other blog

Jumatatu, 19 Oktoba 2015

POSTED BY DENIC LYAMUYA EAGLEFM


Dar es Salaam. Zimesalia saa 144 za
kampeni ambazo wagombea wa vyama
vyote vya siasa watazitumia kutupa
karata zao za mwisho wakilenga
kupata ushawishi wa mwishomwisho
na hatimaye kunyakua ushindi.
Saa hizo za majeruhi zimesababisha
wagombea urais wa CCM, Dk John
Magufuli, Edward Lowassa wa
Chadema na Anna Mghwira wa ACT –
Wazalendo kujikita katika mikoa “ya
kimkakati” na ile yenye wapigakura
wengi.
Dk Magufuli ndiye aliyefungua pazia la
kampeni Agosti 23 kwenye viwanja wa
Jangwani, Dar es Salaam na kufuatiwa
na Lowassa hapohapo Jangwani kabla
ya Mghwira kuzindua huko Mbagala.
Wagombea hao ambao
wameshazunguka mikoa yote nchini,
watazitumia siku sita zilizobaki kabla
ya siku ya kupigakura kujiwekea
mazingira mazuri ya ushindi.
Akizungumzia mikakati ya mwisho ya
kampeni, Kaimu Katibu Mkuu wa
Chadema, Salum Mwalimu alisema
mikoa yote nchini ni ya kimkakati kwa
chama hicho na Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa), huku akieleza jinsi
Lowassa atakavyohitimisha siku
zilizobaki.
“Kwa sasa, mgombea anaendelea na
mikutano ya kampeni mkoani Mbeya.
Akimaliza huko atarejea Dar es Salaam
kwa ajili ya kufunga kampeni ila
atapita katika mikoa ya Iringa na
Morogoro.
“Tupo katika hatua za mwisho, hivyo
tunaweza kuangalia pia ni wapi
mgombea wetu anaweza kwenda
ukiacha maeneo hayo,” alisema
Mwalimu.
Mjumbe wa kamati ya kampeni ya
CCM, January Makamba alisema
mgombea urais wa chama hicho
atazitumia siku sita zilizobaki kupita
majimbo ambayo aliyaruka katika
baadhi ya mikoa.
“Lengo letu ni kwenda kwenye
majimbo yote, hivyo siku hizi zilizobaki
atapita huko. Kuhusu wapi tutafunga
kampeni zetu tutatangaza siku yoyote
kuanzia leo,” alisema Makamba.
Lowassa jana aliendelea na kampeni
mkoani Mbeya huku Dk Magufuli
akiwa katika Wilaya ya Magu mkoani
Mwanza.
Mikoa ya kimkakati na yenye
wapigakura zaidi ya milioni moja kila
mmoja ambayo huenda wagombea hao
wakaitumia kunadi sera zao za
mwishomwisho ni Morogoro, Tabora,
Dodoma, Kagera, Tanga, Arusha, Mara,
Geita, Kilimanjaro, Kigoma, Shinyanga,
Ruvuma, Mtwara na Simiyu.
Mambo yasiyosikika
Akizungumzia ahadi za wagombea hao,
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama
vya Wafanyakazi (Tucta), Nicolaus
Mgaya alisema wagombea wengi wa
urais wanazungumzia kuongeza
mishahara wafanyakazi, lakini
wanasahau kuzungumzia jinsi
watakavyoongeza marupurupu ya
wafanyakazi hao.
“Hapa nazungumzia kodi ya nyumba,
fedha za usafiri na malipo ya likizo,”
alisema Mgaya alipoulizwa kuhusu
ahadi za wagombea.
Ardhi na Katiba
Pamoja na wagombea hao kuahidi
kutatua migogoro ya ardhi, mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine
(Sua), Profesa Damian Gabagambi
anaona jambo hilo halijatolewa
maelezo ya kutosha.
“Ardhi ni jambo ambalo halijapewa
kipaumbele kwa maana ya kupimwa
na matumizi yake kuidhinishwa na
kulindwa kisheria. Mwingiliano wa
matumizi ya ardhi ni moja ya matatizo
makubwa nchini,” alisema Profesa
Gabagambi.
Alisema wagombea hao hawajagusia
suala la Watanzania kupata Katiba
Mpya, ambayo mchakato wake
ulikwama kabla ya hatua ya Kura ya
Maoni.
“Suala la kusaidia wakulima kupata
masoko ya uhakika halijafafanuliwa
kwa kina wala jinsi ya kuanzisha na
kuendeleza viwanda vidogovidogo kwa
sababu ndiyo vinaajiri wananchi wengi
kuliko vikubwa, ambavyo kila
mgombea anasema atavianzisha
akiingia madarakani,” alisema.
Itikadi
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa
Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu
Nyerere, Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM), Profesa Penina Mlama
alisema hakuna aliyesema akishinda
ataongoza nchi kwa itikadi ipi.
“Tunajua kuwa Wamarekani
wanatumia mfumo wa ubepari na
Mwalimu (Julius) Nyerere alitumia
ujamaa, sasa hawa wa sasa
(wagombea) wanaamini mfumo upi?”
alihoji Profesa Mlama.
Ahadi za Lowassa
Lowassa amekuwa akitumia ahadi ya
elimu bure kuanzia msingi hadi chuo
kikuu kama silaha yake kuu ya kupata
kura kwa wananchi.
“Kipaumbele cha kwanza ni elimu, cha
pili ni elimu na cha tatu ni elimu,”
alisema Lowassa tangu kwenye
uzinduzi wa kampeni zake na
amekuwa akirudiarudia kuhakikisha
kinaeleweka.
Pia, katika mikutano yake mingi waziri
huyo mkuu wa zamani amekuwa
akizungumzia jinsi ya kutatua tatizo la
maji, ambalo linaonekana kuwa kubwa
sehemu nyingi licha ya baadhi kuwa
na vijito, mito na maziwa, akitoa mfano
wa jinsi alivyoshughulikia mradi wa
maji ya Ziwa Victoria, ambao unasaidia
wakazi wa mikoa ya Mwanza, Tabora
na Mara.
“Nitahakikisha maziwa na mito
mikubwa kama Kagera inatumika
kuondoa tatizo la maji,” alisema
Lowassa alipozungumza na wananchi
wa Nkenge, Kagera.
“Kama niliweza kutoa maji Ziwa
Victoria nitashindwa vipi kutoa maji
kutoka Ziwa Tanganyika ili wananchi
mpate maji ya uhakika?” alisema
Lowassa katika mkutano wake wa
kampeni uliofanyika katika Uwanja wa
Mwanga Community Centre, Kigoma.
Lowassa, ambaye amekuwa akiwaita
waendesha bodaboda, wamachinga na
mamalishe kuwa ni marafiki zake,
amekuwa akiahidi kuanzisha benki
maalumu ya kuhudumia wajasiriamali
wadogo.
“Tumetengeza ilani kiboko ambayo
ndani ya miaka mitano Tanzania yetu
itabadilika, lazima tupunguze tabaka
kati ya tajiri na maskini kwa uchumi
wa pamba, chai, dhahabu na gesi kwa
nini tushindwe? Mkitupa ridhaa na
Mungu akikubali, tutakwenda kasi na
tutakuwa na maendeleo,” alisema
Lowassa katika mkutano uliofanyika
mjini Makambako.
Ahadi za Dk Magufuli
Kete kubwa tano za mgombea wa CCM,
Dk Magufuli ambazo amekuwa
akizinadi takriban kila mahali
anapokwenda tangu alipozindua
kampeni zake ni pamoja na kufuta
utaratibu wa kuwakamata na
kuwatoza ushuru usio na tija
waendesha bodaboda na mama lishe
na kuwabana wafanyabiashara
wakubwa kulipa kodi.
Kutoka Mpanda Vijijini alikoanzia
kampeni za mikoani hadi maeneo
anayoyafikia sasa, Dk Magufuli
amekuwa akipata zaidi shangwe pale
anapowaahidi awananchi kutoa
mikopo ya Sh50 milioni kwa kina
mama na vijana kwa kila kijiji nchi
nzima ili kukuza ujasiriamali na
kusomesha watoto bure kuanzia
darasa la kwanza hadi kidato cha nne.
Amekuwa akianisha mikakati yake ya
kudhibiti ufisadi nchini akiahidi
kuanzisha mahakama maalumu ya
kuwafunga mafisadi, ahadi ambao
imeonekana kumbeba kiasi cha
kutoisahau kila anapofanya mikutano
yake.
Katika kipindi hicho cha takriban siku
58 za kampeni, Dk Magufuli ambaye ni
waziri wa ujenzi, amekuwa akiahidi
kuinganisha nchi kwa kujenga
barabara za lami katika kila mkoa na
hata katika miji mikubwa isiyo na
barabara hizo kwenye mitaa na wiki
iliyopita wakati kampeni zilielekea
ukingoni alisaini mkataba wa ujenzi wa
barabara za juu jijini Dar es Salaam.
Ahadi hizo kubwa zimekuwa
zikisindikizwa na mikakati ya kujenga
Reli ya Kati, ya Kusini kuanzia Bandari
ya Mtwara – Songea – Mbamba Bay
kupitia Mchuchuma na Liganga na ile
ya Kaskazini kwa kiwango cha
kimataifa.
Dk Magufuli ameahidi kuboresha
huduma za afya na kusambaza maji na
umeme vijijini ili usaidie kufanikisha
mkakati wa kuifanya Tanzania kuwa
nchi ya viwanda.
Mghwira wa ACT
Mpaka sasa mgombea urais wa ACT-
Wazalendo, Anna Mghwira amefanya
kampeni katika mikoa mbalimbali Bara
na Zanzibar na ahadi zake kubwa
zikiwa ni kumaliza tatizo la maji, ujenzi
wa barabara, viwanda, migogoro ya
ardhi na elimu.
Upatikanaji wa majisafi na salama
umeonekana kuwa tatizo kuu katika
maeneo karibu mengi aliyozunguka
kufanya kampeni zake. Akiwa kwenye
mikoa ya Kanda ya Kusini na Kaskazini
na Dodoma, Tabora na Pwani aliahidi
kuwa serikali yake itapambana
kuondokana na tatizo hilo, kwa haoni
sababu ya kuendelea hasa ikizingatiwa
kuwa Tanzania ni nchi yenye vyanzo
vingi vya maji.
Akiwa Ruvuma kwenye majimbo ya
Tunduru Kusini na Kaskazini,
mgombea huyo aliahidi kuimaliza kero
ya muda mrefu inayowakabili wakazi
wa Tunduru na vitongoji vyake ya
ukosefu wa barabara iliyodumu kwa
kipindi cha zaidi ya miaka 54 ya
Uhuru, kwa kuhakikisha
inatengenezwa kwa kiwango cha lami.
Alirudia ahadi hiyo akiwa Lindi,
Mtwara, Katavi, Kigoma, Rukwa,
Dodoma na Tabora akisisitiza kuwa
nchi haiwezi kuendelea ikiwa hakuna
barabara zinazoungana na barabara
kuu. Kuhusu viwanda, amekuwa
akihoji ni nani walioviua
vilivyokuwapo?
Akiwa katika mikoa ya Kusini, Mtwara
Lindi Ruvuma, aliahidi Serikali yake
itahakikisha inajenga viwanda vya
korosho ili kuondokana na uuzaji wa
korosho ghafi kunakoipunguzia
mapato Serikali. Katika mikutano yake
aliyoifanya Korogwe na Handeni,
Tanga alisema ACT itawajengea
viwanda vya kusindika matunda ili
kuongeza ajira na pato kwa serikali.
Akiwa Mbulu mkoani Manyara,
aliahidi kujenga kiwanda cha pareto
pamoja na viwanda vidogovidogo vya
usagaji wa mazao ya ngano, dengu na
mahindi yanayopatikana kwa wingi
kwenye maeneo hayo.
Maoni ya wananchi
Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo
Kikuu cha Ruaha (Ruco), alisema ahadi
hizo zinaonekana kuwa nzuri na kujibu
vilio vya wananchi lakini tatizo kubwa
linatokea katika utekelezaji wake
kutokana na mfumo mzima wa
kiuchumi.
Alisema rais yoyote atakayepita ili
atekeleze ahadi za elimu bure, afya na
maji bure atatakiwa kupambana zaidi
na mfumo wa uchumi wa dunia ambao
hauungi mkono sera hizo za kijamaa.
Mkazi wa Kigogo, Salim Juma alisema
ahadi za Dk Magufuli ni nzuri na kwa
utendaji zinaweza kutekelezwa lakini
tatizo lipo kwenye chama chake
ambacho kimekithiri ufisadi na hakipo
tayari kwa mabadiliko hivyo
kupunguza kasi ya utekelezaji.
Dar es Salaam. Zimesalia saa 144 za
kampeni ambazo wagombea wa vyama
vyote vya siasa watazitumia kutupa
karata zao za mwisho wakilenga
kupata ushawishi wa mwishomwisho
na hatimaye kunyakua ushindi.
Saa hizo za majeruhi zimesababisha
wagombea urais wa CCM, Dk John
Magufuli, Edward Lowassa wa
Chadema na Anna Mghwira wa ACT –
Wazalendo kujikita katika mikoa “ya
kimkakati” na ile yenye wapigakura
wengi.
Dk Magufuli ndiye aliyefungua pazia la
kampeni Agosti 23 kwenye viwanja wa
Jangwani, Dar es Salaam na kufuatiwa
na Lowassa hapohapo Jangwani kabla
ya Mghwira kuzindua huko Mbagala.
Wagombea hao ambao
wameshazunguka mikoa yote nchini,
watazitumia siku sita zilizobaki kabla
ya siku ya kupigakura kujiwekea
mazingira mazuri ya ushindi.
Akizungumzia mikakati ya mwisho ya
kampeni, Kaimu Katibu Mkuu wa
Chadema, Salum Mwalimu alisema
mikoa yote nchini ni ya kimkakati kwa
chama hicho na Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa), huku akieleza jinsi
Lowassa atakavyohitimisha siku
zilizobaki.
“Kwa sasa, mgombea anaendelea na
mikutano ya kampeni mkoani Mbeya.
Akimaliza huko atarejea Dar es Salaam
kwa ajili ya kufunga kampeni ila
atapita katika mikoa ya Iringa na
Morogoro.
“Tupo katika hatua za mwisho, hivyo
tunaweza kuangalia pia ni wapi
mgombea wetu anaweza kwenda
ukiacha maeneo hayo,” alisema
Mwalimu.
Mjumbe wa kamati ya kampeni ya
CCM, January Makamba alisema
mgombea urais wa chama hicho
atazitumia siku sita zilizobaki kupita
majimbo ambayo aliyaruka katika
baadhi ya mikoa.
“Lengo letu ni kwenda kwenye
majimbo yote, hivyo siku hizi zilizobaki
atapita huko. Kuhusu wapi tutafunga
kampeni zetu tutatangaza siku yoyote
kuanzia leo,” alisema Makamba.
Lowassa jana aliendelea na kampeni
mkoani Mbeya huku Dk Magufuli
akiwa katika Wilaya ya Magu mkoani
Mwanza.
Mikoa ya kimkakati na yenye
wapigakura zaidi ya milioni moja kila
mmoja ambayo huenda wagombea hao
wakaitumia kunadi sera zao za
mwishomwisho ni Morogoro, Tabora,
Dodoma, Kagera, Tanga, Arusha, Mara,
Geita, Kilimanjaro, Kigoma, Shinyanga,
Ruvuma, Mtwara na Simiyu.
Mambo yasiyosikika
Akizungumzia ahadi za wagombea hao,
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama
vya Wafanyakazi (Tucta), Nicolaus
Mgaya alisema wagombea wengi wa
urais wanazungumzia kuongeza
mishahara wafanyakazi, lakini
wanasahau kuzungumzia jinsi
watakavyoongeza marupurupu ya
wafanyakazi hao.
“Hapa nazungumzia kodi ya nyumba,
fedha za usafiri na malipo ya likizo,”
alisema Mgaya alipoulizwa kuhusu
ahadi za wagombea.
Ardhi na Katiba
Pamoja na wagombea hao kuahidi
kutatua migogoro ya ardhi, mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine
(Sua), Profesa Damian Gabagambi
anaona jambo hilo halijatolewa
maelezo ya kutosha.
“Ardhi ni jambo ambalo halijapewa
kipaumbele kwa maana ya kupimwa
na matumizi yake kuidhinishwa na
kulindwa kisheria. Mwingiliano wa
matumizi ya ardhi ni moja ya matatizo
makubwa nchini,” alisema Profesa
Gabagambi.
Alisema wagombea hao hawajagusia
suala la Watanzania kupata Katiba
Mpya, ambayo mchakato wake
ulikwama kabla ya hatua ya Kura ya
Maoni.
“Suala la kusaidia wakulima kupata
masoko ya uhakika halijafafanuliwa
kwa kina wala jinsi ya kuanzisha na
kuendeleza viwanda vidogovidogo kwa
sababu ndiyo vinaajiri wananchi wengi
kuliko vikubwa, ambavyo kila
mgombea anasema atavianzisha
akiingia madarakani,” alisema.
Itikadi
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa
Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu
Nyerere, Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM), Profesa Penina Mlama
alisema hakuna aliyesema akishinda
ataongoza nchi kwa itikadi ipi.
“Tunajua kuwa Wamarekani
wanatumia mfumo wa ubepari na
Mwalimu (Julius) Nyerere alitumia
ujamaa, sasa hawa wa sasa
(wagombea) wanaamini mfumo upi?”
alihoji Profesa Mlama.
Ahadi za Lowassa
Lowassa amekuwa akitumia ahadi ya
elimu bure kuanzia msingi hadi chuo
kikuu kama silaha yake kuu ya kupata
kura kwa wananchi.
“Kipaumbele cha kwanza ni elimu, cha
pili ni elimu na cha tatu ni elimu,”
alisema Lowassa tangu kwenye
uzinduzi wa kampeni zake na
amekuwa akirudiarudia kuhakikisha
kinaeleweka.
Pia, katika mikutano yake mingi waziri
huyo mkuu wa zamani amekuwa
akizungumzia jinsi ya kutatua tatizo la
maji, ambalo linaonekana kuwa kubwa
sehemu nyingi licha ya baadhi kuwa
na vijito, mito na maziwa, akitoa mfano
wa jinsi alivyoshughulikia mradi wa
maji ya Ziwa Victoria, ambao unasaidia
wakazi wa mikoa ya Mwanza, Tabora
na Mara.
“Nitahakikisha maziwa na mito
mikubwa kama Kagera inatumika
kuondoa tatizo la maji,” alisema
Lowassa alipozungumza na wananchi
wa Nkenge, Kagera.
“Kama niliweza kutoa maji Ziwa
Victoria nitashindwa vipi kutoa maji
kutoka Ziwa Tanganyika ili wananchi
mpate maji ya uhakika?” alisema
Lowassa katika mkutano wake wa
kampeni uliofanyika katika Uwanja wa
Mwanga Community Centre, Kigoma.
Lowassa, ambaye amekuwa akiwaita
waendesha bodaboda, wamachinga na
mamalishe kuwa ni marafiki zake,
amekuwa akiahidi kuanzisha benki
maalumu ya kuhudumia wajasiriamali
wadogo.
“Tumetengeza ilani kiboko ambayo
ndani ya miaka mitano Tanzania yetu
itabadilika, lazima tupunguze tabaka
kati ya tajiri na maskini kwa uchumi
wa pamba, chai, dhahabu na gesi kwa
nini tushindwe? Mkitupa ridhaa na
Mungu akikubali, tutakwenda kasi na
tutakuwa na maendeleo,” alisema
Lowassa katika mkutano uliofanyika
mjini Makambako.
Ahadi za Dk Magufuli
Kete kubwa tano za mgombea wa CCM,
Dk Magufuli ambazo amekuwa
akizinadi takriban kila mahali
anapokwenda tangu alipozindua
kampeni zake ni pamoja na kufuta
utaratibu wa kuwakamata na
kuwatoza ushuru usio na tija
waendesha bodaboda na mama lishe
na kuwabana wafanyabiashara
wakubwa kulipa kodi.
Kutoka Mpanda Vijijini alikoanzia
kampeni za mikoani hadi maeneo
anayoyafikia sasa, Dk Magufuli
amekuwa akipata zaidi shangwe pale
anapowaahidi awananchi kutoa
mikopo ya Sh50 milioni kwa kina
mama na vijana kwa kila kijiji nchi
nzima ili kukuza ujasiriamali na
kusomesha watoto bure kuanzia
darasa la kwanza hadi kidato cha nne.
Amekuwa akianisha mikakati yake ya
kudhibiti ufisadi nchini akiahidi
kuanzisha mahakama maalumu ya
kuwafunga mafisadi, ahadi ambao
imeonekana kumbeba kiasi cha
kutoisahau kila anapofanya mikutano
yake.
Katika kipindi hicho cha takriban siku
58 za kampeni, Dk Magufuli ambaye ni
waziri wa ujenzi, amekuwa akiahidi
kuinganisha nchi kwa kujenga
barabara za lami katika kila mkoa na
hata katika miji mikubwa isiyo na
barabara hizo kwenye mitaa na wiki
iliyopita wakati kampeni zilielekea
ukingoni alisaini mkataba wa ujenzi wa
barabara za juu jijini Dar es Salaam.
Ahadi hizo kubwa zimekuwa
zikisindikizwa na mikakati ya kujenga
Reli ya Kati, ya Kusini kuanzia Bandari
ya Mtwara – Songea – Mbamba Bay
kupitia Mchuchuma na Liganga na ile
ya Kaskazini kwa kiwango cha
kimataifa.
Dk Magufuli ameahidi kuboresha
huduma za afya na kusambaza maji na
umeme vijijini ili usaidie kufanikisha
mkakati wa kuifanya Tanzania kuwa
nchi ya viwanda.
Mghwira wa ACT
Mpaka sasa mgombea urais wa ACT-
Wazalendo, Anna Mghwira amefanya
kampeni katika mikoa mbalimbali Bara
na Zanzibar na ahadi zake kubwa
zikiwa ni kumaliza tatizo la maji, ujenzi
wa barabara, viwanda, migogoro ya
ardhi na elimu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni