other blog

Ijumaa, 18 Septemba 2015

Majambazi ya kenya yauawa arusha...soma zaidi...




Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha
Liberatus Sabas
Arusha. Majambazi wane, wakiwemo
raia watatu wa Kenya wameuwa na
polisi mkoani Arusha baada ya
kuhusika kufanya matukio mbalimbali
ya ujambazi wa kupora silaha pamoja
na fedha.
Akizungumza na waandishi wa habari
mkoani hapa, Kamanda wa polisi,
Liberatus Sabas amesema kuwa
majambazi waliouwawa watatu ni
raia wa Kenya ambapo bado majina
yao kamili hayajajulikana huku raia
wa Tanzania ametambulika kwa jina la
Sixtus Alfredy.
Kamanda Sabas amesema kuwa ,polisi
walianza kujibu majibizano hayo ndipo
walipofanikiwa kuua majambazi
watatu ambao walikutwa na
vitambulisho vitatu vya Jamhuri ya
Kenya vyenye majina ya Simon Githinji
Kariuki,Bonifas Mwanmgi Mbulu,
Thadeo Kamau Njuguna na
kitambulisho kimoja cha UN-ICTR
chenye jina la Chacha John Marwa.
Vitambulisho vingine walivyokutwa
navyo ni leseni ya udereva iliyotolewa
Kenya yenye jina la Thadeo Kamau
Njuguna , kadi ya Benki ya Equity
Master Card yenye jina la Simon
Githinji pamoja na kadi ya Benki ya
Cooperative yenye jina la Thadeo
Kamau Njuguna , simu tano aina ya
Nokia , Tecno na Sumsung.
Amesema kuwa, majambazi hao
watatu kila mmoja alikutwa na bastola
pamoja na risasi , mabegi matatu
meusi ambapo baada ya kuyafungua
walikuta bunduki aina ya AK 47 mbili,
SMG moja, bastola tatu, magazine nne
za SMSg, risasi 85 za SMG na AK 47 na
risasi nyingine 28 za bastola.
Kamanda Sabas amesema kuwa, tukio
hilo lilitokea jana Septemba 17 mwaka
huu majira ya saa 3:30 usiku katika
maeneo ya Chekereni wilayani
Arumeru ambapo polisi walipata
taarifa za kiintelejensia toka Agosti 19
mwaka huu juu ya kuwepo kwa kundi
la majambazi wanaotoka nchi jirani ya
Kenya na kuja hapa nchini kwa nia ya
kufanya uporaji kwa kushirikiana na
majambazi wenzao wa hapa nchini.
Alisema miili ya marehemu wote
imehifadhiwa katika Hopsitali ya Mkoa
ya Mount Meru huku jeshi la polisi
likiendelea na uchunguzi zaidi wa
kuwatafuta watuhimiwa wengine
waliotoroka katika tukio hilo na
kubaini mtandao wa majamba

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni