other blog

Alhamisi, 17 Septemba 2015

Jk aagiza haraka nyayo za laitole zifukuliwe


Arusha. Rais Jakaya Kikwete, ameagiza
Idara ya Mambo ya Kale kwa
kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro (NCAA), kuharakisha
kufukua nyayo za kale za Laitole ili
kuvutia watalii na kuongeza pato la
nchi.
Rais Kikwete alitoa agizo hilo juzi,
wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi
wa jengo la kisasa la ghorofa 15
linalomilikiwa na NCAA jijini Arusha.
Alisema anashangazwa na uongozi wa
NCAA na idara hiyo kuchukua muda
mrefu kufukua nyayo hizo za
bianadamu wa kwanza kutembea kwa
miguu, ambazo zipo katika eneo la
Laitole Nyayo.
“Kinachotakiwa pale ni kufukuliwa
nyayo na kujengwa jengo la kisasa la
vioo ambalo, litazuia jua na maji
kuingia.
“Pia litadhibiti mabadiliko ya hali ya
hewa ili kutoharibu nyayo hizo, watalii
wakifika Ngorongoro, wataziona
badala ya kuonyeshwa zilipofukiwa,”
alisema Rais Kikwete.
Akizungumza baada ya kuweka jiwe la
msingi, Rais Kikwete alipongeza
uongozi wa Ngorongoro kuwezesha
mradi huo mkubwa wa kitega uchumi.
Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,
Balozi Mwanaidi Maajar alisema ujenzi
wa jengo la kitega uchumi utagharimu
Sh42.3 bilioni.
Alisema ujenzi huo ulianza Novemba
2013 na utakamilika Novemba 2016 na
hadi sasa ghorofa tatu zimejengwa.
Maajar alisema tayari mkandarasi
amelipwa kiasi cha Sh10.2 bilioni ili
kuendelea na ujenzi huo na kwamba
kila mwezi zinatarajiwa kujengwa
ghorofa mbili. Alisema mkandarasi wa
jengo hilo ni Kampuni ya kimataifa ya
CATIC Engineering Limited na
anaendelea vizuri na ujenzi.IMEEANDALIWA NA DENNIC LYAMUYA MTU WA KIRUA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni