other blog

Alhamisi, 22 Desemba 2016

Ndalichako asitisha ajira za waalimu wa sanaa yaani arts kwa ngazi ya sekondari kama ulikuwa unasubiria ajira mkuu anza kufanya vitu vingine.

WAZIRI wa Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi,
Profesa Joyce Ndalichako,
ametoa masharti mapya ya
ajira za ualimu nchini, huku
akisema Serikali haitaajiri
walimu wa masomo ya sanaa
(arts) kwa kuwa wapo wa
kutosha.

Akizungumza mjini Dodoma
jana wakati akifungua
mkutano mkuu wa mwaka wa
Wakuu wa Shule za Sekondari
Tanzania (TAHOSSA), Profesa
Ndalichako, alisema Serikali
kwa sasa haiwezi kuajiri
walimu wa masomo hayo
kwa kuwa inataka kuajiri
walimu wa masomo ya
sayansi na hisabati ambao
idadi yao ni ndogo.
“Pamoja na uamuzi huo mpya,
ajira za walimu wapya wa
masomo ya sayansi nazo
zimebadilika kwani wale wote
waliohitimu ualimu wa sayansi
na hisabati, wanatakiwa
watume vyeti vyao kabla ya
kupangiwa kituo cha kazi.
Kuhusu wale walimu wa
‘arts’, kule tuna walimu wa
ziada ambao tutajaribu
kuwapanga kutokana na shule,
kwani wengi walikuwa
wamepangwa shule moja.
Kwahiyo, tutaangalia utaratibu
wa kuwapanga kulingana na
mahitaji,’’ alisema Profesa
Ndalichako.
Akizungumzia suala la ubora
wa elimu nchini, Profesa
Ndalichako aliwataka walimu
wakuu hao kuhakikisha
wanasimamia ubora wa
elimu kwa kuwa wao ndio
wanaowaandaa wanafunzi
kabla hawajaenda vyuoni.
“Vilevile pelekeni takwimu
sahihi za wanafunzi waliopo
katika shule zenu kuisaidia
Serikali katika kupanga bajeti ili
iweze kutoa fedha sahihi.
“Hapa kuna kimbembe, yaani
wakati mwingine huwa
najifanya nimepoteza takwimu
ya shule fulani, nikiziomba na
kutumiwa, zinakuwa ni tofauti
na zile za mwanzo.
“Hili nawaomba mkalisimamie
ili iwe rahisi kwetu kupanga
bajeti yenye tija,’’ alisema.
Kuhusu ujenzi wa maabara
katika shule za sekondari,
waziri huyo alisema kwamba
kutokana na nyingi
kukamilika, Serikali itatoa
vifaa vya maabara kuanzia
Januari mwakani baada ya
kuwa vimeingia nchini
kutoka vilikoagizwa.
Awali, akisoma risala ya
walimu hao, Rais wa
TAHOSSA, Bonus Nyimbo,
aliiomba Serikali itoe waraka
wa kupiga marufuku
matumizi ya simu kwa
wanafunzi shuleni kwa kuwa
zimekuwa zikichangia
kushuka kwa ufaulu kwa
baadhi ya wanafunzi.
“Ili kuboresha elimu,
tunaiomba Serikali itoe waraka
wa kupiga marufuku matumizi
ya simu kwa wanafunzi kwani
simu nyingi tunazozikamata
tunakuta mule hakuna
taaluma,’’ alisema Nyimbo.
Kwa upande wake,
Mkurugenzi wa Global
Education Link, Abdulmalik
Molel, ambaye pia kampuni
yake ilipewa tuzo ya heshima
katika kuendeleza elimu
nchini, alisema ni jukumu la
kila mmoja kutimiza wajibu
wake ili kuiendeleza elimu ya
Tanzania.
“Kila mmoja anapaswa
kutimiza wajibu, wazazi,
walezi na walimu, waambieni
wanafunzi wasiwe na
‘expectation’ (matarajio)
makubwa kwani wanapokuwa
na matarajio hayo, wakienda
vyuo vikuu wanakuwa
wasumbufu,” alisema.
Wakati hayo yakiendelea, juzi
taarifa ilitolewa jijini Dar es
Salaam na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi,
Maimuna Tarishi, ikisema
kwamba, walimu wahitimu
wa masomo ya sayansi na
hisabati waliohitimu shahada
na astashahada mwaka 2015,
wanatakiwa kuwasilisha
nakala za vyeti vya elimu ya
sekondari vya kidato cha nne
na sita na taaluma ya ualimu
kwa uhakiki.
Pamoja na hayo, hivi
karibuni Serikali ilitangaza
kusitisha ajira zote nchini ili
kukabiliana na wimbi la
watumishi hewa.
Sambamba na uamuzi huo,
nyongeza za mishahara kwa
watumishi wa Serikali nazo
zilisimamishwa ili
kukabiliana na watumishi
hao hewa ambao walikuwa

Imeandaliwa na ben mrosso kutoka dodoma

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni