other blog

Jumapili, 26 Julai 2015

Steps Entertainment kusaidiana na serikali kupambana na wahalifu wa filamu postead by mr kimario

Meneja Mkuu wa kampuni ya usambazaji filamu Steps Entertainment Bw.Jairaj Almoradan akifafanua jambo wakatiwa mkutano na Sekretarieti ya Bodi ya Filamu Tanzania,wakati wa makubalianoya Utekelezaji wa sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza ya mwaka 1976 kati ya wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo na Makampuni mbalimbali ya Filamu nchini.wa pili kulia ni Afisa uhusiano wa Steps Entertainment Bw. Cloude Ngalaba,wa tatu kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi.Joyce Fissoo ,wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Sekretarieti ya bodi ya Filamu Tanzania.Bi. Angela Ngowi. Mazungumzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Bodi ya Filamu jana jijini Dar es salaam.PICHA NA ANNA ITENDA MAELEZOMwenyekiti wa Pili Pili Entertainment Bw.Nilesh Bhatt akieleza jambo wakati wa mahojiano na sekretarieti ya Bodi ya Filamu Tanzania. wa pili kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi.Joyce Fissoo ,wa kwanzakulia ni Mwenyekiti wa Sekretarieti ya bodi ya Filamu Tanzania.Bi. Angela Ngowi. Mahojiano yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Bodi ya Filamu jana jijini Dar es salaam…………………………………..KAMPUNI ya usambazaji na utengenezaji filamu nchini Steps Entertainment imeahidi kushirikiana na serikali kupambana na wanaokiuka sheria ya filamu na michezo ya kuigiza ya mwaka 1976.Hayo yamesemwa jana na meneja Mkuu wa Steps Entertainment Bw. Jairaj Almoradan jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na Sekretatieti ya Bodi ya filamu Tanzania.Bw.Almoradan amesema kampuni yake haitapokea kazi za wasanii wasiofuata sheria kwa kutengeneza filamu zilizo kinyume na maadili na zilizo kinyume na sheria.Amesema kuwa sheria inawataka kutengeneza filamu zinazofuata maadili na kuwasilisha master kopi kwa ajili ya kuidhinishwa kuingia sokoni.“tutajitahidi kuwaeleza wasanii na tutakuwa wakali kutopokea filamu ambazo tunaona zipo kinyume na maadili na utamaduni wetu.”Amesema Bw. Almoradan.Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Bi. Joyce Fissoo amesema bodi imekuwa ikipata malalamiko kuhusiana na baadhi ya filamu kuwa kinyume na maadili ya Mtanzania.“Sisi kama bodi kazi yetu ni kukaguafilamu na matangazo yake kama yapo kimaadili na yamefata sheria ikiwa ni pamoja na kuzipa madarajafilamu hizo kabla hazijaenda sokoni.”amesema Bi.Fisso

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni