other blog

Jumatano, 29 Julai 2015

NA KTK MICHEZO CECAFA:Gor Mahia yafuzu nusu fainali


Mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini Kenya, Gor Mahia wameendeleza fomu yao bora katika kombe la CECAFA kwa kuilaza Malakia ya Sudan Kusini kwa magoli mawili kwa moja na kufuzu kwa nusu fainali.Beki wa Uganda, Godfrey Walusimbi ALIGEUKA KUWA MFUNGAJI NA KUTIA WAVUNI MAGOLI MAWILI.Mfungaji matata, Michael Olunga anayesakwa kutokana na ufungajiwake, alimuandalia pasi Walusimbi katika dakika ya 3 nayewalusimbi hakuchelea kuipa Gor uongozi.Gor ilizidisha uongozi wake kupitia Walusimbi KATIKA dakika ya 28 na kuwafanya mashabiki waGor waliokuwa katika uwanja wa kitaifa wa Dar Es Salaam.Kipa Boniface Oluoch ambaye amekuwa na fomu nzuri ya kutofungwa kwa zaidi ya mechi kumi kwenye ligi KUU NCHINI Kenya alifanya vyema langoni kwakuzaba shuti ya David Dada kunako dakika ya 13Kipindi cha kwanza kilikamilika Gor ikiongoza kwa magoli mawili kabla ya Thomas Jacob kuipa Malakia matumaini kwa kuelekezampira uliorushwa na Wisely Arasa's langoni katika dakika 66.Mkufunzi wa Al Malakia, Ramzi Sebit amelaumu usimamizi wa mechi kwa kupoteza.''Mwamuzi hakufaya usimamizi bora wa mechi'' alidai.Mpinzani wake, Frank Nuttal, anayeifunza Gor Mahia, amefurahia ushindi huo huku akiongeza kuwa wanalenga kufanya vyema katika nusu fainali.Gor, iliyoaga Makala ya kombe hilo mwaka uliopita sasa itamenyana na Al Khartoum ya Sudan.Al Khartoum, iliyochukua nafasi ya El Merreikh kuwakilisha Sudan kwenye kombe hilo, iliicharaza APR ya Rwanda kwa magoli manne bila jibu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni