Mwanza.Hakuna shaka ushindani msimu ujao utakuwa baina ya makocha wa kigeni dhidi ya wazawa kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.Hadi sasa, makocha wa kigeni wameendelea kupata ulaji baada ya klabu ya Toto Africans ya hapa kumleta Mjerumani Martin Glerics, hali inayomfanyaawe kocha wa sita kutoka Ulaya kutua nchini kufundisha soka.Mjerumani huyo aliyetua nchini juzi tayari kwa kazi ya kuinoa Toto ataungana na wenzake, Mwingereza Stewart Hall wa Azam, Mdachi Hans Pluijm wa Yanga.Wengine wanaotarajiwa kuonyesha uwezo wao msimu huu ni Mwingereza Dylan Kerr wa Simba, Mfaransa Patrick Liewig wa Stand United ya Shinyanga pamoja na raia wa Finland, Mika Lonnstrom wa Majimaji ya Songea mkoani Ruvuma.Ujio wa makocha wa kigeni pengine utaondoa utawala wa Azam, Simba na Yanga kupokezana ubingwa kutokana na kuwa na makocha wageni.ADVERTISEMENTAkizungumza na gazeti hili, Glerics alisema amekuja nchini kufanya kazi moja ya kuhakikisha timu hiyo inakuwa bora kwenye Ligi Kuu msimu ujao.“Nimekuja Mwanza kwa lengo lakuwapa mafanikio Toto Africans kwenye ligi msimu ujao, nimeiona timu na nitaangalia ni mfumo upi nitautumia kwenye mashindano ambao wachezaji wangu wataweza kuumudu uwanjani,” alisema.Kocha huyo amekuja na msaidiziwake, Lucas Stellmach pia kutoka Ujerumani ambaye atakuwa akifundisha timu ya vijana ya klabu hiyo.Msemaji wa Toto, Cuthbert Japhet pamoja na mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu hiyo, Peter Onyango alisema kocha huyo atapewa mkataba wa mwaka mmoja wa kukinoa kikosi hicho.“Kocha atapewa mkataba wa mwaka mmoja kukinoa kikosi chetu na ataanza mara moja mazoezi na ndiyo maana umemwona amekuja moja kwa moja kuwaona wachezaji hapa uwanjani ni kocha mzuri ambaye tuna imani ataweza kuing’arisha Toto Africans,” alisema Japhet.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni