Mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema
Edward Lowassa akishuka kwenye moja ya
daladala .
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam
limemtahadharisha mgombea wa urais
kwa tiketi ya Chadema Edward
Lowassa kuwa kampeni alizoanza kwa
kuyatembelea makundi kadhaa
zinaweza kutumiwa na maadui wa
kisiasa kumdhuru.
Hata hivyo, wanasiasa wametakiwa
kufuata ratiba ya kampeni kwa
kuzingatia mwongozo wa Tume ya
Uchaguzi (NEC) ili kulisaidia jeshi hilo
kukabiliana na vitendo viovu.
Onyo hilo limetolewa ikiwa ni siku ya
pili tangu Lowassa na mgombea
mwenza Juma Duni Haji walipoanza
kuwatembelea wananchi huku
wakitumia usafiri wa umma.
Kwa kutumia staili hiyo, leo Lowassa
akiwa na Duni Haji wametembelea
maeneo ya Tandika, Tandale na
Kariakoo jijini Dar.
Akizungumza na wanahabari leo jijini
Dar, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum
Dar es Salaam, Suleiman Kova
amesema ziara iliyofanywa leo
maeneo ya Swahili, Kariakoo
zimesababisha mikusanyiko isiyo ya
lazima na kusimamisha shughuli za
maendeleo.
Baada ya CCM kuzindua kampeni zake
mwishoni mwa juma lililopita viwanja
vya Jangwani, jijini Dar es Salaam,
Chadema nacho kinajiandaa kufanya
hivyo Agosti 29 maeneo hayohayo.
-
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni