ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu(BOT) Amatus Liyumba (62) amehukumiwa kwenda jela miaka miwili baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma.Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Lameck Mlacha wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akiwa mmoja wa jopo la mahakimu watatu waliokuwa wakiongozwa na Hakimu Mkazi Edson Mkasimongwa.Hukumu ya kesi hiyo ilianza kuunguruma saa 3:00, asubuhi huku chumba cha mahakama kikiwa kimejaa pomoni, watu mbalimbali wakiwemo ndugu, jamaa, marafiki na wafuatiliaji wengine wa kesi kila mmoja alikuwa na uso za hisia tofauti, ambao baada ya hukumu hiyo baadhi yao walionekana kububujikwa na machozi.Mshtakiwa Liyumba alisomewa hukumu mbili tofauti, ambapo hukumu iliyotumika kumfunga Bw. Liyumba ilionekana kukubalika na mahakimu wawili kwa kufanana, huku Bw. Mkasimongwa akitoa maoni yaliyotofautiana na wenzakekwa kuona kuwa Bw. Liyumba hanahatia.Akisoma hukumu ya kwanza Hakimu Lameck Mlacha alisema mashahidi watano upande wa mashtaka kati ya mashahidi wanane walisisitiza kuwa gharama katika Mradi wa Ten Milambo ulisababishwa na matumizi mabaya ya madaraka.Mashahidi hao walisema kuwa mshtakiwa alikuwa akisaini na kutoa maelekezo katika mradi huo uliokuwa chini ya uongozi wa idaraaliyokuwa akiiongoza mshitakiwa.Hakimu Mlacha alisema kuwa mahakama imebaini kuwa mshtakiwa alikuwa akitoa maelekezo kinyume na utaratibu wa BOT kiasi cha kuwa na nguvu yakubadili uhalisia wa sura ya mradi,badala ya kazi hiyo kufanywa bodi ya BoT kisheria.Hata hivyo wakili aliyekuwa akimtetea mshtakiwa Bw. Majura Magafu aliiomba mahakama hiyo kuwa na huruma licha ya mteja wake kuonekana kuwa na hatia, kwa kuwa ameitumikia BoT kwa uadilifu kwa miaka 35. Pia aliiombamahakama kuangalia umri wake akiwa kama mstaafu huku akitegemewa na familia yake.Akitoa maombi hayo Bw. Magafu aliiomba mahakama impunguzie mteja wake adhabu, kwa kumwamuru kulipa faini badala ya kifungo.Kesi hiyo ambayo tangu mwanzo ilikuwa na mvuto wa namna yake ilikuwa chini ya jopo la mahakimu Edson Mkasimongo, Benedick Mwingwa na Lameck Mlacha ambapo upande wa mshtakiwa ulikuwa ukiongozwa na wakili Hilaly Mkate.Katika kesi hiyo mashahidi 10 walijitokeza kutoa utetezi upande wa Serikali, wakiwemo wale wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), huku shahidiwa tano akiwa ni mmmoja wa washtakiwa katika kesi ya wizi wa mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), Bw. Bosco Kimela.Awali Mwendesha Mashtaka Wakiliwa Serikali, Bw. Prosper Mwangamila alidai mbele ya mahakama kuwa Bw. Liyumba, katiya mwaka 2001 na 2006 akiwa ameajiriwa na BoT, alitumia vibayaofisi yake kwa kuchukua uamuzi katika ujenzi wa majengo pacha ya benki hiyo.Kabla ya kubaki na kosa moja alilohukumiwa nalo jana, Bw. Liyumba alikuwa akikabiliwa na makosa mawili, ambapo kosa la pili lilikuwa ni kuisababishia serikali hasara sh. bilioni 221 katika ujenzi wa Minara Pacha ya BoT. Upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha kosa hilo, hivyo likafutwa.Hata hivyo Wakili wa Bw. Liyumba, Bw. Magafu alisema anatarajia kukata rufaa mara baada ya kupatanakala kwa kuwa kuna makosa madogo madogo yaliyojitokeza katika hukumu hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni