other blog

Ijumaa, 4 Septemba 2015

Nyota watatu kuiua Nigeria watajwa Wakati timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ ikijiandaa kuikabili Nigeria, wachezaji watatu au


Wachezaji hao ni Mbwana Samatta, John
Bocco na Thomas Ulimwengu.
Dar es Salaam. Wakati timu ya Taifa
ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ ikijiandaa
kuikabili Nigeria, wachezaji watatu au
wanne wameonekana ndiyo
watakaoamua mechi hiyo mapema
endapo watacheza katika ubora wao.
Wachezaji hao, Mbwana Samatta, John
Bocco na Thomas Ulimwengu ndiyo
pekee wameshikilia mkononi roho za
Watanzania ili kuhakikisha wanaipa
ushindi wa mapema Stars.
Stars inaikabili Super Eagles ya
Nigeria Jumamosi katika mchezo wa
kuwania tiketi ya kucheza fainali za
Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka
2017. Timu hiyo ilirejea jana saa 9
alfajiri ikitokea Istanbul, Uturuki
ilikoweka kambi ya wiki moja
kujiandaa na mchezo huo dhidi ya
Nigeria utakaochezwa kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchambuzi masuala ya soka, Joseph
Kanakamfumu aliliambia gazeti hili
jana kuwa mchezaji pekee anayeweza
kuamua mchezo huo kwa kuleta
matokeo mazuri ni Samatta.
Kanakamfumu alisema Samatta ndiye
atabeba matumaini ya Watanzania,
lakini kama ataamua kucheza mpira
kwa kiwango ambacho amekuwa
akikionyesha akiwa TP Mazembe.
Kwa upande wake, Ally Mayay
anawataja Samatta, Ulimwengu na
Mrisho Ngassa kama wachezaji
wanaoweza kuibeba Stars.
Alisema tatizo la Stars siyo ulinzi wala
kiungo, isipokuwa washambuliaji
ambao wanakosa umakini wa kutumia
nafasi zinazopatikana. Kulingana na
Nigeria ilivyo na kikosi imara cha
wachezaji wengi wanaocheza soka la
kulipwa nje ya nchi hiyo, Stars haiko
nyuma kwani inao wachezaji
inaowategemea kuleta furaha kwa
mashabiki.
Samatta, Ulimwengu wanaocheza soka
la kulipwa kwenye klabu ya TP
Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo (DRC), tayari wamewasili
nchini na Ngassa anayecheza soka ya
kulipwa Afrika Kusini akisubiriwa.
Enyeama ‘aiogopa’ Stars
Wakati huohuo, nahodha na kipa wa
Nigeria, Vincent Enyeama amejitoa
kwenye kikosi kitakachoivaa Taifa
Stars, Jumamosi.
Mtandao wa Supersport.com
umekariri vyanzo kutoka kambi ya
Super Eagles mjini Abuja ukieleza
kuwa kipa huyo mwenye miaka 33
amejiondoa kwa sababu za kifamilia.
Kujitoa kwa Enyeama kunaifanya
Super Eagles kumuita kipa Carl Ikeme
wa Wolves au Ikechukwu Ezenwa wa
Sunshine Stars.






Ewe mpenzi msomaji usipoteze kura yako mpe lowasa tupaate mabadiliko ya kweli ok,

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni