Dar es Salaam.Rais Jakaya Kikwete ametia saini sheria tanozilizopitishwa na Bunge hivi karibuni licha ya kupingwa na wabunge wa upinzani wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).Rais Kikwete alitia saini Sheria ya Mafuta na Gesi; Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini; Mafuta na Gesi Asilia Tanzania; Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafutana Gesi; Sheria ya Tume ya Walimu na Sheria ya Masoko ya Bidhaa zote za mwaka 2015.Akizungumza jana Ikulu kabla yakutiwa saini sheria hizo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema: “Sheria hizi zimejibu kilio cha walimu kutakakuwa na tume yao, zimejibu kiliocha wakulima cha kuwa na masoko huru na ya wazi, pia zitawawezesha Watanzania wengi kushiriki katika uchumi wa gesi na mafuta.”Kabla ya kusainiwa kwa sheria hizo, kila waziri husika alifafanua mambo muhimu yaliyozingatiwa wakati wa uandaaji wa sheria. Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alisema Sheria ya Mafuta na Gesi ya mwaka 2015, imeweka utaratibu ambao Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitashirikiana katika utafutaji, uchimbaji na uendeshaji wa vitalu vya mafuta na gesi.Kuhusu Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi, Simbachawene alisema hivi sasamikataba yote ya madini, mafutana gesi asilia iliyoingiwa baada ya kutungwa kwa Sheria hiyo iliyosainiwa kabla, itawekwa wazi kulingana na vipengele husika vya mikataba.Waziri wa Fedha, Saada Mkuya alisema Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Gesi imeweka utaratibu mzuri wa kukusanya mapato yatokanayo na rasilimalihiyo na pia imetoa mamlaka kwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kusimamia mapato hayo. Waziri wa Elimu na Utamaduni, Dk Shukuru Kawambwa alisema kuwa Sheria ya Tume ya Walimuitawawezesha walimu kuhudumiwa kwa pamoja na kuondoa malalamiko kwa walimu wa shule za msingi na sekondari Bara na Visiwani.Kushiriki mazishi ya KisumoRais Kikwete atahudhuria mazishi ya muasisi wa Tanu na CCM, Mzee Peter Kisumo yaliyopangwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii nyumbani kwake Usangi, Mwanga.Mtoto wa marehemu, Fred Kisumo alisema Serikali imeomba mazishi hayo yafanyike kati ya Ijumaa au Jumamosi ili Rais aweze kushiriki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni