other blog

Jumatano, 29 Julai 2015

Na katika teknologia.. Kampuni ya simu bandia za iphone yavamiwa


Kampuni iliyodaiwa kutengeneza simu bandia 41,000 aina ya Iphones kutoka kampuni ya Appleimevamiwa huko Uchina na watu 9 kukamatwa.Oparesheni hiyo ilishirikisha mamia ya wafanyikazi waliokuwa wakiandaa vipuri vya simu vilivyotumika kama simu mpya aina ya iphone tayari kuuzwa nje,huku simu hizo bandia zikizalisha kitita cha dola miloni 19.Kampuni hiyo iligunduliwa tarehe14 mwezi Mei lakini ikabainika katika mitandao ya kijamii na ofisiya usalama ya umma Beijing siku ya jummapili.Oparesheni hiyo ilianzishwa mwezi wa januari.Uchunguzi huo uliongozwa na kundi la mke na mumewe kaskazini mwa mji mkuu wa Uchina, kulingana na mamlaka yaBeijing.Walisema kuwa walidokezewa na mamlaka ya Marekani ambayo ilinasa simu hizo bandia .Ripoti hiyo inajiri wakati kuna msako wa bidhaa bandia unaotekelezwa na Uchina huku mamlaka hiyo ikiyashinikza makampuni kuweka nembo za ubora wa biadha.Uchina pia imekubali kufanya kazina mamlaka ya Marekani kupunguza kuwepo kwa bidhaa bandia zinazotoka nchi hizo mbili.Mshirikishe mwenzako

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni