other blog

Jumanne, 22 Septemba 2015

Kwa vume kunani.. Liewig ajitetea Stand United kuchemsha Wakati uongozi wa Stand United ukiwakingia kifua mashabiki wa timu hiyo kwa kumfanyia vurugu


Kocha wa Stand United, Patrick Liewig
Dar es Salaam. Wakati uongozi wa
Stand United ukiwakingia kifua
mashabiki wa timu hiyo kwa
kumfanyia vurugu kocha, Patrick
Liewig mwenyewe amesema uwezo
wake hauwezi kupimwa kwa mechi
mbili.
Liewig ameiongoza Stand kushinda
mechi moja na kutoka sare mbili tangu
alipojiunga na timu hiyo alijikuta
kwenye wakati mgumu wa kutaka
kupigwa na mashabiki baada ya timu
yake kuruhusu kipigo cha mabao 2-0
dhidi ya Azam wiki iliyopita mjini
Shinyanga.
Akizungumza na gazeti hili jana,
Mfaransa huyo alisema anajiamini na
anaamini yeye ni kocha mwenye
uwezo huku akisisitiza asipimwe kwa
matokeo ya mechi mbili ambazo timu
yake imekwishapoteza tangu kuanza
kwa ligi.
“Nahitaji kupewa muda, timu ya Stand
inajengwa taratibu, mashabiki wawe
na subira endapo wanahitaji mafanikio
kwani naamini ushindi hupo,” alisema
kocha huyo kwa kifupi.
Mwenyekiti wa Stand United, Aman
Vicent alisema kitendo kilichofanywa
na mashabiki wao kinaweza kutokea
katika timu nyingine yoyote ni cha
kawaida katika soka.
“Unajua tulitarajia makubwa
ukizingatia kocha analipwa fedha
nyingi sasa kitendo cha kufungwa
mechi mbili mfululizo kiliwakasirisha
mashabiki na kulazimika kufanya kile
kilichotokea, lakini tumeyamaliza na
tunajipanga kwa mechi zijazo,”
alisema Vicent.
Liewig aliajiliwa kuinoa Stand kama
kocha mkuu miezi michache kabla ya
ligi kuanza, kocha huyo pia aliwahi
kuifundisha Simba huku akiacha
rekodi ya kuwaibua vijana kwenye
timu hiyo.
Naye Mchambuzi wa soka na kocha wa
zamani wa Taifa Stars, Mshindo Msolla
amemtetea kocha huyo raia wa
Ufaransa na kueleza kuwa hastahili
kulaumiwa hivi sasa kutokana na
matokeo ya timu hiyo imepata na
kusisitiza kuwa wachezaji wa timu hiyo
hakuwasajili yeye.
“Liewig hastahili lawama, timu
ameikuta tayari imesajiliwa hivyo
matokeo ya sasa yanawahusu uongozi,
wanachotakiwa kufanya kwa sasa ni
kumpa muda wa kuijenga timu hiyo na
itakapofika kipindi cha dirisha dogo
aachiwe afanye usajili wa wachezaji
anaowahitaji,” alisema Msolla.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni