other blog

Jumatatu, 14 Septemba 2015

Efm...yazindua rasmi kipindi na shindano la uhondo dar.. na mwanahabari wetu DENNIC LYAMUYA...




Wanahabari wakichukua tukio .
EFM radio kupitia kipindi chake kipya
kiitwacho Uhondo imendaa shindano la
Kanga kwa ajili ya wanawake wote
wasikilizaji wa redio hiyo .
Akizungumza na wanahabari leo kwenye
ofisi za Efm radio zilizopo Kawe , jijini Dar
es Salaam, Mtangazaji na mtayarishaji wa
kipindi hicho , Dina Marios amesema kuwa
lengo la shindano hilo amabalo linaanza
leo na kuishia Oktoba 5 mwaka huu , lina
lengo la kuwahamasisha wanawake
wakione kipindi hicho kuwa kimekuja kwa
ajili yao.
Alisema kuwa kipindi hicho kitaweza
kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na
njia nyingine kumwonesha mwanamke
namna nyingine ya kumkomboa badala ya
kukakaa nyumbnani . Faida nyingine ni
pamoja na wanawake kujifunza ujasiliamali
kupitia biashara ya khanga .
“ Mfumo wa shindano lenyewe utakuwa
kama ifuatavyo yaani wasikilizaji wa Efm
redio ambao ni wanawake wanakaribishwa
kushiriki shindano la kubuni maneno ya
khanga kupitia kipindi cha ‘ Uhondo’ na
maneno hayo yawe na neno ‘ UHONDO ’
kwa kutumia mfano Uhondo wa Ngoma
uingie ucheze ,” alisema Dina nakuongeza:
“ mshindi wetu atajinyakulia kitita cha
shilingi za kitanzania milioni moja,”
alisema.
Vile vile aliongeza kuwa shindano hilo
halitaishia hapo, kwani baada ya kupata
mshindi neno lake la ushindi
zitatengenezwa khanga zitakazoandikwa
neno hilo ikiwa ni hatua ya pili sasa ya
kumwezesha mwanamke kujikwamua
kiuchumi.
Hata hivyo , aliongeza kuwa baada ya
kutengenezwa khanga hizo, Efm kupitia
kipindi hicho , itatoa nafasi kwa wanawake
kutengeneza pesa na kujikwamua kwa
kuuza khanga hizo na mwanamke yeyote
hasa kwa mikoa ya Dar es Salaam na
Pwani atachukua khanga hizo na kuziuza
pasipo kulipia pesa yoyote ambapo kwa
kila doti moja ya khanga atapata asilimia
30 ya pesa .Alisema washiriki watapewa
mafunzo maalum kwa jili ya kuwawezesha
katika uuzaji wao.
( NA DENIS LYAMUYA/EFM)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni