other blog

Jumamosi, 25 Julai 2015

MakalaElimu yakoma kuwa ufunguo wamaisha

Wadau walalamikia MMEM na MMESNI wanafunzi 126,847 tu kati ya 367,756 waliofanya mtihani mwaka2012 waliofaulu katika viwango mbalimbali, 240,909 waliobaki hawakuambua kitu.Matokeo hayo yaliishitua Serikali iliyolazimika kuunda Tume kutafutachanzo cha tatizo. Tayari Tume hiyo imewasilisha taarifa yake serikalini na tayari Serikali imekwishaliagiza Baraza la Mitihani la Taifa kurekebisha matokeo hayo.Kuporomoka kwa matokeo hayo ni mwendelezo wa mporomoko wa siku nyingi; kwa mfano, mwaka 2007 ambapo ufaulu ulikuwa asilimia 90.3, ulishuka mwaka uliofuata, 2008 kwa asilimia 7.4 kufikia asilimia 83.6 ya ufaulu. Na mwaka 2009, ufaulu ulishuka kwa asilimia 13.2 kutoka ule wa 2008 wa asilimia 83.6 hadi asilimia 72.5; na kushuka tena kwa asilimia 30.5 kutoka ufaulu wa 2009 hadi asilimia 50.4 mwaka 2010.Mwaka 2011, ufaulu uliporomoka kwa asilimia 7.9 kutoka ule wa 2010, hadi asilimia 46.4 mwaka huo; na ukaendelea kuporomoka kutoka asilimia 46.4 [2011] hadi asilimia 34.5 mwaka 2012.Kwa mujibu wa takwimu hizi ni kwamba, matokeo ya mitihani ya kidato cha nne yameendelea kuporomoka kwa miaka yote sita mfululizo, na kwamba, pamoja na sababu za kufeli zilizotolewa na Tume ya Serikali, ukweli unabakia kuwa matokeo hayo yalikuwa hayaepukiki kama tutakavyoona katika makala haya.Kati ya Wanafunzi 367,756 waliofanya mtihani mwaka 2012 nchini, wanafunzi 240,909, sawa naasilimia 65.5 walipata daraja sifuri;wanafunzi 103,327 sawa na asilimia 28.1 walipata daraja la nne, na wanafunzi 23,520 sawa na asilimia 6.4 walipata daraja kati ya la kwanza na la tatu; ambapo wanafunzi 1,641 kati ya hao walipata daraja la kwanza, 6,453 daraja la pili na 15,426 walipata daraja la tatu.Kwa mujibu wa Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, unaojumuisha Wilaya za Shinyanga (Mjini na Vijijini), Kahama na Kishapu, Eva Lopa, Mkoa una shule za sekondari127, zikiwamo za Serikali 111 na 16za mashirika ya dini na watu binafsi.Anakiri kuwa, ufaulu, hususan, kwamitihani ya kidato cha nne kwa miaka miwili, 2011 na 2012, umeshuka kutoka asilimia 63.7 ambapo kwa mwaka 2011 wanafunzi 8,913 kati ya 13,988 waliofanya mtihani huo walifaulu kwa daraja la kwanza hadi la nne; na wanafunzi 5,075, sawa na asilimia 36.3, walifeli kwa kupata daraja sifuri; ikilinganishwa na mwaka 2012 ambapo kati ya wanafunzi 7,814 waliofanya mtihani huo, 3,775 walishinda kwa kati ya daraja la kwanza na la nne, sawa na asilimia 48 ya waliofanya mtihani, na 4,039, sawa na asilimia52, walipata daraja sifuri.Anazitaja changamoto kuwa ni pamoja na upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi, kwa Wilaya ya Kahama yenye shule za sekondari 42 za Serikali, mahitaji mwaka 2012 yalikuwa ni 980, lakini walikuwapo 502, sawa na asilimia 52 ya mahitaji; Wilaya ya Kishapu (shule 26) mahitaji yalikuwa walimu 576, waliokuwapo ni 207 (36%); Shinyanga Mjini (shule 179) mahitaji yalikuwa walimu 424, waliokuwapo ni 313 (74%), na Shinyanga Vijijini (shule 26) walihitajika walimu 750, lakini kulikuwa na walimu 358 tu, sawa na asilimia 48 ya mahitaji.Kwa ujumla, uhitaji wa walimu ulifikia wastani wa zaidi ya asilimia 50, hivi kwamba, ingawa tatizo la upungufu wa walimu lipo, lakini si kubwa kuweza kuathiri matokeo kwa kiwango cha ufaulu duni wa mwaka 2012.“Hili japo ni tatizo, lakini si kubwa sana. Kwani pamoja na upungufu wa asilimia 47 wa walimu mwaka 2012 ilipofanyika mitihani yenye matokeo haya, bado Mkoa ulipangiwa jumla ya walimu wengine wapya 461, wakiwemo 250 wa shahada na 211 wa stashahada, ambapo walimu 188 wa stashahada na wengine 165 wa shahada walikwisharipoti”, anasema Lopa.Ukiondoa tatizo duni la upungufu wa walimu,Raia Mwemakatika utafiti wake wa kiuandishi wa habari, limebaini kuwa, tatizo mojakubwa ni miundombinu ambapo kwa mfano, mwaka 2012 wakati mahitaji ya madarasa yalikuwa madarasa 1,593 kwa Mkoa mzima, kulikuwa na madarasa 942 tu, sawa na asilimia 59 ya mahitaji.Mahitaji ya nyumba za walimu yalikuwa nyumba 1,742, lakini zilikuwapo 255 tu, sawa na asilimia15 ya mahitaji; mahitaji ya madawati yalikuwa 46,378, yaliyokuwapo ni 31,292, sawa na asilimia 67 ya mahitaji. Katika haya, tatizo la nyumba za walimu ni kubwa, hasa kwa walimu wa shule za sekondari za vijijini na kusababisha maisha magumu na ya kukatisha tamaa walimu.Vitendea kazi nalo limetajwa kuwa tatizo kubwa. Kwa mujibu wa Lopa, kwa mwaka 2012, shule zilihitaji jumla ya maabara 333, lakini kulikuwa na maabara 42 tu, sawa na asilimia 13 ya mahitaji; maktaba zilitakiwa 113, zilizokuwapo ni nne tu sawa na asilimia 3.5 ya mahitaji; hosteli zilitakiwa 319, lakini kulikuwa na 33tu, sawa na asilimia 10 ya mahitaji.Ukichukulia upungufu mkubwa wa maabara, na upungufu wa walimu wa sayansi, ambao masomo wanayofundisha lazima yatahiniwe katika mitihani, ni dhahiri matokeo yatakuwa mabayakwa vyovyote vile.“Masomo ya sayansi yanayotegemea maabara, kama vile bailojia, kemia na fizikia lazimayatahiniwe; unatarajia nini kwa mwanafunzi ambaye hajawahi kuona maabara mbali na kufeli?”, anahoji Afisa Elimu Wilaya ya Shinyanga, Josephat Ntabindi.Tatizo si mchakato, ni MMEM na MMESWanafunzi walioathiriwa na matokeo hayo ya mwaka 2012 ni wale waliomaliza darasa la saba mwaka 2008, chini ya programu yaMpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi – MMEM, ulioanzishwa mwaka 2002; wakajiunga na kidato cha kwanza mwaka 2009 hadi cha nne mwaka 2012, chini ya programu ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari – MMES, ulioasisiwa mwaka 2004. Ni kusema kwamba, hawa ndio waanzilishi na wahitimu wa kwanzawa kidato cha nne chini ya mipango hiyo miwili ya majaribio kwa pamoja.Mpango wa MMEM unalenga kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anakwenda na kumaliza elimu ya msingi bila kutahiniwa wala kukatisha masomo. Chini ya mpango huu, mitihani ya darasa la nne ya kuwapima uwezo na kuwaimarishawanafunzi kimasomo, ilifutwa na kuingiza mtindo wa kuzoa wanafunzi kwenye “kokoro” – wazuri na wabovu, ilimradi wamalize elimu ya msingi bila kujali elimu bora, bali bora elimu, au bora liende.Kwa Mkoa wa Shinyanga, takwimu zifuatazo za ufaulu duni, zinathibitisha kuporomoka kwa elimu ya msingi chini ya MMEM, na hivyo kuingiza wanafunzi dhaifuelimu ya sekondari: mwaka 2007 ufaulu ulishuka kutoka asilimia 59.8 na mwaka 2006 ulishuka hadi asilimia 33.6. Vivyo hivyo, mwaka 2008 ufaulu ulikuwa asilimia 34.0, ulishuka kufikia asilimia 31.9 mwaka 2009. Na kwa miaka 2010, 2011 na 2012, kulikuwa na ongezeko dogo la ufaulu lisilozidi asilimia mbili juu ya asilimia 31 ya2009.Mpango wa MMES, uliobuniwa na kuanza kutumika mwaka 2004, unalenga kuhakikisha idadi ya watoto wanaoingia sekondari inaongezeka bila kuchujwa wala kuzingatia ubora wa elimu wanayopata wakiwemo wale wa “kokoro” la MMEM, hadi wafike kidato cha nne. Chini ya MMES, mitihani ya kidato cha pili ya kuchuja na kuwaimarisha wanafunzi kuingia kidato cha tatu ilifutwa.Lengo la mipango hii miwili (MMEM na MMES) ni kujaza madarasa bila ubora wa elimu. Ukichukulia kwamba shule zote chini ya programu hizi zilianzishwabila maandalizi wakati huo huo zikiandamwa na uhaba wa maabara, walimu wa sayansi, mabweni na nyumba za walimu, vitabu, hamasa duni ya walimu ya kujitolea na kutoridhika na kazi ya ualimu; matokeo yake ni kwa shulekuzalisha wanafunzi “wanaofaulu” bila kujua kusoma na kuandika.“Kuondolewa kwa mitihani ya mchujo kwa darasa la nne na kidato cha pili, kumegeuza shule hizi kuwa za kisiasa zaidi na janga kwa elimu. Tunakwenda wapi?”, anahoji Mkuu wa Shule ya Sekondari, Bunambiyu wilayani Kishapu, Fortunatus Misana, na kuongeza kuwa, haishangazi kuonawanafunzi wakiingia kidato cha kwanza bila kujua kusoma na kuandika; na kwamba hawa ndio sehemu ya wahanga wa matokeo ya 2012.Mwalimu Mkuu wa shule moja Wilayani Kahama, ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alilaumu viongozi wa Serikali kutotilia maanani maslahi duni ya walimu huku wao (viongozi) wakishindana kupora na kujinufaisha na rasilimali za Taifa. Alisema: “Walimu kufundisha hukuwamekata tamaa kutokana na maslahi duni ni changamoto kwa elimu nchini; viongozi wametia pamba masikioni, wamejifanya kutokuona kwamba walimu bado wamo ndani ya mgomo baridi”.Aliongeza: “Kauli za viongozi kwamba anayeona kazi ya ualimu hailipi, atafute kazi nyingine; au kwamba, hata walimu wasiponipigia kura nitapigiwa na watu wengine, ni kudharau kazi na taaluma ya ualimu.”Akihusisha hayo na matokeo mabaya ya kidato cha nne ya mwaka 2012, alisema: “Kauli kama hizi zinakatisha tamaa na zilitolewawakati vijana hawa wakiwa kidato cha kwanza mwaka 2009; na sote tumejionea matokeo yake”.Hoja ya Mwalimu huyu, kama ilivyopia hoja ya Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Lopa, ni kwamba, sualala upungufu wa walimu si zito kusababisha matokeo mabaya kiwango cha mwaka 2012, bali ni walimu kutosikilizwa, miundombinu duni na programu za elimu zisizofanyiwa utafiti kabla ya kuanza kutumika.Wakati haya yakitokea, swali linaloulizwa ni: “Wako wapi watotowa viongozi kama wanasiasa na wengineo wa Wilaya na Mikoa, wanaohamasisha kuwapo kwa shule za MMEM na MMES?”.Udhaifu TAMISEMIHatua ya kuhamishia shule za sekondari kwenye mamlaka ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kutoka usimamizi wa Wizara ya Elimu tangu mwaka 2009; kumedhoofisha na kuteteresha usimamizi na ukaguzi wa shule hizo kutokana na udhaifu wa TAMISEMI kifedha, kimiundombinu na kirasilimaliwatu, hivyo kufanya shule ziendeshwe kisiasa zaidi badala ya kuendeshwa kitaaluma.Kana kwamba, balaa hili liliwalenga vijana hao waliomaliza kidato cha nne mwaka 2012, hatua hii ilichukuliwa wakati vijana hao ndiyo wameingia tu kidato cha kwanza chini ya MMES.Hatua hii imetafsiriwa kuwa ni kujivua (kutelekeza?) kwa Serikali Kuu kusimamia elimu, kana kwamba elimu si haki ya wananchi kama ilivyo tu haki ya usalama kwaraia unaosimamiwa na Serikali Kuu.“TAMISEMI wana uzoefu wa kusimamia elimu ya msingi zaidi kuliko elimu ya sekondari; kuwavisha mzigo wa elimu ya sekondari bila maandalizi ni kuiweka rehani elimu hiyo”, anasema Mwalimu Castory Kassiga, ambaye ni mwalimu mkuumstaafu wa Shule ya Sekondari OldShinyanga.Yapo maoni pia kwamba kuwekwa kwa shule za sekondari chini ya usimamizi wa Serikali za Mitaa zinazosimamiwa na madiwani wanasiasa na Bodi za Shule zenye wajumbe wengi wasio na elimu ya masuala ya usimamizi wa elimu, kumesababisha shule hizo kuathiriwa na mazingira na kupoteza ubora, hadhi, na heshimaya elimu kwa ujumla.Kwa mujibu wa maoni hayo, si nadra kukuta shule ya sekondari imefungwa kwa siku moja au zaidi, kutokana na walimu kutakiwa kushiriki kwenye matukio na majanga ya kijamii kama vile yowe (mwano) la kuibiwa mifugo kijijini, vilio na harambee nyingine za kijadi, kwa kuhofia kuadhibiwa kwakutoshiriki kwao kama sehemu ya wanavijiji chini ya Serikali za Vijiji.Utafiti uliofanywa naRaia Mwemakwa Wilaya za Kahama, Kishapu naShinyanga umebaini kuporomoka kwa ukaguzi wa shule kwa wilaya zote kwa sababu ya uhaba wa wakaguzi na vitendea kazi kama vile magari na fedha. Wilaya zote hizi hazina gari hata moja kwa ajili ya ukaguzi wa shule za sekondari, ikilinganishwa na vitengo vya elimuya msingi ambavyo vina gari zaidi ya moja pamoja na fedha za kutosha.Kwa mfano, kwa mwaka 2012/2013, Bajeti ya Elimu ya Sekondari kwa Wilaya ya Shinyanga, ilikuwa Shs. 309m na Sh. 2m tu kwa matumizi mengineyo kwa mwezi; ikilinganishwa na bajeti ya Sh. 1bn na matumizi ya sh. 25m kwa mwezikwa elimu ya msingi. Pamoja na kuwekewa fungu duni, hata zilipotolewa mara nyingi sehemu ya fedha hizo zilitumika kwa shughuli tofauti na za elimu kwa vile hakuna anayejali.Mwaka 2012, kwa Mkoa mzima, ukaguzi wa shule za sekondari ulifanyika kwa asilimia 10 tu, ikilinganishwa na asilimia 25 kwa shule za msingi kutokana na uhabawa Bajeti na Wakaguzi. Matokeo hasi ya ukaguzi duni kwa shule hizo ni pamoja na utendaji wa walimu kutopimwa; utekelezaji wa mitaala kupuuzwa; na maendeleo ya shule na wanafunzi kutopimwa na hivyo kuzalisha watahiniwa na wahitimu mazuzu.Kwa mujibu wa Lopa, Mkoa hauna wakaguzi wa shule za sekondari wenye sifa, na badala yake kazi hiyo inafanywa kwa sehemu kubwana waratibu wa elimu ya msingi.“Kusema kweli shule nyingi hazikaguliwi kwa sababu ya ukosefu wa fedha; na zile zinazokaguliwa, ukaguzi si thabiti kwa kutokuwa na wakaguzi wenye sifa”, anabainisha Lopa.Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari,Ibinzamata, ambaye pia ni Katibu wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari (TAHOSA) Mkoa wa Shinyanga, Nassoro Busuri, anatahadharisha juu ya athari za MMEM, MMES na usimamizi wa elimu ya sekondari kuhamishiwa TAMISEMI chini ya muundo na mfumo wa elimu uliopo sasa nchini:Anaonya Busuri: “MMEM, MMES na TAMISEMI ni kaburi la elimu nchini. Kama Serikali itaendelea kukumbatia na kulea mifumo ya elimu kama huu, inayozalisha wahitimu wa kwenda kuporomosha, kumomonyoa, kugawa na kuuwa Taifa; wahitimu wasiohitaji kusoma wala kuwa na vyeti vyenye mamlaka, bali vyeti tu vya kuingia darasani, basi tusahau maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa nchi yetu na nafasi yetu ya ushindani katika Shirikisho tarajiwa la Afrika Mashariki.”Kama anayosema Katibu wa TAHOSA Mkoa wa Shinyanga, yana ukweli ndani yake; basi, kwetu elimu sasa sio tena ufunguo wa maisha, bali ni kifungo kwa kufuli la maisha”.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni