other blog

Jumamosi, 5 Novemba 2016

Joyce ndelchako afumuka makubwa kuhusu bodi ya mkopo na aamuru kuwa wote walioomba mkopo wapatiwe. shuka nayo hii..

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya
Juu (HELSB), imeagizwa
kuhakikisha kuwa fedha zote
zilizotengwa kwa ajili ya
mikopo ya wanafunzi
wanaoendelea na masomo
zinapelekwa vyuoni ifikapo
leo.
Agizo hilo lilitolewa bungeni
jana na Waziri wa Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Ufundi,
Profesa Joyce Ndalichako
baada ya wabunge mbalimbali
kuomba miongozo kwa Spika
kuhusu kuwapo kwa wanafunzi
wengi waliokosa mikopo kwa
mwaka wa fedha 2016/17.
Mwongozo kwa Spika ulitiliwa
mkazo na Mbunge wa Chalinze
(CCM), Ridhiwan Kikwete
aliyeeleza kuwapo taarifa
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM) kuwa
wanafunzi wanataka kugoma
kwa kukosa fedha za mikopo.
Kutokana na miongozo hiyo,
Mwenyekiti wa Bunge, Najma
Giga aliitaka Serikali kutoa
maelezo.
Akitoa kauli ya Serikali, Profesa
Ndalichako alisema fedha za
mikopo kwa ajili ya wanafunzi
zilikwenda vyuoni wiki moja
iliyopita.
“Tatizo lililotokea kwa UDSM
sijui kama walidanganyana au
la lakini hawakujaza fomu.
Serikali haitatoa mkopo kwa
mwanafunzi ambaye hajajaza
fomu. Na waliosaini leo
wataingiziwa fedha zao kwenye
akaunti na vyuo,” alisema.
Kuhusu wanaoendelea na
masomo, Profesa Ndalichako
alisema wanafunzi wote
wanufaika na wanaoendelea na
masomo wataendelea kupatiwa
mikopo kama ilivyokuwa
mwaka uliopita.
Alisema wanafunzi ambao
vyuo vyao vimewasilisha HELSB
taarifa za matokeo, Bodi
imekwishawatumia fedha
vyuoni kwa ajili ya kuwapa
mikopo wanafunzi hao.
Hata hivyo, alisema taratibu za
kuwabaini wanafunzi wenye
sifa zinaendelea na wasio na
sifa wataendelea kuondolewa
kupata mikopo.
Pia, alikiri kuwa ucheleweshaji
wa matokeo ya wanafunzi
wanaoendelea na masomo
umeathiri kasi ya kutuma fedha
vyuoni.
“Wizara yangu imekwishaagiza
vyuo vyote ambavyo
havijawasilisha matokeo ya
mitihani ya wanafunzi wao kwa
mwaka wa masomo uliopita,
kufanya hivyo mara
moja,” alisema.
Ndalichako alisema hadi
kufikia Novemba 3 mwaka huu,
Sh71.042 bilioni
zilikwishatumwa vyuoni kwa
ajili ya wanafunzi wa mwaka
wa kwanza na wanaoendelea
na masomo.
Akizungumzia utoaji wa
mikopo kwa mwaka wa fedha
2016/17, Ndalichako alisema
katika mwaka huo, Sh483
bilioni zimetengwa na
zimelenga kutoa mikopo kwa
wanafunzi 119,012, wanafunzi
93,295 wanaoendelea na
masomo na wa mwaka wa
kwanza 25,717.
Ndalichako alisema katika
mwaka wa fedha 2016/17
wanafunzi 58,010 walidahiliwa
na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU)
na orodha yao iliwasilishwa
HELSB na hadi Novemba 2,
mwaka huu, wanafunzi 21,190
wa mwaka wa kwanza
wamepewa fedha. Kati yao
4,321 ni yatima, 118 wenye
ulemavu na 87 ni waliosoma
sekondari kwa ufadhili wa
taasisi mbalimbali.