other blog

Jumapili, 4 Septemba 2016

mh.... hi ni hatari. CCM watashia kuanzisha ukuta .. Nimeamin kwamba wapinzani ndo mafisadi wakubwa... Hongera magufuli.

WABUNGE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameingia katika mzozo mkubwa na Rais John Magufuli, na sasa wameanza Job Ndugai, kumlazimisha Spika wa Bunge, awanusuru, MwanaHALISI linaweza kueleza.
Habari kutoka Ikulu, Ofisi ya Spika na Kamati ya Wabunge wa CCM, zinasema wabunge hao wamejiapiza kuwa Ndugai na Rais Magufuli wamekalia moto.
Sababu kuu inayotajwa ni hatua ya serikali, kwa amri ya Rais Magufuli, kuhoji na kufikisha mahakamani baadhi ya wabunge wa CCM wanaotuhumiwa kuomba rushwa kutoka kwa taasisi wanazosimamia.
Wabunge wa CCM waliofikishwa mahakamani ni Kangi Lugola (Mwibara), Victor Mwambalaswa (Lupa), na Suleiman Sadiq (Mvomero). Wanatuhumiwa kwa kwa kosa la kuomba rushwa ya milioni 30 kutoka kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Gairo ili wampendele katika kukagua hesabu za halmashauri yake mwaka 2015/16.
Mwingine ni Richard Ndassa (Sumve), ambaye anatuhumiwa kwa  kushawishi na kuomba rushwa ya Tsh 30 milioni kutoka kwa Felchesmi Mramba, Mtendaji Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)  ili amsaidie kuwashawishi wajumbe wengine wa Kamati ya Mtaji na Uwekezaji kupitisha bila kipingamizi taarifa ya TANESCO kwa mwaka 2015/2016.
Taarifa zinasema kuwa hadi Ijumaa iliyopita, Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) ilikuwa imehoji wabunge wengine 18 wa CCM, na ilikuwa imeshakamilisha taratibu zote za kuwafikisha mahakamani.
Miongoni mwa wabunge hao ni Martha Mlata (Viti Maalumu), Raphael Chegeni (Busega), Margareth Sitta (Urambo Mashariki), Mary Mwanjelwa (Viti Maalumu), Edwin Sanga (Kondoa Mjini). Majina mengine hayakupatikana hadi tunakwenda mitamboni.
Baada ya taarifa za kufikishwa mahakamani wabunge hao kuanza kuenea, kundi la wabunge wa CCM linadaiwa kumzonga Ndugai, wakimtaka awasimamie wabunge wa chama chake, asiruhusu wadhalilishwe.
Watoa habari wetu wanasema wabunge walimweleza Ndugai kuwa kitendo cha serikali kudhalilisha wabunge wa CCM kitaondoa umoja wao wa kutetea serikali, na kitaathiri msimamo wao katika umoja wa wabunge wa chama chao.
“Mweleze rais asitudhalilishe, sisi ni wabunge wa chama chake; asitafute sifa zake peke yake,” mbunge mmoja kijana alinukuliwa akimweleza Ndugai.
Kabla hata Ndugai hajawasiliana na rais kuhusu hoja za wabunge, taarifa zinasema rais mwenyewe alipata taarifa hizo kutoka kwa “vijana wake” ndani ya wabunge hao.
Mtoa habari kutoka Ikulu ameeleza gazeti hili kuwa Rais alipompigia simu Ndugai alizungumza kwa ukali, “hiyo ni mijizi, acha ifungwe tu.”
Gazeti hili lilipohitaji ufafanuzi wa Ndugai kuhusu masuala haya alithibitisha kuwa wabunge wake  wameshahojiwa na TAKUKURU, lakini akagoma kusema alichoambiwa na rais.
“Ni kweli kuna wabunge 18 wameshahojiwa na Takukuru. Hata hivyo, tumeshindwa kuwa na maelezo ya pamoja kwa kuwa kuna wengine wameitwa kama mashahidi, na wengine wamehojiwa kama watuhumiwa,” Alisema.
Alisema kilichotokea ni kwamba wabunge hao wamekuwa wanaitwa kwa nyakati tofauti, kwa sababu tofauti. “Mwingine anaitwa leo anahojiwa kwa tuhuma, mwingine anaitwa kesho kwa ushahidi pengine baada ya kutajwa na mwenzake,” alidokeza.
Baadhi ya wabunge wa CCM wameliambia gazeti hili kuwa kuna kesi zinatengenezwa kisiasa, hivyo wanajipa muda kuliweka sawa suala la tuhuma zinazowakabili.
Hata hivyo, taarifa zinasema wabunge wameikamia serikali, na wengi wao wanajiapiza kuunga mkono hoja za wapinzani kama namna ya kumkomoa Rais Magufuli.
Taarifa hizo hizo zinasema rais mwenyewe baada ya kusikia vitisho vya wabunge wa CCM, amemwambia Ndugai, “kama watatunisha misuli nitavunja bunge, turudi kwenye uchaguzi, tuone watarudi wangapi miongoni mwao.”
Taarifa hizi zinakuja ikiwa ni wiki moja tangu Spika kuahidi kuwa suala hilo litazungumzwa vizuri ndani ya Bunge kwa kuzingatia kanuni wala si mtaani. Source ni mwanahalisi..

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni