other blog

Jumatano, 26 Agosti 2015

Kipindupindu chaota mizizi Dar, Morogoro Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa wa kipindupindu uliolikumba jiji la Dar es




TAHADHARI: Wafanyakazi wa afya katika
kambi ya wagonjwa wa kipindupindu
iliyopo katika Zahanati ya Mburahati jijini
Dar es Salaam, wakifanya usafi katika wodi
hiyo juzi. Picha na Venance Nestory
Dar/Moro. Idadi ya watu waliopoteza
maisha kutokana na ugonjwa wa
kipindupindu uliolikumba jiji la Dar es
Salaam imeongezeka na kufikia saba
huku waliolazwa wakifikia 230 na
Mkoa wa Morogoro ukiwa na
wagonjwa 32 na mmoja kupoteza
maisha.
Akizungumza ofisini kwake jana,
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk
Seif Rashid alisema Wilaya ya
Kinondoni inaongoza ikiwa na
wagonjwa186 huku Ilala na Temeke
zikiwa na wagonjwa 22 kila moja.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Morogoro,
Nicolaus Chiduo alisema tangu Agosti
18, watu 42 wameugua ugonjwa huo,
na kutibiwa na sasa wamebaki 18.
Dk Rashid alisema wizara yake
imetengeneza kambi katika manispaa
zote tatu; Kinondoni ipo katika
Zahanati ya Mburahati, Ilala (Kituo
cha Afya Buguruni) na Temeke
(Hospitali ya Temeke).
Alisema kuwa wananchi wanaweza
kuwasiliana na mganga Mkuu wa Mkoa
kwa simu namba 0767300234, endapo
wataona mtu mwenye dalili za
ugonjwa huo ili ushauri utolewe jinsi
ya kumsafirisha.
“Naomba sekta nyingine kama maji,
elimu, mawasiliano, uchukuzi na ujenzi
tushirikiane kutokomeza ugonjwa huu
kwa kuwapatia wananchi elimu ya
ugonjwa huu,” alisema Dk Rashid.
Ofisa Afya Wilaya ya Kinondoni,
Mathias Kapizo alisema tayari
wameanza kuchukua sampuli za maji
kutoka kwenye maeneo yaliyoripotiwa
kutoa wagonjwa wengi ili kubaini
chanzo cha tatizo hilo.
Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya
Temeke, Joyce Msumba alisema wilaya
hiyo ilipokea wagonjwa 25 waliokuwa
na dalili za ugonjwa huo ila sampuli
zilionyesha kuwa 22 hawakuwa na
ugonjwa huo.
Alisema wagonjwa watatu wa familia
moja ambao sampuli zao zilionyesha
kuwa wana vimelea vya ugonjwa huo,
hawakutokea katika wilaya hiyo, bali
Manzese na mmoja alipoteza maisha.
Morogoro
Kuhusu athari za kipindupindu
wilayani Morogoro, imeelezwa kuwa
mgawo wa maji katika maeneo mengi
ndicho chanzo kikuu cha kuongezeka
kwa idadi ya wagonjwa.
Akizungumza kwenye kambi ya
Sabasaba, Dk Chiduo alisema Idara ya
Afya imelazimika kufungia maeneo
yote ya baba na mama lishe hasa yale
yenye mkusanyiko wa watu na kuzuia
uuzaji wa vyakula ndani ya mabasi.
Maeneo yaliyopigwa marufuku
kufanya biashara ya vyakula ni Soko
Kuu la Morogoro, Soko la Mawenzi na
maeneo yote ya stendi ikiwamo ya
Msamvu.
Alitaja maeneo yaliyoathiriwa kuwa ni;
Kilakala, Kihonda, Chamwino, Mkundi,
Boma, Lukobe, Kiwanja cha Ndege,
Sua, Kididimo, Nanenane, Kichangani,
Mafiga, Mwembesongo, Polisi Line,
Mzinga, Mzumbe, Sultani, Mafisa na
Mazimbu. Aliwataka wananchi
kuzingatia usafi katika maeneo yao na
kuacha kukaa na kula katika maeneo
ya mikusanyiko kama misiba.
Akizungumza marufuku ya kuuza
chakula, mama lishe, Amina Salim
alisema kinachowaumiza ni mikopo
waliyochukua katika taasisi za fedha.
Kauli hiyo iliungwa mkono na Samson
Akida aliyesema: “Wengi wetu
tumekopa ili tufanye biashara, sasa
hapa tunajiuliza tutalipa na kurejesha
nini?”
Imeandikwa na Lilian Lucas na
Emma Kalalu.
-

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni