Data zinasubiriwa kwa hamu kuhusu
dawa inayotumainiwa kuponya
ugonjwa wa udhoofu wa ubongo
(Alzheimer) baadae leo .
Watafiti watatangaza matokeo ya
uchunguzi kuhusu matumizi ya dawa aina
ya solanezumab, ambayo wagonjwa na
wanasayansi wanatuami inaweza kuwa
tiba ya kwanza ya kupunguza kasi ya
kupungua kwa kazi ya ubongo
Dawa iliyopo kwa sasa inasaidi kupunguza
dalili , lakini haisitishi kufa kwa seli za
ubongo.
Dr Eric Karran, kutokakituo cha utafiti wa
maradhi hayo nchini Uingereza , anasema
dawa hiyo inaweza kuhakikishwa kuwa na
"uwezo mkubwa".
Maelezo ya uchunguzi kuhusu dawa ya
solanezumab yatatolewa katika mkutano
miji Washington.
Dawa hiyo imekua matumaini makubwa
ya malengo ya utafiti unaolenga seli za
protini ziitwazo amyloid ambazo humea
kwenye ubongo mtu anapokuwa na
maradhi ya Alzheimer .
Inadhaniwa kuwa kuundwa kwa lundo la
amyloid baina ya neva za seli
kunasababisha kuharibik na baadae kufa
kwa seli za ubongo.
Majaribio ya sawa ya maradhi hayo
yanayowakumba mamilioni ya watu
duniani yaligonga mwamba mwaka 2012.
Hata hivyo, wakati kampuni ya Marekani
ya Eli Lilly ilipoangalia kwa makini data,
ilibainika kuwa kuna ishara inaweza
kufanya kazi kwa wagonjwa wanaoanza
kupata ugonjwa huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni