other blog

Jumanne, 28 Julai 2015

Obama sasa rasmi aonyesha kero kwa viongozi wa afrika watukutu wa madaraka... na benson mwAnga.


Rais wa Marekani Barrack
Obama,amewasuta viongozi wa Afrika
ambao wanaendelea kusalia
madarakani hata baada ya katiba
kutowaruhusu kuendelea kuwania
tena wadhfa wa urais.
Katika hotuba ya kwanza ya rais wa
Marekani kwa muungano wa Afrika katika
makao makuu ya umoja huo mjini Addis
Ababa,amesema kuwa Afrika haitapiga
hatua iwapo viongozi wake watakataa
kuondoka madarakani baada ya muda
wao kuisha.
Amemtaja hayati Nelson Mandela wa
Afrika Kusini, ambaye alikaa madarakani
kwa muhula mmoja tu wa miaka mitano
na anafahamika pakubwa kote duniani
huku akiheshimiwa kama kigogo wa bara
Afrika, tofauti na marais wengi
wanaoendelea kukwamia madaraka.
Ameongezea kuwa wakati waandishi
wanapofungwa huku wanaharakati
wakitishwa,demokrasia huwepo tu kwa
jina.
Akimnukuu shujaa Nelson Mandela
akisema kuwa unapoheshimu uhuru wa
wengine watu wote huwa huru.
Amesema kuwa ishara kuu ya maendeleo
katika taifa ni vile linavyowachukulia
wanawake wake.
Amewaambia viongozi wa Afrika kwamba
maendeleo ya bara hili yanategemea
demokrasia,uhuru na haki za
kibinaadamu.
Anasema kuwa muda umewadia wa
kubadilisha mtizamo wa Afrika kama bara
duni lenye kulemewa na umaskini na
mizozo.
Aidha amepongeza umoja wa Afrika AU
na shirika la Umoja wa mataifa katika
mapambano dhidi ya makundi ya
wapiganaji wa kiislamu kama vile, Boko
Haram kaskazini mwa Nigeria na Al -
Shaabab Afrika mashariki.
Amemtaja hayati Nelson Mandela wa
Afrika Kusini, ambaye alikaa madarakani
kwa muhula mmoja tu wa miaka mitano
na nafahamika pakubwa kote duniani
huku akiheshimiwa kama kigogo wa bara
Afrika, tofauti na marais wengi
wanaoendelea kukwamia madaraka.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni