other blog

Jumatatu, 26 Desemba 2016

MDADA AFARIKI GAFLA KANISANI ROMBO AKIWA ANAPAMBA KANISANI..

kwenye picha ni mdada aliyefariki gafla baada ya kuanguka juu ya jukwaaa kanisani mdada

aliyetambulikana kwa jina la CATHERIN ELIGI MANG'ORO alianguka kwenye aliteleza na kuanguka kwenye jukwaaa wakati akiwa anapamba jukwaa kwa ajili ya misa takatifu ya christmass.. dada huyo alipata ajali hiyo katika kigango cha kwamaksau kilichopo PAROKIA YA KENI ....ROMBO MKOANI KILLIMANJARO..

wadau walisaidiana ili kukimbiza hospitalini lakini huhudi zao pamoja na daktari hazikuzaa matunda.. DADA CATHERIN ametuachia pengo kubwa alikuwa mhitimu wa chuo kikuu msubiri ajira pasipo hata kufarahia matunda ya elimu yake mungu kamuita kwenda kumuandalia makao huko mbinguni.. tunaamini dada yetu aliaga akiwa anafanya  kazi ya kanisa basi na mbinguni ataendelea na kazi hiyohiyo ya kumsifu mungu..

tuliobaki mim na ww tumkumbuke mungu kila wakati kwani hatujui saa wa siku atakayojuja mwana wa mungu tumsifu mungu daima hekaluni

DADA YETU CATHERIN TULIKUPENDA ILA MUNGU KAKUPENDA ZAIDI ..MUNGU AKUREHEMU UPUMZIKE KWA AMANI.         AMINA

Alhamisi, 22 Desemba 2016

Ndalichako asitisha ajira za waalimu wa sanaa yaani arts kwa ngazi ya sekondari kama ulikuwa unasubiria ajira mkuu anza kufanya vitu vingine.

WAZIRI wa Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi,
Profesa Joyce Ndalichako,
ametoa masharti mapya ya
ajira za ualimu nchini, huku
akisema Serikali haitaajiri
walimu wa masomo ya sanaa
(arts) kwa kuwa wapo wa
kutosha.

Akizungumza mjini Dodoma
jana wakati akifungua
mkutano mkuu wa mwaka wa
Wakuu wa Shule za Sekondari
Tanzania (TAHOSSA), Profesa
Ndalichako, alisema Serikali
kwa sasa haiwezi kuajiri
walimu wa masomo hayo
kwa kuwa inataka kuajiri
walimu wa masomo ya
sayansi na hisabati ambao
idadi yao ni ndogo.
“Pamoja na uamuzi huo mpya,
ajira za walimu wapya wa
masomo ya sayansi nazo
zimebadilika kwani wale wote
waliohitimu ualimu wa sayansi
na hisabati, wanatakiwa
watume vyeti vyao kabla ya
kupangiwa kituo cha kazi.
Kuhusu wale walimu wa
‘arts’, kule tuna walimu wa
ziada ambao tutajaribu
kuwapanga kutokana na shule,
kwani wengi walikuwa
wamepangwa shule moja.
Kwahiyo, tutaangalia utaratibu
wa kuwapanga kulingana na
mahitaji,’’ alisema Profesa
Ndalichako.
Akizungumzia suala la ubora
wa elimu nchini, Profesa
Ndalichako aliwataka walimu
wakuu hao kuhakikisha
wanasimamia ubora wa
elimu kwa kuwa wao ndio
wanaowaandaa wanafunzi
kabla hawajaenda vyuoni.
“Vilevile pelekeni takwimu
sahihi za wanafunzi waliopo
katika shule zenu kuisaidia
Serikali katika kupanga bajeti ili
iweze kutoa fedha sahihi.
“Hapa kuna kimbembe, yaani
wakati mwingine huwa
najifanya nimepoteza takwimu
ya shule fulani, nikiziomba na
kutumiwa, zinakuwa ni tofauti
na zile za mwanzo.
“Hili nawaomba mkalisimamie
ili iwe rahisi kwetu kupanga
bajeti yenye tija,’’ alisema.
Kuhusu ujenzi wa maabara
katika shule za sekondari,
waziri huyo alisema kwamba
kutokana na nyingi
kukamilika, Serikali itatoa
vifaa vya maabara kuanzia
Januari mwakani baada ya
kuwa vimeingia nchini
kutoka vilikoagizwa.
Awali, akisoma risala ya
walimu hao, Rais wa
TAHOSSA, Bonus Nyimbo,
aliiomba Serikali itoe waraka
wa kupiga marufuku
matumizi ya simu kwa
wanafunzi shuleni kwa kuwa
zimekuwa zikichangia
kushuka kwa ufaulu kwa
baadhi ya wanafunzi.
“Ili kuboresha elimu,
tunaiomba Serikali itoe waraka
wa kupiga marufuku matumizi
ya simu kwa wanafunzi kwani
simu nyingi tunazozikamata
tunakuta mule hakuna
taaluma,’’ alisema Nyimbo.
Kwa upande wake,
Mkurugenzi wa Global
Education Link, Abdulmalik
Molel, ambaye pia kampuni
yake ilipewa tuzo ya heshima
katika kuendeleza elimu
nchini, alisema ni jukumu la
kila mmoja kutimiza wajibu
wake ili kuiendeleza elimu ya
Tanzania.
“Kila mmoja anapaswa
kutimiza wajibu, wazazi,
walezi na walimu, waambieni
wanafunzi wasiwe na
‘expectation’ (matarajio)
makubwa kwani wanapokuwa
na matarajio hayo, wakienda
vyuo vikuu wanakuwa
wasumbufu,” alisema.
Wakati hayo yakiendelea, juzi
taarifa ilitolewa jijini Dar es
Salaam na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi,
Maimuna Tarishi, ikisema
kwamba, walimu wahitimu
wa masomo ya sayansi na
hisabati waliohitimu shahada
na astashahada mwaka 2015,
wanatakiwa kuwasilisha
nakala za vyeti vya elimu ya
sekondari vya kidato cha nne
na sita na taaluma ya ualimu
kwa uhakiki.
Pamoja na hayo, hivi
karibuni Serikali ilitangaza
kusitisha ajira zote nchini ili
kukabiliana na wimbi la
watumishi hewa.
Sambamba na uamuzi huo,
nyongeza za mishahara kwa
watumishi wa Serikali nazo
zilisimamishwa ili
kukabiliana na watumishi
hao hewa ambao walikuwa

Imeandaliwa na ben mrosso kutoka dodoma

Jumatatu, 19 Desemba 2016

Chuo cha serikali za mitaa kimetoa harufu ya ufisadi wa ngono....Waziri ataka Bodi Chuo cha Serikali za Mitaa kushughulikia malalamiko

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), Mhe.George Simbachawene, ameiagiza bodi ya chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo mkoani Dodoma (LGTI), kuyafanyia kazi malalamiko ya vitendo vya rushwa ya ngono katika idara ya taaluma na mitihani. Mhe.Simbachawene ametoa agizo hilo tarehe 25 Novemba, 2016, wakati alipokuwa akizungumza na wanafunzi pamoja na uongozi wa chuo hicho wakati wa mahafali ya nane ya chuo hicho. Amesema katika moja ya maeneo ambayo hajaridhishwa nayo, idara ya mitihani ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wanafunzi juu ya urasimu uliopo hasa wakati wa wanafunzi wanapo hitaji matokeo yao. Aidha, Waziri Simbachawene amesema malalamiko mengi yamekuwa katika idara hiyo kwa kipindi kirefu lakini uongozo wa chuo hicho umeendelea kulikalia kimya bila kuchukua hatua. "Naiagiza bodi ya chuo kuhakikisha kuwa idara hii inachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kuifumua na kuiunda upya kwani malalamiko haya yamekuwa ya muda mrefu watu wanaohusika na idara hii wamekuwa na ukilitimba wa hali ya juu mwanafunzi anapotaka kupata matokeo ya mitihani yake ni atazungushwa kama nini," amesema Mhe.Simbachawene. Amesema hali hiyo imekuwa ikiashiria uwepo wa vitendo vya rushwa mbaya ya ngono kati ya wahusika wa idara ya mitihani na wanafunzi wa kike lakini pia wanafunzi wa kiume kudaiwa fedha. "Naomba mlifanyie kazi suala hili haraka sana kwani haya malalamiko mimi ninayo kwa mda mrefu lakini na shangaa uongozi mmekaa kimya hali ambayo imefikia hatua hata kama mwanafunzi kalipia ada ya hosteli lakini bado atazungushwa hadi muhusika mwentee apende utazani anaomba bure,"amesema. Aidha aliongeza kuwa kitu kingine ambacho anautaka uongozi wa chuo hicho kukifanyia kazi ni namna ya matumizi ya fedha za chuo kwani kumekuwepo na upotevu wa fedha lakini hakuna hatua zilizochukuliwa kwa waliohusika. "Fedha za chuo zimeibiwa na wahusika wapo hadi hii leo lakini hakuna kilichuuliwa naomba wahusika wasimamishwe haraka ili uchuguzi ufanyike na hatua zingine kuchukuliwa kwa wahusika," alisema. Hata hivyo amesema kuwa kuna kila sababu ya serikali kutengeneza utaratibu ambao utakuwa unatumika katika kuwaajili wanafunzi wanaomaliza katika chuo hicho ambao wanataaluma ya utumishi katika mamlaka za serikali a mitaa. "Serikali inatumia takribani bilioni 8.3 kwajili ya kuendesa chuo hichi kilamwaka lakini wanafunzi wanapotoka hapa wanakosa kazi hali ambayo si sahihi kutokana na uwezkezaji huo unaofanywa na serikali kwa mwaka kwani hata ujenzi wa chuo hiki umeghalimu sh. bilioni 36.5 hivyo ni lazimu wahitimu hawa tuwatumie ipasavyo,"alisema Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya chuo hicho Prof. Suleiman Ngware alisema kuwa maagizo yote yaliyotolewa na Waziri atayafanyika kazi haraka iwezekanvyo na wahusika wote watachukuliwa hatua. "Mheshimiwa Waziri yote uliyoagiza tutayafanyia kazi na hatua kali zitachuliwa kwa wahusika wote bila ya kumuonea mtu," amesema Prof. Ngware.

Ijumaa, 16 Desemba 2016

Serekali inajua alipo ben saanane.. Lisu aomba watumie vyombo vyao vya ulinzi kumsaka.. CCM ni lini mtatupa uhuru.. We want lema alive.. And max wa jf akiwa huru....tumechoka

Mwanasheria Mkuu wa Chadema,
Tundu Lissu, akizungumza na
waandishi wa habari, Dar es Salaam
jana kuhusu kupotea kwa msaidizi
wa mwenyekiti wa chama hicho, Ben
Saanane. Kulia ni Ofi sa Habari,
Tumaini Makene na Katibu Mkuu
wa Baraza la Vijana (Bavicha), Julius
Mwita.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeitaka Serikali kutumia vyombo vyake vya ulinzi na usalama kumtafuta msaidizi wa mwenyekiti wa chama hicho, Bernard Saanane , ambaye ametoweka katika mazingira ya kutatanisha zaidi ya mwezi mmoja sasa. Chadema imesema Serikali ndiyo yenye uwezo pekee wa kiufundi kujua na kuamuru mashirika ya simu kueleza mawasiliano yake ya mwisho yalivyokuwa. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema katika siku za karibuni, Saanane amekuwa akiongoza kampeni kwenye mitandao ya kijamii, kuhusu kuhakikiwa kwa shahada za uzamivu (PhD) kwa baadhi ya viongozi. Mwanasheria huyo wa Chadema, alisema wakati fulani Saanane alitumiwa ujumbe wa maneno kupitia simu yake ya kiganjani akitishiwa kuacha kuikosoa Serikali. “Nanukuu maneno aliyotumiwa: “Ben Saanane unachokitafuta ndani ya Serikali hii utakipata, kwa elimu na uwezo wako hatukutarajia ungefikia hatua ya ajabu kwa namna ulivyofikia, hujiulizi kwanini upo huru hadi muda huu. “You are too young to die. Tunajua utaandika na hili, andika lakini the next post hutaandika ukiwa na uhuru wa kutosha, andika but your days are numbered. “Unajua kuna rafiki yako alipuuza na hutaki kuandika kuhusu yeye, labda kwa kuwa alitangulia, andika Ben, andika sana, ongea, sema lakini utajikuta mwenyewe na chatu,” alinukuu Lissu. Alisema: “Katika miezi ya hivi karibuni watu ambao wamekuwa wakiikosoa Serikali kupitia mitandao ya kijamii wamekuwa wakikamatwa na watwambie kama wanamshikilia Ben Saanane ili tujue. “Serikali ndiyo yenye udhibiti wa mipaka yetu kuanzia baharini, nchi kavu, mipaka yetu ya anga na hata katika bandari, hivyo ituambie,” alisema Lissu. Aidha mbunge huyo wa Singida Mashariki alisema yeyote anayefahamu taarifa za Saanane azitoe hadharani katika vyombo vya habari, polisi na hata katika vyombo vingine vya Serikali. Aidha Lissu alisema taarifa za kupotea kwa Saanane wamezifikisha ngazi za kimataifa na wataendelea kuzisambaza ili dunia nzima ijue. Akizungumzia kuhusu taarifa ambayo imesambaa katika mitandao ya kijamii kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe anajua aliko Saanane, alisema: “Mara ya mwisho Ben amewasiliana na mwenyekiti Novemba 14 mwaka huu akiwa Dodoma na huwa hawaongozani, bali Ben anafanyia kazi zake makao makuu ya chama.”

Jumatatu, 12 Desemba 2016

Nafazi za kazi serikalin wizara ya afya. Jinsia wazee walemavu na watoto.. Omba mapema...

NAFASI YA KAZI WIZARA YA
AFYA, MAENDELEO YA JAMII,
JINSIA , WAZEE NA WATOTO
Wizara YA Afya , Maendeleo
ya Jamii, JiNSIA , Wazee , na
Watoto imepeta kibali cha
mpango wa ajira ya dharula
kwa wataalamu wa fani za
tabibu na wauguzi mpango
huu utaendeshwa chini ya
mradi kwa ufadhili wa fedha
mfuko wa cdc, award no.
5U2GGHOO1062-03
kwa muda wa miaka miwili
mradi utaajiri watumishi
m192 ambao watafanya kazi
katika wilaya mbalimbali
zenye uhaba wa watumishi
wa kutoa huduma za afya
hasa kwa waathirika wa
wenye virus ivy UKIMWI .
watumishi hawa watalipwa
mshahara na stahiki nyingine
kwa kufuata tarabitu na
kanuni za serikali. Watumishi
wanao takiwa ni
- TABIBU
WASAIDIZI
(NAFASI 95)
wenye ngazi ya
astashahada
(CERTIFICATE IN
CLINICAL
MEDICAL)
- WAUGUZI
(nafasi 97 )
wenye ngazi ya
astashahada
(CERTIFICATE IN
NURSING AND
MIDIWIFERY)
Wizara inakaribisha maombi
ya kazi kutoka kwa
watanzania wenye sifa
zilizotajwa hapo juu , wawe n
vitu vifuatavyo
- Cheti cha
kumaliza  kidato
cha nne
- Cheti cha
taaluma
aliyosomea
kutoka kwenye
chuo
kinachotambulika
na serikali
barua ya
maombi
ionyeshe wilaya
unayotaka
kupangiwa
- Maombi
yatumwe kwa
KATIBU MKUU,
WIZARA YA AFYA,
MAENDELEO YA JAMII,
JINSIA, NA WATOTO,
6 SAMORAL MACHEL
AVENUE,
S.L.P 9083
11478, DAR ES SALAAM,
TANZANIA.
ORODHA YA HALMASHAURI
ZA WILAYA NA IDADI YA
WATUMISHI
WALIOPENDEKEZWA
ARUSHA
NA MKOA HALMASHAURI TABIBU WAUGUZI JUMLA
1 arusha Arusha CC 3 3 6
2 dar es salaam Ilala MC 3 3 6
Temeke MC 3 3 6
Kinondoni MC 3 3 6
3 dodoma dodoma MC 2 3 5
4 geita Geita DC 2 2 4
5 iringa mufindi DC 3 3 6
Iringa MC 2 2 4
6 kagera bukoba DC 3 3 6
Muleba DC 2 2 4
7 kigoma Kigma Ujiji MC 2 3 5
8. Kilimanjaro Moshi Dc 3 3 6
9i Lindi Lindi DC 2 2 4
10 Mara Musoms DC 2 2 4
Rorya DC 2 2 4
11 Mbeya Chunya DC 2 2 4
Kyela Dc 3 3 6
Mbarali DC 2 2 4
Mbeya DC 3 3 6
Mbozi DC 2 2 4
Rungwe DC 2 2 4
12 Morogoro Morogoro DC 3 3 6
13 Mwanza Nyamagana DC 3 3 6
Sengerema DC 2 2 4
14 Njombe Njombe DC 2 2 4
Wang’ing’ombe DC 2 2 4
15 Rukwa Sumbawanga DC 2 2 4
Sumbawanga MC 2 2 4
16 Ruvuma Mbinga DC 2 2 4
Songea MC 2 2 4
17 Shinyanga Kahama DC 3 3 6
Shinyanga MC 2 2 4
18 Tabora Igunga DC 2 2 4
Ndega DC 2 2 4
Tabora MC 3 3 6
19 Tanga