other blog

Ijumaa, 18 Septemba 2015

JAMAN HAYA MASHAMBA KWANI TUTAKUFA NAYO.. ROMBO HII NI AIBU

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania,
Said Mwema
KATIKA hali isiyo ya kawaida Jeshi la
Polisi wilayani Rombo,limelazimika
kusimamia shughuli ya mazishi
baada ya kundi la watu wanne
kuzuia mwili wa marehemu Gaspar
Evarist (18) aliyefariki kwa ajali ya
pikipiki usizikwe shambani kwake
kijiji cha Muriae, wilayani Rombo.
Mkuu wa Polisi wilayani hapa, Ralph
Meela alisema kuwa vurugu hizo
zilisababishwa na mama wa
marehemu huyo na watoto wake
wakitaka mwili huo usizikwe kwenye
shamba la baba yake mzazi bali
wakauzike sehemu nyingine.
Akifafanua zaidi Meela alisema
chanzo cha mzozo huo ni baba wa
marehemu kufariki miaka mingi
iliyopita na hivyo waliokuwa
wakizuia mwili huo walidhani kuwa
endapo marehemu atazikwa hapo
shamba hilo litakua la kwake na
hivyo watakosa urithi.
Alisema katika vurugu hizo
zilisababisha uharibifu wa mali,
kwani wahusika walivunja msalaba
wa jumuiya pamoja na kumzuia
padre kuendesha ibada ambaye
ndugu walimtishia na hivyo
kuondoka kuepuka vurugu hizo.
Baada ya polisi kufika waliwakamata
watuhumiwa na kisha kusimamia
mazishi hayo.
Wakati huo huo mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la
Lewanga Kimario (23) mkazi wa kijiji
cha Mrere Mashati wilayani Rombo
amefariki dunia baada ya kujinyonga.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Rombo,Ralph
Meela amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo. Meela alisema kuwa tukio
hilo lilitokea Juni 25, mwaka huu
majira ya saa 9:00 alasiri katika Kijiji
cha Mrere Mashati.
Meela alisema kuwa mwili wa
marehemu ulikutwa ukiwa
umening’inia juu ya paa la nyumba
yake.
Aidha alisema kuwa chanzo cha kifo
hicho bado hakijajulikana. Kwa
mujibu wa baba mzazi wa
marehemu, Thomas Kimario alisema
kabla ya tukio marehemu alikua
akisumbuliwa na malaria kali na
hivyo inaweza ikawa ndio sababu ya
kifo chake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni