Wakenya kwenye mtandao wa twitter
wameizomea shirika la habari la
Marekani CNN kwa kuipaka tope
''Kenya'' siku moja tu kabla ya ziara
ya rais wa nchi hiyo Barack Obama.
Wakitumia kibwagizo #SomeoneTellCNN
waliizomea shirika hilo kwa kupeperusha
ripoti chini ya kichwa
''Hofu ya usalama huku Obama akizuru
kitovu cha ugaidi''.
Wakenya kwenye mitandao ya kijamii
waliizomea CNN kwa kuashiria kuwa
Kenya imeshindwa kukabiliana na kundi
la kigaidi la Al Shabaab.
Katika ripoti hiyo Mchanganuzi wa
maswala ya kiusalama anasema kuwa
jeshi la
''Marekani imeimarisha mashambulizi
dhidi ya kundi la Al Shabaab katika siku za
hivi punde,ilikutoa ujumbe kwa uongozi
wa kundi hilo la kiislamu lisijaribu kwa
njia yeyote kutibua ziara ya rais Obama''
Kisha wanaonesha picha za shambulizi la
kigaidi katika maduka ya Westgate.
Hii si mara ya kwanza kwa ripoti za
shirika hilo kuwaudhi wakenya.
Mwaka uliopita wakenya waliishambulia
shirika hilo kwa kuchapisha ripoti
iliyoonesha kuwa kuna hatari kubwa
mapigano ya kikabila kabla ya uchaguzi
wa mwaka wa 2014 nchini humo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni