other blog

Alhamisi, 23 Julai 2015

AU yateka ngome ya mwisho ya Al shaabab


Mji muhimu wa mwisho uliokuwa
mikononi mwa kundi la Al Shabaab
kusini magharibi mwa Somalia wa
Baardheere umechukuliwa tena na
vikosi vya Muungano wa Afrika (AU) -
miaka 7 baada ya wapiganaji hao
wenye itikadi kali kuingia kwa mara
ya kwanza katika mji huo .
Wakazi wa mji huo wamesema vikosi vya
Kenya na Somalia vikiwa na silaha nzito
na usaidizi wa mashambulizi ya anga
viliuvamia mji huo , ambao wapiganaji wa
Al Shabaab waliutoroka usiku.
Vikosi vya AU nchini Somalia, na vile vya
jeshi la Somalia, vilifanikiwa kuuteka mji
huo baada ya mashambulizi makali.
Majeshi kutoka Kenya, Somalia na
Ethiopia yamekua yakiendesha harakati
za kuuteka mji wa Baadheere kwa siku
chache zilizopita.
Kumekuwa na mapigano makali viungani
mwa mji huo, lakini wanamgambo wa
Alshaabab walisalim amri na kuukimbia
,na hivyo kutoa fursa ya mji huo
kuchukuliwa bila mapigano .
Wakazi wanasema kamanda mmoja wa
Somali na vyombo vya habari
vinavyounga mkono Al Shabaab
wamethibitisha kuchukuliwa kwa mji huo.
Harakati hizo za kuuteka mji wa
Baadheere zimefanikiwa siku chache
kabla rais wa Marekani Barack Obama
kufanya ziara Afrika mashariki ambapo
suala la usalama nchini Somalia litakuwa
kwenye ajenda kuu za ziara yake .
Kundi la Al shaabab lina uhusiano na
mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda
linapigana dhidi ya serikali ya Somalia
kwa ajili ya udhibiti wa nchi hiyo.
Wiki iliyopita mashambulizi ya ndege
zisizokua na rubani (drone)
zilizoshambulia ziliripotiwa kuwauwa
makamanda wa ngazi ya juu wa Al
Shabaab.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni