other blog

Jumatano, 29 Julai 2015

Vip diamondi ataweza... Akon kuleta umeme Afrika


Muimbaji wa miondoko ya R&b anayeongoza katika chati za juu za muziki huo duniani 'Akon' ameamua kutumia tasnia yake ya muziki kukabiliana na maendeleo endelevu ya watu wa barani Afrika.Nyota huyo wa R & B anazindua mpango maalumu wa mafunzo unaoitwa "Akon Angaza Afrika" ambao una lengo la kutumia nguvu ya jua kuzalisha umeme huku akiwa na matumaini ya kuwafikia watu milioni 600 baraniwa Afrika.Ufunguzi wa huo umefanyika mjini mkuu wa Bamako nchini Mali, baadaye mafunzo hayo yatafundisha kwa wadau wa mradi huo jinsi ya kutunza mifumo ya nishati hiyo inayoendeshwa kwa nguvu ya jua.Samba Bathily ambaye ni mwanzilishi msaidizi wa mradi huo, anasema jua na teknolojia hiyo ya ubunifu itasaidia kuleta umeme katika nyumba na kwenyejamii kwa ujumla.Kwa sasa anasema kuwa wanaimarisha utaalamu wa Kiafrika na kwamba hilo ni lengo lao.Ameelezea sababu ya kuwekeza zaidi kwenye nishatiya umeme kwamba ni moja ya njia ya kutoa fursa za kiuchumi na huduma za kijamii kwa bara la Afrika ambalo sehemu kubwa ni giza kutokana na ukosefu wa Nishati.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni