigumu mtu kulifuatilia jambo kwa umakini, hapa nashauri kufanya tafakuri au ama kama walivyozoea watu kusema; kitmeditation.Hii inasaidia kutatua tatizo au kuwa na muda wa angalau kwa siku mara mbili mtindo wa kuvuta pumzi ndani na kisha kutoa nje na wakati ukiingiza pumzi ndani shikilia angalau dakika moja hivi kisha itoe nje. Kwa kufanya hivyo utaweza kuondokana na msongo wa mawazo.Kuwa na tabia ya kulala vyema. Kulala ni muhimu katika kuimarisha utunzaji mzuri wa kumbukumbu, ulalaji wa chini ya saa saba unasababisha mtu kushindwa kufuatilia jambo kwa umakini.Pia, ulalaji wa kupitiliza saa nanemfano mtu kulala saa tisa na kuendelea husababisha matatizo ya mwili kuuma, kujihisi kuchoka au uvivu na hivyo kusababisha mtu tu kukaa katika hali kama ya kibumbuazi bila kufanya jambo lolote na kufikiri vyema.Acha tabia ya kuvuta sigara. Uvutaji wa sigara huzidisha matatizo katika viungo vyetu na husababisha mtu kupata magonjwa ya mshituko pia kuziba mishipa inayopeleka oksijeni kwenye ubongo.Kula vizuri na kwa usahihi. Tafiti zinaonyesha kuwa kuna aina ya vyakula vinavyosaidia kuboreshautunzaji wa kumbukumbu, mfano matunda, mboga za majani, wanga, vitamini B, B6 naB12.Mfano spinachi, meloni, maharagwe ya soya, matunda jamii ya ndimu, vitamin C na E mfano nyanya nyekundu, karanga, mbegu, samaki wa maji baridi na mafuta ya walnut.Husisha viungo vingi ikiwezekana. Hata kama wewe unajifunza kwa kutazama soma unachojifunza kwa sauti, kile unachotaka kukumbuka, hata kama unaweza kukiwekea katika sauti ya kuimba ili ukiimbe, fanya hivyo. Hapo utakuwa umehusisha viungo kama macho, mdomo, mkono na hii inasaidia mambo yakiwa mengi, hujui la kufanya na kadhalika.Pangilia taarifa zako. Jaribu kuandika taarifa zako kwenye kitabu kwa mpangilio wa tarehe na taarifa nyingine muhimu.Penda kuwa mwelewa, achana na tabia ya kukariri, anza na kuweka tabia ya kuelewa jambo na kulielezea kwa lugha yako mwenyewe.Husisha kile ulichokielewa na kwa kulinganisha na taarifa mpya. Kwa kuunganisha au kuoanisha na taarifa ile uliyoelewa kabla inasaidia kutengeneza kitu kimoja kikamilifu.Kulingana na tafiti mbalimbali, wanadamu wengi hutumia asilimia ndogo ya ubongo wao. Hii hutokana na uvivu au kukosamuda wa kupangiliwa vyema, mfano mwanadamu wa makamo hutumia asilimia tano ya akili yake au chini ya hapa kwa wanadamu wa kawaida. Hii nyingine hubaki bila kutumika. Anza sasa kuutumia ubongo wako ukuletee mabadiliko. Wewe una uwezo mkubwa wa kutunza kumbukumbu na kuweza kuleta mabadiliko kimaisha. Anza leo.-

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni