other blog

Alhamisi, 23 Julai 2015

awasilisha uchunguzi kifo cha bosi UN




JAJI Mkuu wa Mahakama ya
Tanzania, Mohamed Chande
Othman, amekabidhi taarifa ya
uchunguzi wa kifo cha aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa
(UN), Dag Hammarskjöld kwa
Katibu Mkuu wa umoja wa huo
wa sasa, Ban Ki-moon.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
na Ofisi ya Mawasiliano ya
Mahakama Kuu, Jaji Chande
alikuwa Mwenyekiti wa jopo huru
la wataalamu lililoundwa na Ki-
Moon kutafuta ukweli juu ya kifo
hicho.
Hammarskjöld alifariki dunia kwa
ajali ya ndege Septemba 18,
mwaka 1961 maeneo ya Ndila,
Zambia, wakati akitafuta suluhu
ya mgogoro wa vita nchini Congo
(DRC). Pamoja na Jaji Chande,
jopo hilo lilikuwa na wajumbe
wengine wawili; Kerryn Macaulay
wa Australia na Henrik Larsen wa
Dermark.
“Kazi hiyo iliyochukua miezi
mitatu imekamilika na
kuwasilishwa kwa Ki-moon
ambaye pia ameiwasilisha kwa
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa,” ilisema taarifa hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni