other blog

Jumamosi, 29 Agosti 2015

Kikwete atahadharisha kauli za uvunjifu wa amani Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amesema baadhi ya kauli zinazotolewa


Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya
Kikwete amesema baadhi ya kauli
zinazotolewa na Umoja wa Vyama vya
Upinzani (Ukawa), zinaashiria uvunjifu
wa amani pindi matokeo ya kura
yatakapoanishwa baada ya zoezi la
upigaji kura Oktoba 25 mwaka huu.
Rais Kikwete alisema baadhi ya kauli
hizo zimekuwa zikionyesha wazi
viashiria vya uvunjifu wa amani na
upotoshaji kwa kundi kubwa la vijana
ambao wanapiga kura kwa mara ya
kwanza.
Akizungumza wakati akizindua
Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao
jijini Dar es Salaam Rais Kikwete
alisema;
“Wamediriki kusema wazi bila kificho
kwamba patakuwa hapatoshi, hizi ni
kauli zinazoashiria uvunjifu wa amani.
Tunachokisema CCM ushindi kwetu ni
lazima na tutashinda kwa kishindo na
kwenda nginja nginja mpaka Ikulu.”
Kikwete alisema CCM imejipanga
kuhakikisha inapata ushindi katika
Uchaguzi Mkuu ujao na kuongeza
kuwa ili kufanikisha hilo wamepanga
kikosi kazi ambacho kitatembea
nyumba kwa nyumba, chumba kwa
chumba, mtu kwa mtu ikiwa kwa sasa
tayari wameshaanza kufanya kampeni
zao kupitia mtandao ya simu za
mkononi.
Katika hafla hiyo ya kuzindua kampeni
hiyo inayoratibiwa na msanii wa
filamu na Miss Tanzania mwaka 2006,
Wema Sepetu, Rais Kikwete aliwataka
wanawake kaungalia mazuri yote
yaliyofanywa na Serikali ya CCM katika
kumuinua mwanamke.
-

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni