other blog

Alhamisi, 23 Julai 2015

Chapa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) TFDA Dodoma yateketeza bidhaa feki za Mil. 20/- .


Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)
Kanda ya Kati imeteketeza bidhaa
zisizofaa kwa matumizi ya binadamu
zenye thamani ya Sh. milioni 20.
Akizungumza mara baada ya kukamilika
kwa kazi ya uteketezaji jana mjini hapa,
Kaimu Meneja wa TFDA Kanda ya Kati,
Fredrick Luyangi, alisema bidhaa
zilizoteketezwa zina uzito wa tani 4.4.
Luyangi alisema bidhaa hizo ni dawa tani
0.44, chakula tani 3.08 na vipodozi uzito
wa tani 0.93.
Aidha, TFDA imewaonya wafanyabiashara
kuacha kuuza bidhaa zisizofaa, zilizoisha
muda wa matumizi na pia vipodozi
vyenye viambata vilivyopigwa marufuku
baada ya kuonekana kuwa vina sumu.
"Wafanyabiashara wote wanatakiwa
kuzingatia kanuni na sheria ili wauze
dawa, vyakula na vipodozi vinavyofaa kwa
matumizi ya binadamu," alisema.
Aliongeza vilevile kuwa wananchi
wanapaswa kuepuka matumizi ya vyakula,
dawa na vipodozi ambavyo vimeisha
muda wake na ambavyo havijasajiliwa
nchini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni