Kiungo Mbrazili Andrey CoutinhoADVERTISEMENTDar es Salaam. Wakati Yanga ikimpa majaribio kiungo Mcameroon Batetakana Flavius kwa ajili ya usajili msimu ujao, uongozi wa klabu umeamua kusitishwa kwa mikataba ya nyota wao wawili wa kigeni, Joseph Zutah na kiungo Mbrazili Andrey Coutinho.Katika kikao hicho kilichofanyika juzi katika hoteli moja jijini Dar es Salaam, Yanga kupitia uongozi wao uliomshirikisha kocha mkuu, Hans Pluijm ulibariki kuondolewa kwa wachezaji hao wawili ambao viwango vyao vimeshindwa kukidhi mahitaji yao.Wakati Zutah akiondolewa na Coutinho, tayari uongozi huo haraka umetafuta mbadala, ambapo beki raia wa Togo, Vincent Bossou anayechezea timu ya Goyang Hi FC ya Korea Kusini yuko katika hatua za mwisho kutua katika timu hiyo kuimarisha ulinzi.Mghana huyo aliyesajiliwa na Yanga katika kipindi hiki cha usajili ameshindwa kuhimili ushindani wa namba katika kikosi hicho, akizidiwa na beki Juma Abdul huku Coutinho akionekana bado hajafanikiwa kukubalika katika muda wa mwaka mmoja aliodumu katika kikosi hicho baada ya kuletwa naaliyekuwa kocha wa timu hiyo, Marcio Maximo.“Zutah hakuwa mchezaji tuliyekuwa tunategemea kuwa naye wakati tukiambiwa sifa zake tulilazimika kumkubalia kocha, lakini kila kitu kipo wazi kwamba hakuwa na ubora huo kulingana na aina ya wachezaji tulionao sasa tumeamua kumsitishia mkataba pamoja na Coutinho,” alisema kiongozi mmoja anayesimamia usajili.“Uamuzi huo tuliuchukua kwa kuwashirikisha makocha wetu katika kikao kirefu tulichokifanyajana (juzi) na sasa tunahangaikiakuleta wachezaji wapya tukianza na huyo Bossou ambaye tunamleta kuimarisha safu yetu ya ulinzi,” aliongeza.Katika hatua nyingine, klabu hiyo imemweka kwenye mabanokiungo Batetakana baada ya kusema yeye na wengine walio kwenye majaribio kwenye klabu hiyo wanatakiwa kuonyesha viwango vya kuridhisha, vinginevyo itakula kwao.Kocha msaidizi wa Yanga, Boniface Mkwasa alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa wanataka kuona wachezaji wote walioko kwenye majaribio ya kujiunga na klabu hiyo wanaonyesha uwezo na kiwangocha juu ili wapate kulishawishi benchi la ufundi liwape nafasi ndani ya kikosi chao.Mkwasa alisema kuwa falsafa yaYanga ni kumsajili mchezaji atakayetoa mchango kwenye timu hiyo na si vinginevyo hivyo wanahitaji mtu atakayeweza kufanya kazi.“Muda wa usajili umebaki mfupina kama mnavyoona kuwa kuna wachezaji wapo hapa kwa majaribio. Wachezaji hawa badowapo kwenye uangalizi wetu kama benchi la ufundi na iwapo wakituthibitishia uwezo wao tutawasajili ila wakishindwa hatuwezi kuwapa nafasi,” alisema.Mkwasa ambaye anainoa Taifa Stars aliongeza kuwa hilo halitokuwa kwa wachezaji hao, bali hata wale ambao wapo kikosini kuwa wakishindwa kuonyesha uwezo wao wataisikia hewani timu hiyo.“Yaliyopita kwenye Kombe la Kagame yatabaki kuwa historia kwani sasa hivi tunajipanga kwa ajili ya mashindano yaliyopo mbele yetu. Kama kuna mchezaji ataonekana kutomudu kile ambacho tunataka kifanyike basi tutaachana naye hata kama tayari yupo kikosini,” aliongeza.Kiungo Batetakana alisema kuwa ana uhakika kuwa benchi la ufundi la Yanga litaridhika na uwezo na kumpa mkataba wa kuchezea timu hiyo.
other blog
Jumatano, 5 Agosti 2015
USAJILI: Yanga yawakata Zutah, CoutinhoWakati Yanga ikimpa majaribio kiungo Mcameroon Batetakana Flavius kwa ajili ya usajili

Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni